SoC01 Ni wajibu wetu kujitoa kuwasaidia watu wenye mahitaji muhimu katika jamii

Stories of Change - 2021 Competition

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,525
6,470
JF

Katika jamii kuna makundi ya watu mbalimbali, wapo watu wanaojiweza kumudu mahitaji yao yote lakini pia kuna makundi ya watu hawajiwezi kumudu mahitaji yao ya kila siku katika maisha

Mahitaji muhimu katika maisha ya mwanadamu ni Chakula, malazi na mavazi,, katika jamii yetu hii kuna watu wanakosa mahitaji hayo

Makundi ya watu wenye uhitaji zaidi ni
•watoto yatima
•waanga wa majanga mbalimbali
•Makundi ya watu wenye ulemavu
•Wazee
•Wakimbizi
kwa uchache makundi hayo hapo juu yanakosa mahitaji muhimu ya kibinadamu

Hebu jaribu kujiuliza wewe hapo unayejiweza, utayamudu vipi maisha endapo huna chakula?

maisha yataenda vipi bila kuwa na sehemu ya kuishi na nguo ubadilishe kila siku?

Kama ulikuwa hufahamu sasa naomba ufahamu kwamba mimi na wewe hapo tunaowajibu (lazima) kuwasaidia watu hawa wenye mahitaji muhimu katika jamii

Ni muhimu sana kuwasaidia watu hawa kwa sababu zifuatazo
•Kulinda na kuheshimu utu..hakika utu huifadhiwa na upatikanaji wa chakula malazi na mavazi!
• upendo, amani na mshikamano vinadumishwa katika jamii
• Haki za watu wengine kuishi zinaheshimika kupitia msaada wako wewe
• Kiroho,, Mungu naye hutukumbuka na kutuongezea zaidi pale tulipopunguza
• Misaada yetu inapunguza makundi tegemezi katika jamii
• Hupunguza umasikini katika jamii

Ni mtu wa aina gani anatakiwa kuwasaidia watu wenye mahitaji?
Mtu yoyote yule mwenye uwezo anaweza kumsaidia mtu mwenye uhitaji kwani waswahili husema wema usizidi uwezo hivyo saidia kadili ya uwezo wako,,, uwe na kidogo au kikubwa wewe saidia tu

Hapa Tanzania watu wenye mahitaji wengi humkumbuka sana marehemu Reginald Mengi..Hakika huyu mtu aliwajali watu wenye uhitaji

Ni zamu yetu sasa, mimi na wewe tujitoe kuisaidia jamii kwa kuwagusa hawa watu wenye mahitaji

Tutoke tuwatembelee yatima na wazee katika vituo vya kulea wazee na watoto yatima vilivyo karibu nasi

Tutoke sasa tuzitembelee public schools huko kuna watoto wengi wenye mahitaji wanatusubiri tuwawezeshe wafanikishe ndoto zao kielimu na kimaisha

Mwisho, ni wajibu wa kila mtu anayejiweza kuwasaidia watu wenye uhitaji,, pia serikali na taasisi binafsi hazina budi kushirikiana kuhakikisha zinayasaidia makundi haya muhumu katika jamii

nawasilisha
 
Mkuu,umeandika kitu cha maana sana hapa ambacho kama kikitekelezeka basi tutawapunguzia mateso wasio jiweza,

Kila mwenye uwezo akisaidia mtu asiyejiweza au mwenye uhitaji basi tutapunguza sana mateso kwa binadamu wenzetu,

Dunia ni mapito tu,toa kidogo ulicho nacho na Mungu atakulipa,

Big up mkuu,hii thd imegusa maisha ya wenye uhitaji.
 
Kama unapesa kawasaidie wewe tu inatosha mkuu
Kwani kuna mtu amekulazimisha mkuu? Ila tambua kua,Dunia ina zunguka,maisha ni kama gwaride,wambele anaweza kua nyuma na wanyuma anaweza kua mbele,

Ndio maana wahenga wanasema hakuna ajuaye kesho ya mwenzake na wema hauozi.
 
shukrani sana mkuu
Mkuu,umeandika kitu cha maana sana hapa ambacho kama kikitekelezeka basi tutawapunguzia mateso wasio jiweza,

Kila mwenye uwezo akisaidia mtu asiyejiweza au mwenye uhitaji basi tutapunguza sana mateso kwa binadamu wenzetu,

Dunia ni mapito tu,toa kidogo ulicho nacho na Mungu atakulipa,

Big up mkuu,hii thd imegusa maisha ya wenye uhitaji.
 
Back
Top Bottom