Namna mvuto unavyo athiri maisha yetu

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,869
9,696
Je, ulishawahi kujiuliza kwanini wahudumu wote wa mlimani city ni pisi kali?

Kwanini asilimia kubwa ya wahudumu wa ndege (air hostes) ni pisi kali?

Kwanini wahudumu wa Baa asilimia kubwa ni pisi kali?

Kuna siri gani haswa? Je, mvuto ni sura (muonekano wa nje)? Mvuto ni kitu gani? Mtu mwenye mvuto anasifa zipi?

Kwa maoni yangu mvuto ni ile hali ya kupendwa na watu wanaokujua na wasiokujua kwa kutumia muda wao kukufuata au kuwa karibu na wewe huku wakikufikiria kwa mazuri.

Je, una marafiki?

Unapofika sehemu yeyote watu hukufuata au hukukwepa?

Je Unapofika nyumbani baada ya kutoka kazini watoto hukupokea kwa kukukimbilia? Au kila mmoja huingia mitini?

Usichoke twende taratibu
GridArt_20240515_175836439.jpg

Chukulia mfano wewe ni huyo hapo katikati pichani mwenye rangi nyekundu, mstari unaokuunganisha wewe na mtu mwingine ni wa kufikirika namaanisha katikati ya wewe na mtu kuna kamba ya kufikirika inayokuunganisha wewe na mtu kwa lugha ya kikemia tunaita bond.
Ili umvute mtu ni lazima uwe na nguvu iitwayo mvuto. Kwa mfano ili msanii awavute mashabiki ni lazima awe na mvuto bila kujali uzuri wa nyimbo zake. Ili mwanasiasa akubarike na watu wengi ni lazima awe na mvuto bila kujali uzuri wa sera zake.

Nguvu iitwayo mvuto ndio humpa mtu umaarufu.

CASE STUDY
1. Mandonga vs kaoneka
2. Harmonize akiwa nje na ndani ya wsafi
3. Diamond kufanya collabo na Davido

Je kuna aina ngapi za mvuto?

Kwa maoni yangu kuna aina tatu za mvuto
1. Mvuto wa kuzaliwa
2. Mvuto bandia

Mvuto wa kuzaliwa huu ni mtu huzaliwa nao na huonekana tangu utotoni. Mfano mtoto mdogo anayepiganiwa na kila mtu ambebe

Mbuto bandia ni mvuto wa kiujanja ujanja na kona nyingi nyingi. Huu mvuto hutegemea mtu mwenye mbuto wa kuzaliwa.

Kivipi?

Mfano pichani hapo juu ni mtu mwenye mvuto wa kuzaliwa. Ghafla anatokea mtu mjanja anaenda kusimama nae katikati huyo mwenye red color, automatically na yeye anakuwa na mvuto lakini ni mvuto wa muda.

Mfano
MO na SIMBA
GSM na YANGA
CCM na DIAMOND (kampeni za uchaguzi).

Je utaupata vipi mvuto na kuufanya ukunufaishe.

Tafuta mtu mwenye nguvu ya mvuto simama naye kati kati kisha mtumie kujinufaisha katika njia inayofaa isiyoumiza mtu.

Mfano kama una duka mtafute mtu mwenye mvuto ambaye hajajijuua kama anamvuto mtumie akuuzie kwa kumpa ajira.

Oa mke mwenye mvuto (usichanganye mvuto sio sura peke yake) trust me maisha yako yatabadirika.

Kama hauna ramani mtafute mtu mwenye mvuto mfanye awe mtu wako wa karibu utanufaika.

Haya ni maoni yangu je wewe unaelewa nini kuhusu mvuto?
 
Hapa sasa mtaanza kutumia uchawi kuiba nguvu za wengine.

Kila mtu atumie vipawa vyake kuishi.

Kama umepewa kipawa cha mvuto kitumie kufanikiwa, na kama hauna mvuto basi tumia vipawa vingine ulivyonavyo na wewe ufanikiwe pia.

Usitumie nguvu ya mtu au vipawa vyake kujineemesha bila ridhaa yake. Huo ni wizi na ujambazi.

Ni mapepo tu ndio yanayoishi kwa kuiba nguvu za watu. Usiwe kama pepo. Jitegemee.

Cc : NAMBA MOJA AJAYE NCHINI DR Mambo Jambo
 
"Kwa mfano ili msanii awavute mashabiki ni lazima awe na mvuto bila kujali uzuri wa nyimbo zake. Ili mwanasiasa akubarike na watu wengi ni lazima awe na mvuto bila kujali uzuri wa sera zake"

HAPO 👆 umepuyanga mkuu, kwamba mwanasiasa ili akubalike na wananchi ni lazima awe na mvuto bila ya kujali uzuri wa sera zake????? 🤒 😎

BIG NO!!!!!
 
Je ulishawahi kujiuliza kwanini wahudumu wote wa mlimani city ni pisi kali?

Kwanini asilimia kubwa ya wahudumu wa ndege (air hostes) ni pisi kali...
Nilitabiriwa makubwa utotoni Hadi ukubwani!!

Kitaa wale wazee chama wale wenye kutaka kusikia muelekeo wa kiuongozi huko tunapoenda hupenda kunisikiliza!!

Mimi ni scientist lakini nikikaa na vijana was artists hata kama hawasomi hiyo chemistry wanapenda kukaa na kunisikiliza jinsi ninvyo relate equations na everyday life!wanafurahi sana!!

Wengine "Nyerere",waziri"kiongozi,mkuu Hadi wale wasionijua online wanatabiri live live kwamba hivi au vile !aiseh mvuto!!

Sasa Kuna wahuni nikiwa mdogo wakataka ku sepa na Mimi aiseh!!waliuguza Hadi Mzee akakata tamaa!!

Kuna ndoto akaota then alipoifanyia kazi siku ya pili ndio ndio akakuta nipp fresh!!

Wenye uwezo au nyota kubwa kubwa wanawindwa sana na Wana majaribu makubwa sana maishani !!

Ni vile tunajitahidi kujiunganisha na supernatural power iitwayo Mungu Mwenyezi,Maombi na sadaka yakiwa SI unit!

Watoto kunikimbilia,watu kunisikiliza pale ninapoongea!!halafu uwezo was ku explain something out of nothing to consider about!!

Tunapambania ndoto zetu zitimie kiroho na kimwili!!

Mungu atubariki!
 
"Kwa mfano ili msanii awavute mashabiki ni lazima awe na mvuto bila kujali uzuri wa nyimbo zake. Ili mwanasiasa akubarike na watu wengi ni lazima awe na mvuto bila kujali uzuri wa sera zake"

HAPO 👆 umepuyanga mkuu, kwamba mwanasiasa ili akubalike na wananchi ni lazima awe na mvuto bila ya kujali uzuri wa sera zake????? 🤒 😎

BIG NO!!!!!
Lowassa anazungumza dakika 3 tu, Elimu, Elimu, Elimu... Angalia mapokeo ya wananchi
 
Mvuto mwenzake nyota
Nyota yako ikiing'aa lazima ukubarike

Note; kuna baadhi ya watu hutumia nguvu za kiganga ili wakubalike
 
Basi mie wakati nasoma hapa, nikawaza eti mwisho nitakutana na dawa ya mvuto kwa sie tusiokua na mivuto

Hapa sasa mtaanza kutumia uchawi kuiba nguvu za wengine.

Kila mtu atumie vipawa vyake kuishi.

Kama umepewa kipawa cha mvuto kitumie kufanikiwa, na kama hauna mvuto basi tumia vipawa vingine ulivyonavyo na wewe ufanikiwe pia.

Usitumie nguvu ya mtu au vipawa vyake kujineemesha bila ridhaa yake. Huo ni wizi na ujambazi.

Ni mapepo tu ndio yanayoishi kwa kuiba nguvu za watu. Usiwe kama pepo. Jitegemee.

Cc : NAMBA MOJA AJAYE NCHINI DR Mambo Jambo
Anza na hawa
8AA-941x1024.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom