Mwaka wa nne huu naishi Mbeya, Wanyakyusa nawapa maua yenu japo mna mapungufu machache

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,095
Kwanza kabisa ieleweke mkoa wa Mbeya kuna makabila mengine kama wasafwa, wandali, wamalila, n.k. Ila wageni wengi huwa tumekariri wanyakyusa sababu ndio main tribe, karibu kila mkoa una main tribe wageni hawajui sub tribes, Ruvuma main tribe ni wangoni ila kuna wamatengo, Mara main tribe ni Wakurya ila kuna wajita, Njombe main tribe wakinga ila kuna wabena, n.k.

Wanyakyusa kwa haraka haraka naweza kusema ndio kabila linaloongoza kwa wasomi wengi, viongozi, watu kwenye system, n.k. Kwa Tanzania yote ya mikoa ya kusini.

Inshort wanyakyusa kwa uzoefu wangu ni watu wakarimu zaidi tena kwa vitendo na hakuna maneno ama kutangazwa ukishasaidiwa.

Nimeshakwenda ofisi flani nikiwa mgeni wa mifumo ila kuna mbaba wa kinyaki alinisaidia a to z utadhani mimi mtoto wake, nilishangaa sana.

Suala la msosi wa wanyakyusa wala si taabu, utakula vizuri tu labda wasipike ubwabwa wapike ndizi

Ni wacha Mungu hasa kwa upande wa wanawake, sehemu kama mitaa ya Nzovwe kunaitwa Nigeria sababu kuna nyomi la makanisa, wingi huu umeweza kuwafanya wanyakyusa kuwa mstari wa mbele kutoa wachungaji wengi na waimba gospel katika ngazi ya taifa.

Nikiwa mwizi kichapo kikinizidia ntakimbilia kwa wanyakyusa at least ntapata dozi ya kati kisha nipelekwe polisi, nikizubaa naweza kukatwa mapanga

Wanyakyusa wanathamini sana elimu kwa lengo mtoto aje apate ajira, Mbeya ni sehemu ya pili hapa Tanzania kwa kuwa na vyuo vingi nyuma ya Dsm. Ni Kabila la nne kwa wasomi nyuma ya wahaya, wachaga na wasukuma (kuna wasukuma milioni 10 na zaidi hata kukiwa na 1 msomi katika kila wasukuma 10 bado ni wengi)

MAPUNGUFU YAO...

Pamoja na hayo mapungufu yapo na hayo ni:

Rundo la ndugu.. Kwa kawaida ndugu inabidi wawe wale mliozaliwa nao na wale wa upande wa wazazi kina mjomba, shangazi, ma mdogo, ba mkubwa, n.k. Pamoja na watoto wao Ila wanyaki wamevuka, hata mjukuu wa mke wa pili wa bamdogo wa babu ni ndugu,

Ukabila - Wanyakyusa kwanza wengine msubiri, Kwenye fursa / nafasi za kazi mnyakyusa akishika madaraka ni kawaida kujaza wanyakyusa wengine, ukichanganya na kuwa na ndugu wengi ni shida hio, mlolongo ni mrefu sana.

Wanawake kujali zaidi ndugu kuliko mme, huna sauti mbele ya mwanamke linapokuja suala la ndugu zake hata awe mjukuu wa bamdogo wa babu.

Ubabe kwa baadhi ya wanawake ni tatizo, na hasa ukizingatia wengi wana miili yenye afya ukiwa legelege usije ukajaribu kutumia violence, utaaibika!! Wao wanataka muwe sawa na hii inaleta taabu wao kumnyenyekea mume, wao hudhani ni msimamo au kukataa kuendeshwa ila ni ubabe. Kwenye nyumba mama ndie mwenye sauti.

Wengi sio wana uwezo mdogo kusimamia biasbhara sababu ya kuingiza undugu usio na mipaka kwenye biashara, mtu ukifanikiwa kidogo tu kwenye biashara ndugu huanza kukuelemea na nilichogundua wana uoga wa kuwawajibisha ndugu kwa hofu ya kutengwa. Ndio maana wengi hupendelea ajira ambazo serikali huwalipa mshahara, Ni wazi hata ukienda Mbeya biashara zimeshikiliwa zaido na wageni hasa wakinga.

Ni hayo tu lakini kwa ujumla wanyakyusa wapo juu.
 
Kuna kabila la Wasukuma...

Hili kabila tulifungwa kamba Sana, huwezi kubali mpka ufike unyantuzuni ndio utakubali...., kwa mda mfupi tuu ila sina hamu na wale watu.

Najua ndio mnaongoza kwa kua wengi humu mtaniandama, na mlivyo wachawi mnatamani muitoe hii ID kafara.

Ukabila upo sehemu nyingi ila hawa wamezidi, Wanapenda kunyenyekewa, roho mbaya.

Potelea kote, lawama hapewi mbuzi.
 
Kuna kabila la Wasukuma...

Hili kabila tulifungwa kamba Sana, huwezi kubali mpka ufike unyantuzuni ndio utakubali...., kwa mda mfupi tuu ila sina hamu na wale watu.

Najua ndio mnaongoza kwa kua wengi humu mtaniandama, na mlivyo wachawi mnatamani muitoe hii ID kafara.

Ukabila upo sehemu nyingi ila hawa wamezidi, Wanapenda kunyenyekewa.

Potelea kote, lawama hapewi mbuzi.
Nakuunga bro! Niliona mnyatunzu bro hawa watu sio poa kabisa aisee kilichotokea mungu anajua zaidi
 
Bora Siku hizi wamepunguza kuomboleza Msiba.

Miaka ya Nyuma ilikuwa Wanyakyusa wanakaa Siku 40 wakiomboleza Msiba.

Ilifikia kipindi Serikali ikaingilia kati maana ilikuwa inaathiri Uchumi wao.

Huwezi ukakaa Siku 40 Ukilia Msiba bila kwenda kwenye shughuli zako za Kiuchumi
 
Point ya msingi hujaigusa kabisa je kuna madem wazuri? Kwa umri wanguu huu hilo ni jambo la muhimu kujua
 
Back
Top Bottom