Witch hunter
JF-Expert Member
- Nov 21, 2018
- 1,454
- 3,391
- Thread starter
- #21
DahCode zako sio. Kaa nae, si ulimtaka.
DahCode zako sio. Kaa nae, si ulimtaka.
We ni ms_nge sanaSasa nifanye nini ndugu? Nipe wazo basi mwanaume mwenzio... Haya mambo hayana mwenyewe
Tuna kizazi cha vijana wa hovyo sana aiseeSikio la kufa halisikii dawa, sasa ishi na huyo mwanamke uone uchungu wa kuhudumia
Dah. Kama huwezi nishauri acha tu mkuu. Haya ni maisha tuUwe unatembea na mafuta ya nazi kulainisha zoezi wakikudakaView attachment 2969521
Umeshamuharibia ndoa yake haya mchukue uishi nae kwanini unamkimbiaDah. Kama huwezi nishauri acha tu mkuu. Haya ni maisha tu
Tuna vijana wa hovyo sana alafu mbaya zaid anajuaDah classmate umezingua sana. Yaani hadi nyumbani kwa jamaa ulikua unaenda kulala comfortable kabisa. Kama sio chai basi vuna tu ulichopanda.
Mkuu kwa sasa matusi hayasaidii. We nishauri nifanye nini ili kunusuru ndoa yake. Pia na Mimi niwe na amani.We ni ms_nge sana
Yaani mtu anamume na wewe unaendelea nae haya sasa furahi sababu umeshamuharibia maisha yake
Kuna kitu watu wanasahau. Sio kila wakati mume ana uchungu na mke, kuna nyakati anatafuta mtu wa kumchukua bila masharti. Jamaa kajitokeza kapewa mke anaogopa ogopa.mbona easy tu hapo iyo ndo inaitwa win win
Sisi wanaume huwa tuna namna nyingi za kuacha wanawake..!Khabarini wana jukwaa.
Mwaka 2021 nilikutana na dada mmoja mzuri sana, mrembo, mwenye kuvutia na mpole sana ambaye mwanaume yeyote mwenye akili timamu lazima tu angempenda. Basi nikafanya mchakato nikapata mawasiliano yake. Baada ya kuwasiliana na kumueleza shida yangu hakuwa na hiyana hivyo tukaingia katika mahusiano japo alinambia kuwa yeye ni mke wa mtu na ana Watoto wawili.
Kusema kweli tulipendana, mpaka sasa nampenda sana. Mme wake ni mtu wa mishemishe, mara nyingi hayupo. Hivyo nilikuwa naenda usiku kulala kwake na siku nisipoenda basi nilikuwa nampigia simu huyo mpenzi wangu tunazungumza hadi usiku wa manane. Au chatting kwa WhatsApp au sms za kawaida. Japo tulifanya kwa siri sana na mtu asingeweza kugundua, hata rafiki zangu wa karibu hawakujua na rafiki zake pia hawakujua lolote.
Penzi letu lilinoga mno, ilifikia hatua nikawa namiliki CREDIT CARD ya mme wake, na haikuwa issue kufanya miamala midogo midogo. (sio kwamba nilikuwa nalelewa sema tu alinipenda na kuniamini kiufupi tunapendana) pia nilimpenda mno mtoto wake mdogo, nilikuwa nampelekea vizawadi zawadi nikienda kulala, nacheza nako in short ni kacheshi mno kale katoto na kalinipenda pia.
Wakuu, hakuna marefu yasiyo na ncha, hatimaye mwenyemke akajua kwamba mke wake anachepuka, (hapo ndipo chanzo cha tatizo langu) akajaribu kutafuta ajue anachepuka na nani, akatafuta mpaka akapata namba yangu, mke wake akanambia kuhusu hili hivyo tukakubaliana tusitumiane sms na atakuwa ananitafuta yeye. Na mimi niliamua kuchukua extra precaution ikiwa ni Pamoja na kutopokea namba ngeni, pia mke wake alikuwa akinipigia nikipokea nasubiri aanze yeye kuongea ndo na mimi niongee. Baada ya jamaa kuona sipokei namba ngeni wala kujibu sms za namba ngeni aliamua kutafuta jina nililosajiria laini, nashukuru mungu laini yangu hiyo nilisajiri kwa jina la mtu mwingine na mtu huyo alikuwa mkoani hivyo asingeweza kunifahamu.
Baada ya harakati za kunitafuta kugonga mwamba, jamaa aliamua Kwenda mkoani kuendelea na mishe zake. Mimi na mpenzi wangu tukarudisha mapenzi na tukaendelea kuchati na kupeana mambo kama kawaida. Siku ya jumamosi mwezi wa nne tarehe 13 jamaa alirudi, na mke wake alinijuza juu ya ujio wake. Usiku mida ya saa 4 kuna message moja illingia WhatsApp kutoka namba ngeni nanukuu
“NIMEAMUA KUKUACHIA HUYO MWANAMKE, KESHO ATAKUJA MUANZE NAE MAISHA, MIMI NTABAKI NA WANANGU. ASANTE SANA MWANAUME MWENZANGU”
Ujumbe huu ulinishitua sana na ukizingatia ulikuwa umeeandikwa kwa maandishi makubwa kuonesha msisitizo, kusema kweli niliamua kuhama ghetto nikaenda logde kulala ili kulinda usalama wangu maana nilihisi kama naweza patwa na jambo baya. Pia simu nilizima ili isije kuwa tracked nikapatikana kiboya. Usiku sikupata usingizi hata kidogo yaani hata kufumba tu macho hakuna. (acheni jamani watu tunapitia shida sana hapa Tanzania duh) kuna mda natamani hata niwe mkimbizi Afghanistan kuliko kuishi hapa Bongo.
Kuna jambo moja ambalo mke wake hakunambia na alinambia ikiwa ni too late. Kumbe jamaa alimpa zawadi ya simu kabla hajarudi mkoani kwenye mishe zake, simu hiyo alikuwa ameihack achilia mbali normal sms and calls, hata chatting za WhatsApp alikuwa anaziona na kuzisoma. Jambo hili lilinishitua sana maana nilijua atakuwa amenasa pia picture zangu tunazotumiana na mkewe hivyo kudakwa ni suala la mda tu.
Kwa ufupi ni kwamba.
Jana Asubuhi na mapema nilihama huo mtaa, nikaenda mtaa mwingine mbali kabisaa maana nilihisi jamaa anaweza niletea huyo mke wake hadi kwangu. hivyo asubuhi na mapema niliita Kirikuu ikabeba vitu vyangu nikasepa. Leo saa 4 usiku nikapokea simu ya huyu mwanamke (mpenzi wangu) akanambia kwamba
“baba jay (code) amekuja na mwanamke mwingine, mimi amenifukuza amekatalia watoto wake nimekuja hapo kwako wamesema umehama, kwanini umehama bila kunambia? Uko wapi nahitaji tuzungumze.
Ujumbe huu umefanya nikatetemeka kuanzia unyayo mpaka utosi, sikutarajia jambo kama hili, huyu mwanamke anasema anataka aje tuishi, pia nimsaidie afungue shauri mahakamani ili apewe taraka, mgawo wa mali na Watoto pia. Yaani niko njia panda nawaza nimuelekeze nilipo? Dah! Hata sielewi… na mimi sina mpango wa kuoa saa hizi. Yaani kimsingi sitaki kabisaa mambo ya kuoa iwe leo au kesho. Hata nikitaka kuoa siwezi oa single mother, nyumbani watanielewaje? Wakiskia story kuhusu huyu mpenzi wangu je itakuwaje? Duh.
Mambo ni mengi sema siwezi Andika yote ntapoteza mda wenu buree.
Ndugu zangu naombeni Mnishauri nina shida sana. Yaani dunia imekuwa chungu sana kwangu, naishi kwa kujificha kama mnyama duh! Nimechoka na maisha ya utumwa. (better die free than living as a slave)
Karma is realWe ni kijana wa hovyo sana pumbavu kabisa
Nakuhakikishia hio karma haitakuacha
Japo ni hadithi ya kutunga ila Jamaa wala hana shida keshajikusanyia ushahidi wa uchafu wenu anasubiri huyo mwanamke apeleke pua mahakamani yeye hana haraka. Wewe lea mke huyo.Mkuu kwa sasa matusi hayasaidii. We nishauri nifanye nini ili kunusuru ndoa yake. Pia na Mimi niwe na amani.
(acheni jamani watu tunapitia shida sana hapa Tanzania duh) kuna mda natamani hata niwe mkimbizi Afghanistan kuliko kuishi hapa Bongo.
nadhani jamaa anaogopa sababu anahisi kila mwanaume ni ki ng'ang'anizi kama alivyo yeyeKuna kitu watu wanasahau. Sio kila wakati mume ana uchungu na mke, kuna nyakati anatafuta mtu wa kumchukua bila masharti. Jamaa kajitokeza kapewa mke anaogopa ogopa.