Mjamzito afumaniwa akijamiiana hospitalini

utopolo og

JF-Expert Member
Nov 29, 2022
540
1,383
Mwanaume mmoja amemfumania mkewe aliye mjamzito akifanya mapenzi hospitalini alikokuwa amelazwa akitibiwa malaria.

Mwanamke huyo alilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Apac nchini Uganda kwa siku tano na fumanizi hilo lilitokea mume alipomtembelea mkewe muda wa kuona wagonjwa.

Badala ya kupokelewa na sura ya maumivu yatokanayo na maradhi yanayomsumbua mkewe, mume huyo alimfuma mkewe akifanya kitendo hicho na kijana mdogo wa miaka 24 tu ambaye huchoma nyama mjini hapo.

Baada ya kufumaniwa, kijana huyo alikimbia wakati mume akiwa na mshangao wa alichokishuhudia lakini alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi ambako amefunguliwa mashtaka aliyoyakiri.

Gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda linaripoti kuwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Apac, Davis Ndaula amethibitisha kushikiliwa kwa kijana huyo ambaye aliwapa shida kesi ya kumfungulia lakini baada ya kutafakari akashtakiwa kwa kusababisha kero kwa umma kwa kitendo alichokifanya katika wodi ya wanawake hospitalini hapo.

“Mume wa huyu mwanamke alikuja kumjulia hali mkewe aliyelazwa hospitalini kwa siku tano lakini akamfumania akiwa na kijana huyo wakijamiiana kwenye kitanda cha hospitali,” amesema shuhuda ambaye hakutaka kutajwa jina.

Mwananchi 2023
 
Mwanaume mmoja amemfumania mkewe aliye mjamzito akifanya mapenzi hospitalini alikokuwa amelazwa akitibiwa malaria...
Mi huwa sielewi starehe ya mapenzi inayotumia akili na ufahamu wa mtu, namna gani watu wengine wanavyolifanya na kulichukulia!

Hivi saikolojia yako inaweza kukaa sawa na kupandisha mihemko ya mapenzi kwenye kadamnasi iliyopo sehemu ya umma?

Kuna siku nilishuhudia mke wa marehemu akizini na jamaa tuliokuwa pamoja kwenye msafara wa kusindikiza maiti ya mumewe kwenda kuzika kijijini kwao!

Tulipofika "senta" moja usiku umeingia tukaamua kulala ili alfajiri tuendelee na msafara.

Lakini maiti ya mume ipo garini, jamaa linachukua mke wa marehemu uchochoroni kwenda kufanya naye mapenzi!

Sa'huwa najiuliza mtu kama huyo anakuwa mtimilifu kiakili kweli?
 
Hakikisha unatumia hii, 1X3.
 

Attachments

  • IMG_20230114_120552.jpg
    IMG_20230114_120552.jpg
    29.3 KB · Views: 55
Back
Top Bottom