Naomba kufahamu namna ya kupata pesa ya NSSF baada ya kazi kuisha

Ebwana kwa uelewa wangu Mwanachama atapata mafao yake endapo ataachishwa kazi kwa sababu yoyote ile isipo kuwa kuacha kazi yeye mwenyewe hapo atakuwa hana sifa ya kupata mafao, pili mwanachama atapata mafao yake endapo atafikisha umri wa kustaafu kwa hiari miaka 55-59 kwa hiari na miaka 60 kwa lazima. Na ili uweze kupata mafao yako unatakiwa kuwa na kitambulisho chako cha uanachama, barua ya kuachichwa kazi, kitambulisho cha NIDA, uthibitisho kutoka Mahakamani, Akaunti ya benki ambayo ipo inafanya kazi pamoja na mambo mengine utaambiwa hapo.
Uthibitisho wa mahakama toa hiyo kitu haitakiwi,

Nakala zinazohitajika ni:
-Kitambulisho Cha NSSF
-Cheti Cha utumishi
-Barua ya kuachishwa kazi
-Kitambulisho/ namba ya NIDA
-Bank statement.

Baada ya hapo ndani ya wiki mbili atakuwa kashapata hela yake, Ila hili ni kwale wasio na taaluma maalum.
 
Back
Top Bottom