Mwongozo wa ufugaji wa kuku wa nyama (Broiler)

HATUA KWA HATUA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)
Lengo la makala hii ni kukuwezesha wewe mkulima kupata kuku wa nyama wenye uzito sahihi kukuwezesha wewe kupata faida. Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukajua ya kwamba wiki mbili za mwanzo katika uleaji wa kuku wa nyama ni muhimu sana na hivyo yakupasa kuwa mwangalifu...
Asante
 
Mkuu hiyo vigostart inapatikana wapi na bei gani?? Maana kwangu coccidiosis imesababisha vifo karibia 30%
 
Nimekua mfugaji kwa miaka miwili katika ufugaji wa bloirel na kienyeji asili
Bloirer 500 kienyeji nimefikisha 150 hao ni kuchi na kawaida.
CHANGAMOTO ZAU UFUGAJI KIENYEJI
1.Wanatumia muda mrefu kupata faida
Yaani unakaa na kuku hadi wanakuzoea
2.Magonjwa mengi na hivyo kupelekea vifo vingi
3. Upotevu mimi huwa nawafungia na kuwapa chakula ndani ya senyenge lakini wapi huwa wanaruka na kutoka nje. Na haswa vifaranga na kuku wakubwa. Chakula chao nachanganya zile pumba laini za dona na concentrator na funza nawatengenezea.
Hapa nimeshindwa pata ufumbuzi
CHANGAMOTO ZA BLOIRER
1. Uangalizi wa hali ya juu kwamuda mfupi.
2. Ukikosea kuwapa chanjo au dawa vifo ni vingi mno
3. Wanahitaji gharama kidogo kuwafuga. Hivyo bajeti yake isiingiliane na bajet yeyote ile kwenye familia vinginevyo hasara njenje.
FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI
1.Ukowauza kwa wingi unapata faida kubwa
2. Kuongeza afya na ni watam kwa mchemsho
3. Watazaliana kwa wingi hivyo utapata faida ya muda mrefu kwa kuuza mayai,nyama,vifaranga kama utatotolesha utauza tu.
FAIDA ZA BLOIRER
1. Faid chapchap kila baada ya miezi 4 unauza
2. Faida ya haraka kwa muda mfupi vice versa is true.

KARIBUNI WANANZENGO TUJADILI CHANGAMOTO ZA UFUGAJI NYAKATI HIZI NA TUELIMISHANE
 
sitaki kuamini kua hao kuku wa kienyeji wanasumbuliwa na magonjwa sanaaa kuliko hao broilaa
 
Umeelezea vizuri mkuu Ila hapo kwenye broiler nadhani ulikuwa unataka kuongelea kuroiler, broiler ni kuku wa nyama ambae kuanza kumfuga hadi kumuuza inachukua mwezi 1 Tu na sio miez 4 kama ulivosema hapo
 
Kwa kukazia maelezo yako mazuri
.vigaranga day 1 lazima uweke kokoto nyeusi kwenye chombo Cha maji Kama hivyo ili kuzuia kuku kulowana kifuani kwa muda wa siku Saba

View attachment 1843623
IMG_20210706_173512_5.jpg
 
Umeelezea vizuri mkuu Ila hapo kwenye broiler nadhani ulikuwa unataka kuongelea kuroiler, broiler ni kuku wa nyama ambae kuanza kumfuga hadi kumuuza inachukua mwezi 1 Tu na sio miez 4 kama ulivosema hapo
Typing error ni wiki kuanzia nne na kuendelea ingawa wengine wanauza wa wiki 3 na wanakua wakubwa tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom