Mlipuko huu wa Rooters za WIFI kwa kampuni za Simu ipi ni nzuri Kwa matumizi nyumbani?

Mimi natumia vodacom nyumbani ambayo ni ya 4G 20Mbps,na ofisini natumia airtel 5G ambayo ni 30Mbps..
Kiukweli zote zipo vizuri sana,ingawa nimeipenda Airtel kwakua ina powerbank umeme ukikata unaweza tumia mpka 7hrs bila kuzima.
Hata mimi mkuu natumia hiyo ya voda ya 20Mbps nilinunua hiyo powerbank/UPS ya router za Airtel natumia kwenye router yangu, umeme ukikatika inapiga kazi zaidi ya masaa 10.
 
Kwa mitandao ya simu Airtel wapo friendly zaidi, Gharama ndogo za kujisajili ambayo ni laki 2, wanakupa router na powerbank incase umeme unakatika ama upo nje ya nyumba. Vifurushi vyao vinaanzia 70,000 kwa mwezi

Voda pia wapo vizuri ila wame target zaidi wafanyabiashara, usajili bure ila utahitaji ka kila mwezi kulipa, vifurushi vinaanzia 120,000

Tigo wao gharama ghali sana kujiunga 650,000 ila kwa mwezi ni 70,000


Angalia kwako mambo haya
1. Unapata 5G? Kama unapata ni mtandao upi?
2. Pima speed zote za 4G na 5G angalia mtandao upi unazidi speed husika unayotaka kununua...

Then chagua mtandao kutokana na quality ya mtandao ya eneo lako, u naweza toa hela nyingi ukaishia kupata speed mbovu.
Je kuna yenye option ya kulimit matumizi ya data? Mfano mtu nampa gb 1 akimaliza hiyo ndio basi tena,pili iwe inajidisconnect kama mpaka ajiunge tena kwa password.
 
Unaweza ila si kwa hio router, internet itoke kwenye router then iende kifaa cha kubana bundle then hicho kifaa ndio kirushe wifi.
Kifaa kama, simu? Sihitaji kutumia simu, simu yangu inaweza fanya hiyo kazi, lakini naitumia mwenyewe, siwezi iacha home muda wote.
 
Hizo 4G na 5G aangalie kama eneo analokaa lipo covered na network ya 4G au 5G. Unaweza kununua router ya 5G ukaenda kutumia eneo la 3G ni kazi bure...

Asante.
Umeongea sawa kabisa. Hayo makampuni hovyo sana kwenye coverage, mara nyingi utasikia ungekuwa mbezi beach, mikocheni, masaki au posta. Hovyo sana!!!! Waongeze coverage.
 
Mfano route
Sio simu, kifaa cha kubania Bandwidth, inaweza kuwa router, computer etc.

Router anayokupa isp inakuwa ni basic tu, ukitaka feature zozote advanced inabidi ununue yako.
Mfano router gani sokoni inaweza nifanyia haya na nitaipatia kwa kiasi gani?
 
Mfano route

Mfano router gani sokoni inaweza nifanyia haya na nitaipatia kwa kiasi gani?
Neno la kitaalam wanaita "captive portal" router yoyote yenye hio feature itakubali, Mfano ni Router za Ubiquiti, bei kama 500K hivi huko ughaibuni, nimecheki Aliexpress kuna brand za Kichina chini ya laki 2 zinafanya pia, ufanisi sijajua.

Pia waweza ukatumia Computer na software za Internet Cafe kama Antamedia.
 
Naona kama kwa sasa limeingia wimbi la kutangaza na kuuza Rooters za WIFI kwa makampuni ya simu nchini.
Kila mmoja anavutia kwake kwa vifurushi vya Mbps 10, 20 na 30 ambavyo ni kwa 4G na 5G unlimited mwezi mzima.

Je, ninunue toka kwa kampuni gani ambayo huduma zake katika hili ni reliable na price friendly kwa matumizi ya nyumbani?

Msaada tafadhali kwa walio experienced huduma hii iliyokuja kwa kasi!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Chukua router ambayo ni multipurpose ili usiwe kifungoni amua kati ya D-Link wireless router au TP-link
 
Wakuu. Tukiendelea kujadili hii topic hapa nao hawa vipi?
Screenshot_20240224-090847.png


Kuna mtu kawatumia?

Nina simu 2 kwa sasa natumia bundle kubwa sana kwa siku. P
Nilikua na Ile Post paid ya tigo ya watu watatu kuna mmoja anazingua halipi tumezimiwa.

Nadhani Airtel inahusika kwenda.
 
Wakuu. Tukiendelea kujadili hii topic hapa nao hawa vipi?
View attachment 2914424

Kuna mtu kawatumia?

Nina simu 2 kwa sasa natumia bundle kubwa sana kwa siku. P
Nilikua na Ile Post paid ya tigo ya watu watatu kuna mmoja anazingua halipi tumezimiwa.

Nadhani Airtel inahusika kwenda.
Inabidi uchunguze wanatumia technology gani na terms na condition zipoje. Otherwise Airtel ina make sense zaidi.
 
Kwa inategemeana na mahali ulipo kwani kuna maeneo mtandao A unashika sana wajati mtandao B unakuwa hafifu.

1.Fiber
Ndio chaguo lakwanza ikiwa upo maeneo yaliyofikiwa na mtandao wa fiber wa TTCL hasa maeneo ya mjini.Yapo makampuni binafsi yanasambaza fiber ila kwa gharama ya juu kidogo ukilinganisha na TTCL.

UZURI WA FIBER
*Ndio chanzo mama cha internet baada ya wire ndio ifuate wireless hivyo nisawa na kusema upo kwenye branch za mkongo wa Internet.
*Bei nafuu zaudi,Ikiwa na kima cha chini 55,000/= kwa 20 Mbps.
*Haiathiriwi na hali ya hewa.Ukizingatia inatumia wire toka chanzo hadi kwa mlaji hivyo changamoto za umbali,mvua,upepo nk havitokusumbua.
*Hamna Jam.Vifurushi ya unlimited hasa hivi vya kwenda kwa mlaji huwa ni shared network hivyo watumiaji wanapokuwa wengi kasi hupungua.Na hapo ndio utajua maana ya sentensi UP TO 10 Mbps,20 Mbps,30 Mbps nk wakimaanisha speed inaweza kuwa chini ya hapo ama ikafikia hapo.
*Free installation kwa TTCL kwa makampuni binafsi sijajua.

UBAYA WA FIBER
*Haihamishiki yani ipo fixed eneo ulipounganishwa hivyo huwezi kuhama nayo.
* Inachukua muda kuunganishwa kwa TTCL basi huchukua hata mwaka hasa vifaa vikiwaishia hawa sio wakuwategemea kabisa.Makampuni binafsi sijajua ila kama upo kwenye zone zao basi nisuala la wiki tu.
*Ipo limited.Inapatikana kwa wingi maeneo ya mjini kwa walio nje ya mji itakulazimu ugharamike nguzo na vifaa kufikishiwa yani nikama ilivyo kufungiwa umeme wa tanesco.
*Miundombinu kuharibika.Hasa kipindi cha mvua nguo kuanguka waya kukatika ndio kukatika kwa mtandao hadi waje kuunganisha tena.


ANTENA
Hii wanayo Vodacom na Airtel.Mfano huduma ya superkasa ya voda huwa wanaunganisha kwa kutumia antena maalum yenye kuwasiliana na mnara wao ulio karibu yako.Hii inakuwa na kasi moja tu ya 20 Mbps kwa 115000.
Airtel sijajua gharama zao upande wa antena.

UZURI WA ANTENA
*Antena hubust mtandao mana hufungwa nje ya jengo lako hivyo kunasa mawimbi kwa urahisi.
*Ndio utapata kifurushi cha 20mbps kwa 115000 upande wa voda kwa huduma ya supakasi.

UBAYA WA ANTENA
*Ipo fixed eneo lako ulipofungiwa.
*Inaweza kuathiwa na mvua,radi nk
*Lazima utangulize malipo ya miezi 2 ndio waje kukufungia ila pesa utarudishiwa baada ya kumaliza mkataba ikiwa hutaki kuendelea.
*Kwa voda kifurushi ni kimoja tu cha 2) Mbps.

ROUTER
Hapa kuna makampuni matatu voda,tigo na Airtel.
Vodacom wako na router 5G kwa kifurushi kinachoanzia 30 Mbps kwa 120,000.
Utalazimika kutanguliza kulipia miezi 2 ya kifurushi ukitakacho mfano 240000 kwa kifurushi cha 120000 ili usajiliwe.
Sababu ya sifa ya 5G hivyo vifaa vinapatikana maeneo yaliyofikiwa na 5G yao tu.

Airtel wako na router ya 5G kwa kifurushi kinachoanzia 10 Mbps kwa 70000...30 Mbps kwa 110000 nk
Utalazimika kulipia na 200000 ya kifaa (router)
Vifaa vinapatikana maeneo yaliyofikiwa na 5G yao tu.

Tigo wako na router ya 5G kwa kifurushi kinachoanzia 10 Mbps kwa 70000...30 Mbps kwa 100000 nk
Utalazimika kulipia kifaa router kitu kama 600000 hivi.

My take
Chukua router kulingana eneo ulipo ambapo mtandao husika suala la internet wapo vizuri.
Usidanganyike na neno 5G hii ni teknolojia tu ya usafirishaji mawimbi hivyo hata 4G inaweza kucover kifurushi chako.4G inaweza kufikia speed ya 100 Mbps - 150 Mbps huku 5G ikifikia 300 Mbps.
Hivyo hata kama upo eneo lisilo na 5G bado utapata mawasiliano kupitia 4G.
Zingatia sana 5G ikiwa unajiunga na 150 Mbps au zaidi.

*Vifurushi vyote na huduma zote ni unlimited yaani unatumia kwa kupimiwa speed sio GBs hivyo tumia uwezavyo.
*Kwa kuwa unlimited hii haimaanishi uunganishe marafiki na majirani wote kwenye WiFi yako kwa mtashea iyo speed uliojiunga.
*Ili kupata speed halisi ya kupakuwa file basi gawanya kwa 8 Mbps ulizojiunga.Namaanisha kwa mfano umejiunga kifurushi cha 10 Mbps inakuwa 10/8=1.25mbps yaani wakati unadownload basi speed iwe inasoma hadi kufikia 1.25 pale juu ya simu kwenye minara ya mtando na data connection ichezee hapo 700kbps-1.25mbps japo pia yaweza kupitiliza kulingana na eneo ulipo au wakati wa usiku.

Kwangu mimi kwa maeneo niliyopo ni best choice na kifurushi unaweza kubadili muda wowote yaani unacholipia ndio unachopatiwa.

TTCL panahitajika mkurugenzi mwenye uchungu na taifa na kuliinua shirika hilo la Umma linalouliwa na wachache fulanifulani.
Dah umeandika aisee, shukrani sana kwa elimu hii murua kabisa.
 
Back
Top Bottom