KWELI Baadhi ya chura tunaokutana nao majumbani wana sumu inayoweza kukuua

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Wakuu,

chura.jpg

Kuna video nilikutana nayo huko mtandaoni (nimeangalia sijaiona), huyo dada alikuwa anasimulia jinsi rafiki yake alivyokufa baada ya kung'atwa chura. Chura huyo alikuwa ndani ya kiatu chake, wakati anavaa hakumuona, basi huyo chura akamng'ata kwenye kidole baada ya kushtuka (unajua jinsi wadada tunaogopa wadudu) akamtoa kwenye kiatu na kuvaa na kuendelea na kazi zake.

Baada ya siku mbili yule dada akaumwa, homa kali ikamshika kumpeleka hospitali ndio ikaonekana ni hiyo sumu ya chura, na imeshambaa mwilini kiasi ambacho hakuna msaada tena. Mwisho dada alikuwa anakoroma kama chura (kama vile inavyotokea mtu aking'atwa na mbwa mwenye kichaa) mwishowe akafa.

Sasa wakuu mimi nauliza, hawa chura tunaopishana nao majumbani ndio wana sumu kali hivi au kuna aina ya chura ndio wanasumu kali hivyo?
 
Tunachokijua
Chura ni mnyama wenye Uwezo wa kuishi majini na nchi kavu. Mara nyingi vyura wanapatikana zaidi sehemu zenye majimaji, moyoni, kwenye maziwa na mabwawa.

Chura huwa na ngozi laini, rangi mbalimbali, na wana uwezo wa kuruka kwa kutumia miguu yao ya nyuma.

Pamoja na kupatikana zaidi kwenye mazingira yenye maji, ni kawaida baadhi ya aina ya vyura kupatikana kwenye makazi ya watu hususani nyumba zilizo karibu na madimbwi ya maji au mitaro.

Kumekuwa na maswali ya wadau wakihoji kama chura anasumu inayoweza kumuua binadamu. Mleta mada hii anadai amewahi kusikia simulizi ya mtu anayedaiwa kung'atwa na chura na baadaye akafariki.

Upi kweli wa hoja hii?
JamiiCheck imewasiliana na mtaalamu Tito Lanoy Mhifadhi na Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka ambaye anabainisha kuwa katika mazingira ya majumbani kuna vyura wa aina tofauti, wapi wenye sumu na wengine hawana. Akiifafanulia zaidi JamiiCheck Lanoy anasema:

Chura wakikung'ata hawana sumu ila ukishuka yale maziwa wanayotoa na kuyalamba ndiyo Yana sumu. Kuna baadhi ya vyura ukiwashika wanatoa majimaji yanayofanana na maziwa hao ndiyo chura wenye sumu. Majimaji hayo hutokea juu ya ngozi ya karibia na macho na huyatoa kwa madhumuni ya kujilinda wanapohisi hatari au kusogelewa na adui.
Sumu ya chura haimpati Binadamu kwa kung'atwa bali mpaka uishike majimaji hayo na kuilamba au kuyaingiza mdomoni.
Ikitokea umemshika chura Kisha akatoa maji hayo, unashauriwa kunawa mikono mapema ili kuepusha madhara ya sumu.
Si vyura wote wanatoa hayo maziwa maana wapo vyura wanaoliwa. Kuwatambua vyura wenye sumu na wasio na simu kunahitaji utaalamu hivyo unashauriwa unapoona chura maeneo ya kwako usimchezee ili kuepuka kukutana na vyura wenye sumu.
Navyoelew chura wenge slim body ndo wanasumu especially wale wa njano,

Wataalam wanakuja kufafanua zaidi
 
Izo ni story za utotoni ukuumwa na mbwa mwenye kichaa na ww unabweka km mbwa.

Ukiumwa nanchura na ww unalia km chura hapana apo nimekataa ila suala la sumu ni kweli chura wanasumu ila sumu yake huwa na madhara kwa wadudu na wanyama wadogo,

ila kwa binaadam sjui kwakwel
Ila kwa uelewa wangu Sumu nying za wanyama ni ngumu kuua binaadam.

Hata nyoka sio wote wanasumu yenye ngumu kubwa kuua binaadam.
 
Duh! Ila chura wengi wana poison ila hawana venomous, ni kumaanisha hawana uwezo wa kutoa sumu kwa njia ya meno, labda alimshika bila kujua na mkono ukaenda kwa mdomo.
 
Izo ni story za utotoni ukuumwa na mbwa mwenye kichaa na ww unabweka km mbwa,
Ukiumwa nanchura na ww unalia km chura hapana apo nimekataa ila suala la sumu ni kwel chura wanasumu ila sumu yake huwa na mazara kwa wadudu na wanyama wadogo ila kwa binaadam sjui kwakwel
Ila kwa uelewa wangu Sumu nying za wanyama ni ngumu kuua binaadam ata nyoka sio wote wanasumu yenye ngumu kubwa kuua binaadam.
Hilo nimewahi kusikia pia, ngoja tuulize hapa hapa wataalamu wa JamiiCheck watueleze kuhusu hilo.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom