Nebukadneza: Mbabe wa vita, muabudu sanamu aliyekula majani kama ng’ombe (part 2)

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,671
4,925
Kama nilivyowahaidi kuwa itaendelea, kwa wale mlioanza na sehemu hii 👉🏽 Nebukadneza: Mbabe wa vita, muabudu sanamu aliyekula majani kama ng’ombe

Basi inaendelea kama ifuatavyo;

Baada ya Mfalme Sedekia kuuawa, sasa Yehoyakimi akachukua nafasi hiyo ya kuiongoza Yuda (Israel). Hapa kuna kitu ambacho watu wanatakiwa kufahamu. Tuliona kulikuwa na mataifa mengine yaliyokuwa yakipingana na Babiloni chini ya Nebukadneza.

Mataifa hayo yalikuwa mengi lakini yalikuwemo Syria na Palestina. So hapo unaona kulikuwa na nchi iitwayo Palestina na pia kulikuwa n Yuda ambao ndiyo Waisrael. Na wote hao walikung’utwa na Nebukadneza na kufanywa mateka.

Huyu Nebukadneza anafanana stori na jamaa aitwaye Nabonibo. Ukisoma kitabu cha Biblia na vya historia vingine vimemtambua kama Nebukadneza lakini ukisoma vitabu vingine vya dini, kuna mtu anajulikana kama Nabonido. Sasa wengi wanahisi kwamba huyu Nabonido ndiye Nebukadneza, hapana. Ni watu wawili tofauti waliokuwa na maisha ya kufanana tu.

Nebukadneza alikuwa mbabe wa vita, baada ya kuona ameishambulia Yuda, Palestina, Syria na mataifa mengine, sasa akaondoka na kwenda kupigana vita na mfalme Tiro huko Foenike. Vita hivyo vilipiganwa kwa miaka 13 (Soma kitabu cha Ezekiel 29:18 wamemzungumzia sana Tiro mpaka kupigwa kwake na Nebukadneza)

Hapa najua unaweza kujiuliza kwamba kwa nini huyu Nebukadneza alikuwa na nguvu kubwa? Jibu ni moja tu kwamba Yuda walikuwa wanaadhibiwa kwa mambo yote waliyokuwa wameyafanya.

Kulikuwa na sababu zilizomfanya Mungu kuwaadhibu kupitia Nebukadneza. Kwanza ilikuwa ni kutokumuamini tena yeye, watu wakachonga masanamu na kuanza kuyaabudu.

Ngono ikasambaa kila kona, yaani watu walikuwa wakizini mpaka vibarazani, watu walifanya uzinzi mpaka na ndugu zao. Pia watu waliwafanyia matambiko watoto wao wa kuwazaa, kwa hiyo Yuda na Samaria zote zikanajisiwa, sasa Mungu akamuinua Nebukadneza ili kuwaadhibu.

Nebukadneza ambaye alitoka katika taifa la waabudu masanamu, akawa na nguvu kubwa kuliko hata Yuda.

Ukisoma Biblia hasa kitabu cha Ezekiel, ni kama kwa kipindi hiki silaha kubwa ya Mungu dhidi ya mataifa mengine ilikuwa ni Nebukadneza! Kwa nini? Sababu Tiro alipigwa kwa kuwa tu waliucheka mji wa Yerusalemu.

Waliukejeli mji ule, waliutolea maneno machafu na hivyo Mungu akampa roho Nebukadneza kuona ni sahihi kwenda kupambana na Tiro. Haikuwa vita ya kawaida, ilidumu kwa miaka hiyo 13.

Huyu Nebukadneza, kutokana na maguvu aliyokuwa amepewa na Mungu, hata naye Mungu alimuita mfalme wa wafalme, mfalme aliyetawala watu mpaka wanyama.

Ukiachana na hayo kama nchi lakini pia huyu mfalme Tiro alikuwa na makosa yake kemkem, soma Ezekiel 28. Alilaaniwa na kuambiwa angepigwa sana mpaka kusikia aibu. Mwisho wa vita, mfalme huyo alitekwa na kuuawa mbele za watu, kilikuwa ni kifo cha aibu sana kama mfalme.

