Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 21,790
- 36,661
Unasajili on what grounds, whatsapp groups ni feature iliyopo kwa whatsapp app, wamiliki ni meta, meta wanafahamu hili?Msajili wa Jumuiya za Kiraia katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Kihampa, amesema kampeni ya usajili wa jumuiya zisizo za kidini iliyoanza mkoani Dar es Salaam, inahusisha vyama au vikundi vikiwamo vinavyoendeshwa kwa njia ya mtandao wa WhatsApp.
Amesisitiza kuwa ni muhimu vyama na vikundi ambavyo watu wanakusanyika kwa lengo la kufanya sherehe au kuzungumza wakasajili.
Kwa mujibu wa Kihampa, wasiojisajili kwa mujibu wa Kifungu cha 40 cha Sheria Na.3 ya Mwaka 2019 iliyoifanyia mareke bisho Sheria ya Jumuiya Sura Na. 337, kuendesha chama au kikundi chenye sifa ya kusajiliwa bila kusajili ni kosa kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kwa kampeni hiyo, Kihampa alivitaka vyama na vikundi kujitokeza katika ofisi za wilaya husika ambako ndiko usajili huo unafanyika.
"Kuendesha kikundi ambacho hakina usajili, kulingana na kosa ambalo chama au kikundi itafanya maana yake watakuwa wamevunja sheria ya nchi. Madhara ya takayotokea yatatokana na uendeshaji wa chama kwa kwenda kinyume cha sheria.
"Wasisubiri mpaka wachukuliwe hatua za kijinai, hivyo ni vyema wakaja kusajili ili waendeshe shughuli zao vizuri. Kuendesha mikusanyiko bila kufuata sheria ni kosa, ni vyema wakajiepusha na makosa haya.
"Umuhimu wa kusajili vyama na vikundi ni kuimarisha umoja na mshikamano katika taifa. Ni muhimu vyama na vikundi ambavyo watu wanakusanyika kwa lengo la kufanya sherehe au kuzungumza wakasajili vyama na vikundi vyao," alisema.
Alisema ofisi yake imewahi kusajili kikundi kinachokutanisha askari waliopigana vita kuu ya pili ya dunia ambao hukutanika na kuzungumza na kubadilishana mawazo.
Alisisitiza kuwa vikao vingi vya namna hiyo ambavyo huvisajili na kusisitiza kuwa mchakato wa usajili kuanzia mwanzo hadi mwisho ni Sh. 200,000 tu.
Kuhusu usajili ulioanza jana mkoani Dar es Salaam kwa kuanzia na wilaya ya Kigamboni, Kihampa alisema utaendeshwa kwa siku mbili katika ofisi za wilaya husika.
"Wilaya ya Temeke (Aprili 4-5), Ubungo (Aprili 6-7), Kinondoni (Aprili 8-9) na ku- malizia wilaya ya Ilala.," alisema.
Usajili huo, alisema unahusisha vyama na vikundi visivyo vya kidini vya kiuchumi vikiwamo vya wafanyabiashara wadogo, wanaofanya kazi katika masoko, wakulima wafugaji na wamiliki wa mashine za kusaga nafaka.
Pia alisema vyama vyå madereva, utingo, bajaji na vya kijamii ni pamoja na vya kufa
na kuzikana, ujirani mwema, wanaomiliki nyumba au wanaoishi kwenye maeneo ya makazi.
"Vyama au jumuiya za kiutamaduni, vyama vya kiukoo, vya kikanda au umoja unaoanzishwa kwa lengo la kudumisha mila na desturi fulani vinatakiwa kusajiliwa," alisema.
Kihampa alitaja kundi la mwisho ni la jumuiya za kiraia zisizo za kidini zitakazosajiliwa ni vya kitaaluma vikiwamo vya wahitimu wa shule au vyuo vya elimu ya juu au stadi za ufundi Umuhimu wa usajili vyama au vikundi, alisema ni wanachama kupata uhalali wa kisheria kwa kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 40 cha Sherſa Na.3 ya Mwaka 2019, ni sharti la lazima kusajili mikusanyiko au vyama vyote vinavyopaswa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria hii. Alisema umuhimu wa pili ni kutoa hakikisho kwa kulinda mali na fedha za wanachama na kuhakikisha chama kinaendeshwa kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na kulinda maslahi na ustawi wahusika katika kikundi.
Kwa upande wa serikali, alisema umuhimu ni kupata takwimu sahihi na mtawanyiko wa vyama na vikundi vilivyoko ili kuweza kupanga mipango na mikakati mbalimbali ya kuwafikia wananchi. Kihampa alisema kwa upande wa jamii, kuna umuhimu mkubwa wa kusajili vyama hivyo kwa kuwa, vinalenga kuongeza tija na ufanisi, kwa wizara za kisekta kuwafikia na kuwapatia mafunzo pindi inapohitajika.
"Tunatambua vyama na vikundi hivi vipo katika jamii, lakini havijasajiliwa na wengine inawezekana hawajui kabisa kama wanatakiwa kusajiliwa au kama wanatakiwa kusajiliwa waje na nyaraka zipi," alisema.
Alisema katika kampeni hii wale watakaotimiza baadhi ya nyaraka watapatiwa usajili wa haraka na moja ya nyaraka ni barua kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya husika wanakotoka.
Nipashe