X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,817
Mkate Wa Sinia - Mkate Wa Kumimina Aina Ya Kwanza
Vipimo
- 1 Kikombe Cha Mchele
- 1 Kikombe Cha Nazi Ya Unga
- 1 Kikombe Cha Sukari Kupungua Kidogo
- 1 Kikombe Cha Maji Au Maziwa Vuguvugu
- 1 Kijiko Cha Chai Cha Hamira
- Iliki Kiasi Upendavyo
- Ute Wa Yai Moja
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.
- Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka mchanganyiko uwe lani kabisa.
- Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).
- Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
- Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.
- Funika sufuria na uvumbike(bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.
- Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata.