Ni hasara gani kubwa ulishawahi kuipata ikakurudisha nyuma?

Mkuu ningependa ushauri zaidi hapo kwenye ku deal na mafundi haswa ukiwa mbali. Mimi niko Scandinavia na kwa kweli naogopa hata kutuma hela ya kununulia kiwanja achilia mbali kujenga kwa sababu nishasikia hizi habari za ndugu/ marafiki kutokuwa waaminifu. Hili limenipa wakati mgum maana nakuwa nabaki na hela mkononi tu na likizo zenyewe ni siku 25 kwa mwaka kiasi ambacho huwezi kwenda bongo na kufanya la maaana
Waaminifu tupo sana tu sema nyie wakuu mnawaamini masharobaro watu wa mjini maneno mengi utafikiri kameza memory card

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nlijichanga zikafika m3 nikafungua kibanda cha tigo pes , Mpes na Airtel money nikaweka msichn apo mm nikaendelea na kaz zangu baada ya mwez faid ilikua lak moja na sabini ,,, baada ya wiki 1 mbele akatapeliwa laki 4, baada ya siku 2 tena akatapeliw lak 7,,,, nikafunga kibanda nikakiuza nikauza na lain zote nikaachan na iyo biashar sas nimeanzsh nyingine

Sent from my iPhone using JamiiForums
huyo msichana kama hajakufanyia usanii basi zoba.
 
Nilienda ifunda tech nikiwa na div one ya 10 nikamaliza nina div 3 ya 15.
Hii ndio hasara kubwa maishani mwangu, SITOSAHAU.
Nimecheka sana ..
Mkuu imebidi ni-screen shot kabisa hii post yako.
Imebeba ujumbe mzito sana, ipo siku nitakuja kuwasimulia au kuwaonesha watoto wangu.
 
Dada yangu mmoja(wa kufikia) alikuwa amejenga maeneo ya Ulongoni, baada ya kuona fursa kwenye ufugaji wa kuku nikamuomba nitumie kiwanja chake kwa muda kwa ajili ya kufugia. Mwenyewe hakuwa na wazo la kuki-utilize kwa namna yoyote. Akanikubalia, nika-save nikafikisha kama 2.5M, nikajenga mabanda, nikaenda kuku project nikachukua vifaranga kama 300 vya kuroiler, nikamleta mdogo wangu amemaliza form six nikampangishia chumba pale kwa dada nikamkabidhi project.

Picha linaanza kuku wanapoanza kuwa kuku, kila mtu anamsifia dada kwa project, maana hawakujua kama ni yangu, mwenyewe sikuwa naenda pale mara kwa mara. Majirani na wageni wakajua dogo ni mfanyakazi wa dada na project ni ya dada. Kila mtu akampongeza dada kwa kujiongezea kipato kwenye kuku. Kuku wakaendelea kupendeza bana!!! Dada akaanza visa, mara sijui dogo hamsalimii, mara sijui hampi hela, mara sijui dogo ana kiburi, mpaka akamfukuza pale kwake. Ikabidi nitafute room ingine pale jirani kwa ajili ya dogo.

Ile kuku wanafikisha miezi minne na nusu, sikuwa nimepanga kuwauza nilitaka watage nitotoleshe nipanue project. Mpaka hapo nmeshatumia karibia 5.5M (ile kujenga mabanda, kununua kuku, usafiri, chakula, madawa na expenditures za dogo pale).

Ghafla kuku wakaanza kuugua, wanakufa ovyo ovyo. Dogo akaripoti kwa daktari akatafuta ugonjwa akaukosa, akaomba apelekewe mzoga mmoja wa kuku aliyekufa kwa aina ile. Bwana bwana, ile Daktari kuchunguza akakuta viashiria vyote vya sumu kwenye njia ya hewa. Kuku walikufa wote mwisho wa siku.. Iliniuma sana,5.5M of my hardly earned money, sijawahi kusimamisha tena ile project mpaka nipate shamba langu mwenyewe...
Huyo dada yako ni zaidi ya mnyama Dubu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msimu wa korosho 2018/2019 tulishauriana na jamaa angu mmoja kununua korosho kwa mfumo wa 'kangomba' then tuziuze kwa wanunuzi wakubwa ..yy aliwahi kufanya hivyo miaka miwili kabla na ilimlipa..nikaweka 4m ,tukanunua fresh kupitia kwa jamaa ambaye yupo huko na mzigo ukapelekwa ghalani..picha linaanza wanununz hawajafika bei..sisi tulinunua kilo 2500 ,bei ya kwanza ikawa 2700 kama sikosei,wakulima wakagoma then serikali ikaingilia kati ,hapo picha ndio ikanoga sasa,..tumwa wanajeshi huko yakafuata mauhakiki kama hamsini vile bahati nzuri tuliuzia kwa jina la mtu ambaye ni mkulima mkubwa so at least uhakiki haikusumbua ,baadae mkuu akasema atalipa watu wote tu hata wa 'kangomba' hapo kidogo amani ikarudi ...hii ni may 2020 hata senti sijapata na haina hata dalili ya kwamba tutalipwa ..plus hii corona ndio kabisa imekula kwetu dah!

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah hii ni zaidi ya balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dada yangu mmoja(wa kufikia) alikuwa amejenga maeneo ya Ulongoni, baada ya kuona fursa kwenye ufugaji wa kuku nikamuomba nitumie kiwanja chake kwa muda kwa ajili ya kufugia. Mwenyewe hakuwa na wazo la kuki-utilize kwa namna yoyote. Akanikubalia, nika-save nikafikisha kama 2.5M, nikajenga mabanda, nikaenda kuku project nikachukua vifaranga kama 300 vya kuroiler, nikamleta mdogo wangu amemaliza form six nikampangishia chumba pale kwa dada nikamkabidhi project.

Picha linaanza kuku wanapoanza kuwa kuku, kila mtu anamsifia dada kwa project, maana hawakujua kama ni yangu, mwenyewe sikuwa naenda pale mara kwa mara. Majirani na wageni wakajua dogo ni mfanyakazi wa dada na project ni ya dada. Kila mtu akampongeza dada kwa kujiongezea kipato kwenye kuku. Kuku wakaendelea kupendeza bana!!! Dada akaanza visa, mara sijui dogo hamsalimii, mara sijui hampi hela, mara sijui dogo ana kiburi, mpaka akamfukuza pale kwake. Ikabidi nitafute room ingine pale jirani kwa ajili ya dogo.

Ile kuku wanafikisha miezi minne na nusu, sikuwa nimepanga kuwauza nilitaka watage nitotoleshe nipanue project. Mpaka hapo nmeshatumia karibia 5.5M (ile kujenga mabanda, kununua kuku, usafiri, chakula, madawa na expenditures za dogo pale).

Ghafla kuku wakaanza kuugua, wanakufa ovyo ovyo. Dogo akaripoti kwa daktari akatafuta ugonjwa akaukosa, akaomba apelekewe mzoga mmoja wa kuku aliyekufa kwa aina ile. Bwana bwana, ile Daktari kuchunguza akakuta viashiria vyote vya sumu kwenye njia ya hewa. Kuku walikufa wote mwisho wa siku.. Iliniuma sana,5.5M of my hardly earned money, sijawahi kusimamisha tena ile project mpaka nipate shamba langu mwenyewe...

Jamani!...ulifanikiwa kumwambia?
 
Back
Top Bottom