Msajili wa Jumuiya za Kiraia: Serikali haisajili 'groups za WhatsApp' bali inasajili kisheria jumuiya zisizo za kidini

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
130
218
Msajili wa Jumuiya za Kiraia kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Kihampa amesema kuwa Serikali haisajili 'groups' za WhatsApp isipokuwa wanasajili jumuiya mbalimbali ambazo sio za kidini ambazo zipo kwenye jamii.

Anasema kuwa zoezi la usajili ambalo linaanzia kwenye Mkoa wa Dar es salaam lina uhalali kisheria (kwa mujibu wa kifungu cha 40 cha Sheria namba 3 ya mwaka 2019), lakini anadai kuwa wamekuwa wakianza kwa kutoa elimu, na kuwa baada ya kutoka Mkoa wa Dar es salaam zoezi hilo litaendelea kwenye Jiji la Mwanza pamoja na Arusha.

Ameongeza kuwa jumuiya hizo zinaweza kuwa zinajihusisha na masuala mbalimbali katika jamii ikiwemo kuchangiana au baadhi mambo mengine yanayowaunganisha kama jumiya, ambapo amesema zoezi la usajili na kukamilisha kila kitu ikiwemo ada ya mwaka ni laki mbili, lakini baada ya hapo kila mwaka jumhiya itakuwa ikilipia elfu 50 tu ya usajili.

Aidha amesema kuwa utaratibu huo unalenga pia kukusa misingi ya Utawala Bora na kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa sababu Serikali itakuwa na taarifa ambazo zinaweza kuwa msaada katika kuweka mazingira rafiki zaidi.

Akifafanua namna utaratibu huo utakavyokuza utawala bora amesema kuwa kulingana na utaratibu wa kuwasilisha nyaraka, wahusika kwenye jumhiya watawasilisha taratibu zao zinazoonesha utaratibu wa jumiya inavyoendeshwa pamoja na kuweka wasifu (CV) za baadhi viongozi kama inavyotakiwa katika taratibu zinazoratibu suala hilo.

Ameongeza kuwa kupitia utaratibu huo vikundi vyenye Katiba vitaziwasilisha sambamba na vingine kushauriwa namna vinavyoweza kuwa na miongozo bora.

Akizungumza na Kituo kimoja cha redio April 4, 2024, Msajili huyo amedai kuwa utaratibu huo utawafanya kuona uzingatiaji wa haki za kuchagua na kuchaguliwa jambo ambalo amedai kuwa msingi wapo wa utawala bora. Sanjali na hilo amesema kuwa utaratibu huo ni rafiki pia kwa sababu utasaidia kupunguza kero na kuweza kuwawajibisha wahusika ambao ametolea mfano kuwa wamekuwa wakidhurumu pesa za jumuiya.

Zoezi la usajili kwenye Mkoa wa Dar es Salaam limeanza tokea April 2 hadi 10, 2024 ambapo maafisa wanaweka kambi kwenye Wilaya, ambapo baadhi ya jumuiya zinazotajwa kusajiliwa ni jumuiya za umoja wa watu kuzikana, jumuiya za kusaidiana kwenye shida na raha, jumuiya za kitamaduni, kikanda, kikabila, kitaaluma, umoja wa waandishi wa habari, madaktari, wahandisi, wahitimu wa shule, vyuo, umoja wa vikundi vya fani mbalimbali ikiwemo ufundi.
 
Kuna yale makundi ya watu wa mikoani, wilayani, kata na hata vijiji walioanzisha jumuiya zao za kusaidiana katika misiba na sherehe yaliopo dara. Jumuiya zingine tayari zina katiba zao ila usajili serikalini hazina
 
Serikali ianishe hizo jumuiya zinaanzia na watu wangapi, ni zi za fani/ujuzi gani. Kama ni wachongaji, wachoraji, wafinyanzi, wanenguaji, walimbwende/ma model, video queens, wauza vitumbua/maandazi na wengine wengi wasio maarufu.
 
Back
Top Bottom