SoC04 Muongozo utatuzi wa tatizo sugu la ajira, kuelekea Tanzania bora

Tanzania Tuitakayo competition threads

Sea Beast

JF-Expert Member
Aug 5, 2022
1,906
4,091
Salaam Wanajamvi

Kuelekea ujenzi wa Tanzania ile tunayotaka, Mimi napenda kuchangia mawazo yangu na kufungua mjadala katika suala zima la utatuzi wa ajira hapa nchini. kati ya changamoto kubwa tuliyonayo kwa wakati huu ni tatizo sugu la ajira ambalo ndio chachu ya kukuza uchumi binafsi na taifa kwa ujumla.

Najaribu kuweka mawazo yangu kadhaa ambayo yanaweza kusaidia utatuzi wa changamoto hii ya ajira hapa nchini na ninyi munaweza kuchangia mawazo yenu chanya zaidi kuweza kufikia Tanzania ile tunayohitaji.

Kupunguzwa kwa Umri wa kustaafu:
kutokana na idadi kuwa kubwa ya wanaohitaji nafasi za ajira nchini serikali iweke muda wa miaka 15 ya mfanyaki wa umma kufanya kazi na kustaafu hii ikiwa na maana aweze kujijenga kiuchumi na kimtaji katika huo muda hili aweze kufanya uwekezaji kwenye Biashara, hii itafanya wengi kustaafu wakiwa na umri wa miaka si mbali na 45, mbali na umri tuliouzoea wa 75 hii ni sawa na kusema tutaweza kuajiri watu wawili zaidi mpaka watatu ndani ya muda mfupi ukilinganisha na kuwa na umri mrefu wa kustaafua ambao unanyima nafasi wengine.
retirement-planning.asp-FINAL-ed21279a08874c54a3a0f4858866e0b6.png

Photo (source Google)

Kuwapa wanachuo mkopo wa Biashara kupitia Boom lao la Mwisho:
Serikali kwa kushirikiana na bodi ya mikopo na wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha ziweze kutoa mikopo ya Biashara kwa wanufaikaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa kuwapa kima fulani cha fedha kuelekea kumaliza mwaka wa mwisho wa kimasomo, kihasi pendekezwa 1 Milioni mpaka 1.5 Milioni, kihasi hiki kitasaidia sana Graduates kujiajiri katika sekta mbalimbali na wao kuweza kuajiri wenzao, hili litawezekana tukiwawekea utaratibu mzuri wa kulipa deni hilo.
images (24).jpeg

Photo (source Google)

Kuwapo kwa muongozo wa mtumishi wa umma kuajiri wasio na ajira:
Tuweke miongozo ya wafanya kazi wa umma kuajiri kijana hata mmoja au wawili, Tatizo kubwa kwa watanzania ni mtaji hii inamaanisha ukiwa upo nje ya system inakuwa ngumu zaidi kupata mtaji kulinganisha na muajiriwa hasa wa serikali hili kuhakikisha tunatatua tatizo la ajira tuweke muongozo kila muajiriwa wa serikali alazimike kufungua Biashara moja hata ya mtaji mdogo tu kama Biashara ya uwakala na aweze kuajiri kijana asiye na ajira hii itafanya tuweze kupata idadi sawa ya watu waliojiriwa kupitia waajiriwa.
images (21).jpeg

Photo (source Google)

Kufungulia Account ya mtaji mtoto (Toto Account):
Mzazi mara tu unapopata neema ya kupata mtoto tuanze kuwawekea pesa za mtaji akiwa mtoto mpaka anakuwa mkubwa, akaumti hii unaweza kuweka kihasi cha 10,000 tu mpaka 20,000 kwa mwezi kutegemeana na uwezo wako ulimuwekea kila mwezi tukipiga hesabu hadi kumaliza chuo atapokuwa na miaka 25 mtoto wako kihasi cha mtaji kinaweza kufikia Millioni 4 mpaka Milioni 6, hii pesa inatosha kabisa mtoto au watoto wako kuanza maisha yao ya kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao na wao kuweza kuajiri wengine.
images (25).jpeg

Photo (source Google)

Naamini kwa kupitia muongozo huu tunaweza kufikia mahala papyri sisi kama wadau wa dhati katika utatuzi wa changamoto hii kubwa ya ajira na kujenga Tanzania iliyo bora.

Tunaweza kuongeza mawazo zaidi.

Nawasilisha 🙏🙏
 
Najaribu kuweka mawazo yangu kadhaa ambayo yanaweza kusaidia utatuzi wa changamoto hii ya ajira hapa nchini na ninyi munaweza kuchangia mawazo yenu chanya zaidi kuweza kufikia Tanzania ile tunayohitaji.
Wazo zuri bwana Sea

Ajira zote hazihitajiki kutolewa na serikali pekee.

Serikali (ambayo ni sisi) tuweke tu mifumo inayoruhusu watu kujiajiri kwenye tija. Sehemu mojawapo ni nishati ya bei nafuu pamoja na soko la uhakika la bidhaa zetu wajasiriamali.
 
Wazo zuri bwana Sea

Ajira zote hazihitajiki kutolewa na serikali pekee.

Serikali (ambayo ni sisi) tuweke tu mifumo inayoruhusu watu kujiajiri kwenye tija. Sehemu mojawapo ni nishati ya bei nafuu pamoja na soko la uhakika la bidhaa zetu wajasiriamali.
Hoja nzuri, hakika tukiwekeza kwenye soko la uhakika itakuwa chachu ya watu kujiajiri maana soko nalo ni moja ya changamoto kubwa.

Wakulima wanalima mazao yao na hakuna soko la uhakika kabisa inakatisha Tamaaa, wakipeleka madam sokoni wanakutana na bei za kiranguzi na rumbles.

Natumai kupitia mjadara huu serikali itakuwa sikivu.

Intelligent businessman let wazo lako hapa kwenye suala hili la ajira
 
Kuna suala la Familia kwa pamoja kuchangia vijana wanaoanza maisha kwa mtaji wa pesa.
 
Back
Top Bottom