Mke wangu amekosa choo kwa siku saba, nisaidieni

Habari za usiku huu wana JF, naomba msaada wa haraka, mimi na mke wangu tupo mbali kidogo, leo ameniambia hajapata choo kwa siku saba, nimechanganyikiwa hapa sijui nifanyeje na tumbo linamuuma hatari
Kwa siku zote hizo madakitari wameshindwa? Au unatafuta sisi madakitari wa bure! Nenda duka kubwa la dawa lenye wafamasia watakusaidia bure, ila ujue kukosa choo kunaweza kusababisha kifo.
 
Habari za usiku huu wana JF, naomba msaada wa haraka, mimi na mke wangu tupo mbali kidogo, leo ameniambia hajapata choo kwa siku saba, nimechanganyikiwa hapa sijui nifanyeje na tumbo linamuuma hatari
Anapitisha Hewa namaanisha anajamba??
Kama Ndiyo sio Tatizo kubwa..

Ataweza kusaidiwa na hata matunda kama Mapapai..

Ila kama utaweza kamchukulie dawa..
Mchukulie Bisacodyl anza na 15mg (Vidonge vitatu).. halfu kama Bado hakupata Choo kwa Masaa Sita mpaka Nane..Muongeze Bisacodyl 5mg (Kidonge kimoja) kila baada ya masaa nane mpaka apate Choo..

Kama akipata Choo na akataka Kuzuia Asiharishe Zaidi atumie Loperamide vidonge Viwili anywe na anywe kimoja kimoja kila akiona anaharisha na Anunue ORS anywe mara tu baada ya Kuharisha..

NB: Loperamide na ORS viwe Tayari kabla ya kunywa Bisacodyl
 
Habari za usiku huu wana JF, naomba msaada wa haraka, mimi na mke wangu tupo mbali kidogo, leo ameniambia hajapata choo kwa siku saba, nimechanganyikiwa hapa sijui nifanyeje na tumbo linamuuma hatari
Atafute mmasai au duka la kisuni aombe dawa ya kusafisha tumbo ni vimbegu flani ivi...Chap atapata choo hadi panakuwa kama panapiga mluzi akienda Chooni.
 
Habari za usiku huu wana JF, naomba msaada wa haraka, mimi na mke wangu tupo mbali kidogo, leo ameniambia hajapata choo kwa siku saba, nimechanganyikiwa hapa sijui nifanyeje na tumbo linamuuma hatari
Anywe maji ya moto kikombe kimoja kila baada ya lisaa limoja.

Maji yawe yamechemka kama ya chai.
 
Pole
Habari za usiku huu wana JF, naomba msaada wa haraka, mimi na mke wangu tupo mbali kidogo, leo ameniambia hajapata choo kwa siku saba, nimechanganyikiwa hapa sijui nifanyeje

Habari za usiku huu wana JF, naomba msaada wa haraka, mimi na mke wangu tupo mbali kidogo, leo ameniambia hajapata choo kwa siku saba, nimechanganyikiwa hapa sijui nifanyeje na tumbo linamuuma hatari
Pole sana ndugu. Wataalamu wanasema kuwa ukikosa haja kubwa kwa zaidi ya siku tatu ni lazima umuone daktari. You are constipated.
Siku saba ni nyingi mno, madhara makibwa zaidi yanaweza kutokea. Muone daktari haraka sana.
 
Back
Top Bottom