Ni hasara gani kubwa ulishawahi kuipata ikakurudisha nyuma?

JUzi tu imenipiga Ng’ombe 4nimefunga kwa muda nasubiri mfungonuishe ila hii ndogo wala haijaniuma 2010 hadi 2018 nimepoteza 100m kwenye kujaribu biashara tofauti tofauti. nashukuru wote tuko salama na MKE wangu Dinia Ina mambo inawezekana hii kwa winginenikawa ni ndogo
Pole sana ni pesa ndefu sana .ni biashara zipi hizo mkuu..?? Au usimamizi/mbovu?
 
Soo tukio la Mara nilianza baa. Then hostel. Then matofali ya press then nguruwe then baa tena na mm sikomagi then kuzoa taka mtaani
Mikoa ya Arusha Pwanu Tanga DarKWA HIYO NINAUZOEFU WA KUTOSHA WA BIASHARA.
 
Na nitazirudia zote mbele ni sijakubali mambo ni mengi kuna usimamizi. Na kijana kikazi kila Mara Sasa nimeacha kz naona mapadiliko HAWEZI Tunisian mabwana wawili
 
Ila mkuu hakuna kitu kizuri Kama kuitwa boss....
Mimi vibarua walikuwa wananambia boss usijal tuachie hiz kaz zote za shamba tutafanya ss...nikasema hapana kila kazi lazima mkono wangu nami upite ili nijue uzito wa kazi unaendana na pesa ninayo toa..
nimekumbuka kipindi nauza chipsi na jamaa mmoja ambae nilimuajili akawa ananiita bosi kila siku chipsi zinalala m@maeee , nikawa najiona fahariiii kumbe napoteza, chipsi zikilala kesho zinakua mnato.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilijibana hela ya boom nilipomaliza chuo nikawa na vihela bahati nzuri nilivyomaliza tu nikapata sehemu ya kujitolea nalipwa kidogo,basi bwana nikaanza tubiashara cha nguo za ndani za wadada nilianza na mtaji wa elfu 70 sikutaka kuwekeza hela zaidi mtaji hadi ukafika laki 3.

Mara paap sister angu alikopa mkopo bank akashindwa kurudisha kwa wakati nyumba yake ikataka kuuzwa na bank ikabidi tukae kikao kama familia tumuokoe ndugu yetu nikatoa pesa yoote baasi na biashara ikaishia hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msimu wa korosho 2018/2019 tulishauriana na jamaa angu mmoja kununua korosho kwa mfumo wa 'kangomba' then tuziuze kwa wanunuzi wakubwa ..yy aliwahi kufanya hivyo miaka miwili kabla na ilimlipa..nikaweka 4m ,tukanunua fresh kupitia kwa jamaa ambaye yupo huko na mzigo ukapelekwa ghalani..picha linaanza wanununz hawajafika bei..sisi tulinunua kilo 2500 ,bei ya kwanza ikawa 2700 kama sikosei,wakulima wakagoma then serikali ikaingilia kati ,hapo picha ndio ikanoga sasa,..tumwa wanajeshi huko yakafuata mauhakiki kama hamsini vile bahati nzuri tuliuzia kwa jina la mtu ambaye ni mkulima mkubwa so at least uhakiki haikusumbua ,baadae mkuu akasema atalipa watu wote tu hata wa 'kangomba' hapo kidogo amani ikarudi ...hii ni may 2020 hata senti sijapata na haina hata dalili ya kwamba tutalipwa ..plus hii corona ndio kabisa imekula kwetu dah!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu serikali hadi kufikia wiki iliyopita imelipa hela zote kwa wakulima ambao hawakulipwa msimu huo kuna uwezekano huyo mtu mliyemtumia aliwapiga tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NliFungua biashara nikaangukia pua, sikuchoka nikafungua nyingine napo nikaanguka tena,, hadi leo nimekuwa na moyo mzito wa kufanya biashara,

Kuna mwamba ananishauri nianze biashara ya mchele napo roho inasita,

Mwangine ananiambia nunua bodaboda,

Biashara ya nguo nliwai ifanya ila sasa wanawake ni adui sana ktk hii biashara,,





Sent using Jamii Forums mobile app
Elezea vizuri wanawake ni adui kivipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilimo cha matikiti nilikuwa inspired sana na jamaa moja kuwa kitikiti linalipa sana ukiweka 2m unaweza pata return ya 5m nikaona fursa ndo hii niliweka 4m tena ilikuwa pesa ya mirathi ya mama yangu nilichoambulia ni kipande cha tikiti kimoja pesa hata matikiti kumi sikupata

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole mkuu, kwa kuwa tunajifunza, ungeweka mkasa mzima, namna ilivyokutokea hadi kupelekea kuzama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika maisha mpka utoboe ni mtihan mkubwa
Mimi nilianza biashara ya usafirishaji nilianza na magari madogo focus yangu ni kupanuka zaid ...Nikajikusanya mpka nikapata million 47 kuna mshirika mwenzagu ambae alikua pia anafanya biashara hii ila yeye alikua ameshaendelea sana pia mzoefu ana magari makubwa mawili nikamshirikisha malengo yangu ya hii million 47 niliyokusanya nahitaji kununua Fuso kama mjuavyo mambo ya magari lazima utapata ushauri tofauti tofauti..zikapatikana gari 2 Dar kwa kua huyu jamaa alikua na safari ya dar tukakubaliana akifika atenge mda kwa ajili ya kukagua hzo gari mbili ..Jamaa alikagua magari na mwisho tukachagua moja baada ya yeye kuisifia lakin pia mm kwa picha ilionekana safi kabisa ...na kwa sababu jamaa anayajua magari sikutilia shaka kabisa ...picha lina anza jamaa akaniambia kuna gari yake moja anauza Fuso hzi za mchanga akashauri liletwe kwangu akpatkana mtu wa kununua awe anakuja kulikagulia kwangu kwa sababu tuna aminiana nikamwambia haina shida wambie vijana walilete.....Huko Dar sasa nikamtumia hela alipie gari na kupata document zote pia kuna nyumba yangu nilikua najenga nikaona kwa sababu gari linakuja kutoka dar kwa nn nisiagize baadhi ya material ambayo yanapatikana dar kwa bei nzuri ..basi nikamtumia million tatu kwa ajili ya vitu vya nyumba..! Kesho yake jamaa kanitumia picha kunionesha wanavopakia mzgo ..picha za mzigo ukiwa umefungwa tyari.! kufupisha story ....Aisee baada ya hapo mpka kesho Gari na mzgo wake havijawahi fika Mara ya mwisho alinambia wamepata breakdown Dodoma.....

Saa hvi nimekua na roho mbaya likija swala zima LA pesa yangu
Mungu ni mwema napambana kusimama tena Japo Corona nayo ni kama inanichimbia kaburi mambo yamevurugika

Sent using Jamii Forums mobile app
hiyo ndio faida ya uvivu, ungeinuka wewe na yeye wote muende dsm ukalipie na kuondoka na hilo gari wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom