Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Empress_sheila

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
293
335
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka 9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule.
 
Kwa nini mnafosi watoto wasome private schools kuanzia primary?

Kama hana pesa unadhani mahakama itamfunga?

Na btw kesi za namna hiyo haziendi mahakamani zinaenda ustawi wa jamii ambako sana sana mtashauriwa mumpeleke shule ambayo inaendana na kipato chenu..
 
Shida ya ndoa nyingi Zina matatizo hayo mkishaachana tu matokeo ni kwa mtoto ndio atakaepata shida na tuwe makini Sana na hili jambo na Hawa mama zetu Wana tabia ya kumpa maneno mtoto ya kumjenga amchukie baba.

Na sisi hili huwa tunalijua na ndio maana tunaanza kuwapotezea wote na dada yangu inawezekana baba wa mtoto ameligundua hili na akaamua kufanya hivyo hata Mimi nimeachana na mweza wangu baada ya kugundua hayo nikaamua hayo kaani na watoto wenu hata kama mmeachana
 
Wanawake bhana, kumbe umeachiwa nyumba? Na bado unamsumbua baba wa mtoto? Nadhani Hiyo nyumba ilikuwa ni kwa ajili ya maendeleo ya mtoto na sio wewe.

Sasa fanya uuze umsomeshe mtoto shule nzuri unazozitaka. Laah hutaki hivyo rudisha mtoto kwa shule zisizo na ada

Tatizo unaogopa kuonekana umeishiwa wanawake bhana.
 
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule
Sikiliza mama boke miye nilikwambia kipato changu hakiko vizuri tuache mtoto asome shule za serikali tusilazimishe mambo kisa miye na kipato wewe ukaforce mtoto asome private ona Sasa unakuja nishitaki JF
 
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule
1: mzazi mwenzio watoto wake wanasona shule zipi?
2: kama una taka usaidiwe usiombe ada ya mtoto, wewe omba matumizi ya kumlea mtoto, swala la ada litaongelewa wakati kesi ikisikilizwa.
3: huko unakoishi tafuta wakili akuandikie hayo maombi peleka mahakamani atatumiwa summons, summons hiyo usipeleke wewe wala kuipeleka kwa mwenyekiti, apeleke process server wa mahakama ili akikataa kupokea kuwepo kiapo kama ushahidi. Taratibu nyingine utajuzwa huko mahakamani.

Nb wakati mnaachana mliachana kienyeji au? Maana kama mlifata sheria tunategemea mahakama iliweka utaratibu wa malezi ya mtoto including shule.

Hao wanaokushauri uza nyumba achana nao, mida hii wanatoka bar.hawawazi baada ya kuuza mtaishi wapi na mtoto.
 
ukute wakati mnatengana ulimporomoshea matusi/maneno mazito na kumsengenya kwa ndugu, jamaa na marafiki zakooo. Ukaishia kumwambia ... "huna lolotee mwanaume suruali kwanza una kibamiaaa...." kumbe kuna kijamaa kilikuwa kinakupa kiburi akijifanya anaweza kukusaidia kifedhaa. na jamaa nae vyuma vimekaza ndo waanza mtafuta mzazi mwenza kwa kasi ya 4 G

anyway fuata taratibu utapata stahiki yakoo
 
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule
Ada ya wapi wakati Elimu ni bureee!!

Kama ulijichanganya ukampeleka shule za school bus hiyo upambane nayo mwenyewe, maana ukipenda mahakamani akikuambia Mimi uwezo wangu ni kumsomesha mwanangu shule za serikali hapo inakula Kwako maana yawekana hakukubaliana kumpeleka Mtoto shule hizi ikawa ni utashi wako!
 
ukute wakati mnatengana ulimporomoshea matusi/maneno mazito na kumsengenya kwa ndugu, jamaa na marafiki zakooo. Ukaishia kumwambia ... "huna lolotee mwanaume suruali kwanza una kibamiaaa...." kumbe kuna kijamaa kilikuwa kinakupa kiburi akijifanya anaweza kukusaidia kifedhaa. na jamaa nae vyuma vimekaza ndo waanza mtafuta mzazi mwenza kwa kasi ya 4 G

anyway fuata taratibu utapata stahiki yakoo
Inawezekana kabisa mambo ya maex hayo Sasa Mtoto amezaliwa ndani ya ndoa ila wakaachana Mtoto haajanza hata shule ndoa ya Muda mfupi hiyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom