Msaada: Nimuoe huyu binti au nisikilize ushauri wa Wazazi wangu?

Sasa muda wote unaruka nae dhamira yako ilikuwa ni ipi kwake?

Ulikuwa unalala nae kupunguza upwiru?

Ulikuwa unalala nae sababu umelogwa na haujui mwanamke wa kuanza nae maisha utampata wapi?

Ulikuwa unalala nae ili kutest utamu?

Shida huwa ni nini?

Kwann unaanza mahusiano na mtu ambaye ukiambiwa kesho mfunge ndoa awe mkeo wa maisha roho na akili vinakugomea.

Me nadhani ifike wakati sasa ukikuta mwanamke haeleweki na unaona kabisa hana sifa za kuwa mke then umkalie mbali. Kama unataka kupunguza hamu tafuta hawa wakujiuza ili kupunguza hii kasumba ya kuzalisha wanawake ambao hautaweza kuishi nae.

Mnatutesea hawa Malaika mnaowaleta kwa maamuzi ya kibinafsi sana halafu wanakuja kukuta baba na mama hawana akili ya maisha ya pamoja wapo wapo tu wanaanza teseka na kukosa upendo na attention ya baba na mama.

Mimi nawaonea huruma sana na kujiskia vibaya sana watoto hawa wasio na hatia mnawafanyia huu ukatili. Ipo siku mtalipia haya mateso mnayowapa hawa watoto.
 
Kwahiyo huyu binti mmemgeuza mashine ya kutotoleshea sindio? Mnamzalisha mnaenda kuoa wengine!

Mtoto wa miaka mitano ni mkubwa aende kwa baba ake ili binti nae afaidi ndoto zake kuitwa mke. Aliyetangulia aliharibu ila wewe unakwenda kuharibu zaidi, huyu binti akiwa na watoto wawili haoleki tena.

Ukiishi na huyu mtoto jiandae babaake kuletwa hapo kwako amuone mtoto wake, au kukutanishwa kwa siri na mtoto wake. Mama atoe mtoto aanze maisha mapya.
Mleta mada ishi humu, achana na mawazo ya wazazi ila kaa hapa.
 
Ninadhani wazazi wako ni members wa JF pia. Jitahidi kusoma comments zote labda unaweza kugundua ID ya mzazi wako. Msimamo wa wanaJF ni kama wa wazazi wako.
 
Huu ushauri wako leo ingekua ni 80's ama early 90's ungefanya kazi ila kwa kizazi hiki bora achukue mwanae alee kuliko kuoa mwanamke mwenye mtoto,
Najua changamoto zake ndo mana simshauri hata kidogo,
Umewahi kupitia changamoto zipi watu wajifunze?

Ningependa tufahamu walau kupata abc
 
Mechi imeanza 1-0 sema si umesema ana kiumbe chako kakibeba basi akijifungua 1-1. Hapo pambana utafute goli la ushindi.
 
Habari zenu Wana JamiiForums?.

Mimi nimekuwa kwenye mahusiano na dada mmoja Kwa miezi kumi sasa. Dada huyo ni mama WA MTOTO mmoja WA miaka mitano, jamaa aliyezaa naye walisha achana siku nyingi, na Kwa SASA ana familia yake, ila wanalea tu mtoto.

Sasa Kwa BAHATI MBAYA au NZURI huyo dada ana ujauzito wangu WA miezi mitatu na wiki CHACHE ZILIZOPITA niliwasilisha taarifa Kwa wazazi wangu na kusudio langu la kutaka kumuoa. Lakini wazazi wamemkataa katakata na hofu yao ni kwamba mabinti ambao ni single mother mahusiano yao na wazazi wenzao huwa hayaishi, hivyo walishauri niachane naye na nijiandae kulea mtoto atakayezaliwa kama mwanaume wake WA kwanza anavofanya.

Mimi nampenda huyo binti ila wazazi wamemkataa, hapo ndo naumiza kichwa. Na pia wazazi wamesema vinginevyo nikubali kuishi na kulea mtoto wake aliyezaa na mwanaume mwingine Ili kupunguza mawasiliano kati yake na huyo mzazi mwenzie.

Lakini Mimi suala la kulea mtoto WA mwanaume mwenzangu naona itakuwa fedhea sana kwangu. Naombeni ushauri wenu, niwasikilize wazazi au Nile ngumu nimuoe hivyo hivyo.
Sasa ndugu kama umeona wazazi wanaongea pumba kwasababu ya genye zako,utaweza kuwasikiliza wana jf usiowajua kweli....!!! Baba na mama yako ndio nguzo yako
 
Kwahiyo huyu binti mmemgeuza mashine ya kutotoleshea sindio? Mnamzalisha mnaenda kuoa wengine!

Mtoto wa miaka mitano ni mkubwa aende kwa baba ake ili binti nae afaidi ndoto zake kuitwa mke. Aliyetangulia aliharibu ila wewe unakwenda kuharibu zaidi, huyu binti akiwa na watoto wawili haoleki tena.

Ukiishi na huyu mtoto jiandae babaake kuletwa hapo kwako amuone mtoto wake, au kukutanishwa kwa siri na mtoto wake. Mama atoe mtoto aanze maisha mapya.
Nimekuelewa Kwa herufi kubwa Mkuu.
 
Halafu mbona kuna wanawake wengi tu ambao hawajazaa?

Unakwama wapi Mkuu?
Ishu sio kuzaa au kutokuzaa Mkuu, unaweza ukaja ambaye ni fresh hajazaa ila akawa anapasha kipori na ex wake. Nafikiri point ya msingi ni namna ya kudhibiti mawasiliano kati yake na na baba mtoto wake
 
Ishu sio kuzaa au kutokuzaa Mkuu, unaweza ukaja ambaye ni fresh hajazaa ila akawa anapasha kipori na ex wake. Nafikiri point ya msingi ni namna ya kudhibiti mawasiliano kati yake na na baba mtoto wake
Ex wanaweza kuachana na wasitafutane tena. Huo uwezekano upo

Ila Wazazi hawaachani Abadan.
 
Back
Top Bottom