mjenziwakale
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 738
- 967
Salaam,
Katika harakati zangu za kusaka tonge, yupo jamaa ambae nilifahamiana Naye katika biashara, tukawa tumezoeana hadi ikafikia kipindi akiwa na shida na hela namuazima ila anaacha gari yake kama bond, akienda akasupply mizigo yake akilipwa ananirejeshea pesa zangu na yeye anachukua gari yake.
Sasa zamu hii nilimpatia pesa milioni 8 akaniachia gari yake Range Rover namba B akiahidi atarejesha baada ya mwezi mmoja akishalipwa na hiyo halmashauri anakosupply mzigo.
Sasa yapita miezi karibia 6 toka achukue hela na gari lake lipo hapa limelala kila Nikimdai pesa yangu ananambia hajalipwa bado, na hili gari hatujaandikishana kwamba akishindwa kulipa gari iwe mali yangu, binafsi sijawahi kumiliki gari na gari lenyewe nikisema niwe nalitumia kupooza machungu siwezi sababu gari inakula mafuta sana hii.
Imefikia hatua namdai ananambia anatafuta mteja akaliuze hili gari aweze kunilipa hata hvo naona kama sound tu. Nimefikia hatua kumwambia walau anilipe tu nusu ya pesa yangu nilompatia na nusu itakayobaki nihesabu hasara tu ili niweze na mm kulipa madeni yanayoniandama ila bado anadai hela hana coz hajalipwa bado.
Wakuu nafanyaje hapa?