Nebukadneza alijulikana kama mfalme mwenye nguvu, aliijenga Babiloni kwa kutumia kodi za mataifa ambayo yalikuwa chini yake yakiwemo Yuda na Palestina.

Alirudisha na kukarabati mahekalu ya kale katika majiji ya Babuloni ili kupata utegemezo wa makuhani wa Babiloni.

Pia alitayarisha umwagiliaji wa kawaida wa nchi za Babiloni kupitia mtandao mzima wa mifereji iliyounganishwa na Eufrati. Katika utawala wake ufalme wa Babeli mamboleo ulifikia kilele cha ukuu wake.

Katika vitabu vingine vya historia vilimtaja Nebukadneza kuwa katili kupitiliza. Alikuwa anamchukua sungura, anamchuna ngozi na kumla hivyohivyo akiwa na uhai wake.

Ukiachana na hilo, pia zile falme ambazo alizitawala, aliwalazimisha wafalme kuwa machoko. Watawala wa Kirumi kama Tito na wengine walijikuta wakiingia katika suala lake hilo la uchoko.

Pamoja na kuweka wafalme wengi na kuwamaliza, pia mwisho wa siku akaamua kumuua mfalme wa Yuda, Yehoyakimu na mwili wake kuwatupia mbwa.

Hayo yote aliona kama hayatoshi, akawalazimisha watu wamuite Mungu. Wakati akimuweka Sedekia kuwa mfalme wa Yuda, aliwataka wafalme watano wawe chini ya Sedekia. Kuna kipindi wafalme hao walipanga njama za kummaliza Nebukadneza lakini walishindwa kwa kuwa Sedekia alikwenda kuwachoma kwa Nebukadneza.

Kwa hasira, akawachukua wafalme hao watano na kuzifunga nywele zao kwenye mikia ya farasi na kuwaamuru wakimbie kutoka Yuda mpaka Lida, umbali wa zaidi ya kilometa 35.

Pamoja na ujinga wake mwingi lakini Nebukadneza alikuwa akiwaheshimu Wayahudi kwa kuwa aliamini Mungu wao alikuwa wa kweli.

Aliwachukua Daniel, Shadraki na Abednego kwa kuwa alitambua nguvu za Mungu wao, akawaweka karibu naye kwa ajili ya kutafsiri ndoto na maono yake.

Alipewa nguvu na kila kitu ila siku moja baada ya kukaa katika paa la nyumba yake, aliiangalia Babiloni jinsi ilivyopendeza, hapo akajisifia, akasema utukufu wote na uwe kwake. Hilo likamkasirisha Mungu na hivyo kumtupa mbali kabisa, akakosa watu, akaishi porini na kuanza kula majani kama ng’ombe kwa miaka saba.

Baadaye akaangalia mbinguni, kwa mara ya kwanza akamuomba Mungu wa kweli, hiyo ikawa almanusura yake, akarudishwa na kuendelea na maisha yake kama kawaida.

Hakuna marefu yasiyo na ncha. Wanajeshi wa Babiloni wakapigwa na Euphrates huko Zazana. Nebukadneza akakimbia kurudi Babiloni na baadhi ya wanajeshi wake. Huko, akakutana na mtu aitwaye Darius ambaye akamteka na kumchinja kama kuku.

Ukawa mwisho wake. Alikufa akiwa anamjua Mungu wa kweli ni yupi baada ya kuabudu sana masanamu.

Habari yake zaidi inapatikana kwenye kitabu cha Daniel na Ezekiel.
 
Ahsante sana Mkuu , ni Elimu na Burudani pia ..
 
Mkuu Mhaya,
Unasema Nebukadneza alitupwa mbali kabisa na kukosa watu, akaanza kuishi porini miaka Saba huku akila majani kama Ngo’mbe. Je kipindi alichotupwa akiwa anakula majani kama Ngo’mbe ni nani alikuwa akitawala? Walifanya jitihada gani kumtafuta?

somehow it’s a nice story but there’s puzzle that miss between.
 
Back
Top Bottom