Briefly, ni 80% ya mishahara yao walipokuwa job, magari mawili SUV mapya kila mwaka, nyumba mbili za serikali Dar na Dodoma, Wafanyakazi wa ndani ya nyumba na nje wasiozidi watano, both Dar na dodoma, Askari wa kulinda nyumba zote mbili, safari za matibabu ulaya mara mbili kwa mwaka wao na wake zao na walinzi wakifuatana na mpishi mmoja na msaidizi wa karibu, free msosi wa government, walinzi wawili personal na mengineyo!
All this ni mpaka watakapoitwa kwenye haki.
Nina wasiwasi na hizi. Hasa hiyo ya magari na nyumba za Dodoma! Mwinyi ana nyumba gani Dodoma?
Najua wanalipiwa safari ya nje ambazo zinategemea cheo cha mhusika.
Najua wanapatiwa magari lakini sidhani kama ni mapya kila mwaka! Na idadi ya magari nayo inategemea cheo cha mhusika. Hiyo ya msosi.....................mmmhhhh!
Na hata hiyo ya safari ya matibabu imekaa kiaina! Pengine ni check-up inayozungumziwa? Safari ya matibabu si itategemea maradhi yake? Au akishauguwa mara mbili kwa mwaka inabidi ajijue akiugua mara ya tatu?
mkuu fmes.i salute you.1.
Mkuu kama hujui ni kuuliza sio kurukia rukia usioyajua, haya huyajui hawa wakulu siku zote niko nao ninawaona kwa karibu tena sana, ndio maana ninayajua haya sio kwa kusimuliwa, miwnyi kama marais wengine wote wastaafu na mawaziri wakuu wastaafu, ana nyumba ya serikali dar na dodoma, othewise useme sasa akiwa dodoma anakaa wapi? Au kwa nani?
Kwa taarifa yako nyumba yake iko area c, ambako pia kuna makazi ya msuya, warioba, salim, na kingunge, lakini wengine kina malecela, kawawa, mawaziri viongozi wa zenji, katibu mkuu wa ccm wako kilimani area karibu na nyumba ya waziri mkuu ukipita kituo cha relwe, kuelekea dodoma hotel.
2.
Nonesense! Maraisi wanalipwa hela tofauti na mawaziri wakuu, kwa sababu hawafanani mishahara, kwa hiyo 80% ya mshahara wa waziri mkuu haiwezi kuwa sawa na 80% ya raisi mstaafu,
wanapokwenda nje wanalipiwa kila kitu na posho ikiwa ni pamoja na first class ticket ya anything kuanzia ndege mpaka treni, walinzi wawili, mke, mpishi na msaidizi mmoja wa ndani,
however, rais mstaafu anasafiri na at least watu kumi na wote wanalipiwa na serikali, na pia ana bajeti maalum kwa ajili ya shughuli za serikali na siku zote anakuwa standby iwapo atahitajiwa na the sitting rais kwenda popote kumuwakilisha
3.
Another nonesense, wakitoka kwenye power kwanza wanachukua benzi mbili walizokuwa wakizitumia a ll the time kwa kazi za official, zinakuwa zao binafsi, on top of that serikali inatoa suv mbili moja kwa mke moja kwa mstaafu mwenyewe, na ni wajibu wa serikali kuyabadilisha kila mwishoni mwa mwaka,
so far wengi wao wamekuwa hawajali sana, lakini kuna mmoja anayefuatilia kila mwaka na kubadilishiwa, nyumba zao dar na dododma ni lazima zifanyiwe ukarabati kila mwisho wa mwaka, wote wana bajeti maalum ya kuhakikisha kuwa bustani zao zinatunzwa ipasavyo, mazingira ya nyumba zao yanatunzwa ipasavyo, na chakula juu, hizi hela hupewa kiongozi wa wasaidizi wote wa mstaafu.
4.
Kama kuna aina hapo ni moja tu nayo ni wewe kutokujua unachokisema, wastaafu wanatakiwa kwenda europe, us au nje tu ya nchi mara mbili kwa mwaka, kwa ajili ya medical check-up, all paid by the government, hii ni must!
Kuugua has nothing to do na hii medical check-up, ila inakuwa covered na dharura ikitokea anakwenda anyways, i mean hata kama ameshakwenda kuchekiwa mara mbili na mwaka haujaisha akiguaa ghafla anakwenda, ndio maana kawawa siku zote yupo london kuitbiwa, sio kwa bahati mbaya!
Ahsante mkuu!
Hayo magari kama wanapewa mapya kila mwaka ( ulivyodai awali), basi sasa hivi Mwinyi angekuwa na zaidi ya 40
Another nonesense, wakitoka kwenye power kwanza wanachukua benzi mbili walizokuwa wakizitumia a ll the time kwa kazi za official, zinakuwa zao binafsi, on top of that serikali inatoa SUV mbili moja kwa mke moja kwa Mstaafu mwenyewe, na ni wajibu wa serikali kuyabadilisha kila mwishoni mwa mwaka,
FMES......heshima mbele mkuu
......hao wanaojiuliza uliza naona wanataka kupata habari toka kwako........na wala si jingine..........wee rudia kusoma maswali/doubts yao/zao utagundua nasema nini......
FMeS! Tatizo lako ni hayo majigambo na lugha ya matusi. Si wewe peke yako uliyekaribu na hao viongozi. Mimi binafsi sioni sababu ya kukuamini ati kwa sababu unadai hawa ni maswahiba zako. Wewe unakaa nao lakini wengine ndiyo wanaohusika katika kutayarisha hayo mafao. Mimi ningekuamini zaidi ungetaja waraka wa serikali unaotoa hizo stahili zote ulizozitaja. Mpaka sasa ushahidi wako haujani'convince'.
Ujue kuna tofauti kati ya kutengewa nyumba na kupewa nyumba. Nyumba ya Mkapa Masaki amepewa wala si kutengewa. sasa hiyo ya Dodoma aliyopewa ni ipi? Nyumba hizo za Dodoma wametengewa, bado ni za serikali. Kama walizinunua wenyewe au kujenga wenyewe na wangependa kuendelea kuzitumia, serikali inachukua jukumu ya kuzitunza na kuzifanya makazi RASMI ya mhusika.
Hayo magari kama wanapewa mapya kila mwaka ( ulivyodai awali), basi sasa hivi Mwinyi angekuwa na zaidi ya 40, maana la zamani harudishi kama walipewa. Uliponijibu ndiyo ukaelezea kuwa wanatengewa na serikali magari mawili kila mwaka (sio yao) ambayo wakishayatumia bila shaka yanarudi kwenye pool ya magari ya serikali. Usemi wako wa mwanzo ungewafanya baaadhi ya watu waamini kuwa hawa wastaafu wana mlundiko wa magari wliyonunuliwa na serikali wakati si hivyo.
Unachanganya tena mada. Hii mada inahusu viongozi wa serikali (si CCM) na hawa wanajumuisha Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu, Spika, Jaji Mkuu. Wewe umekurupukia Rais peke yake. Hawa wengine nao wanastahili zao ambazo zinaendana na cheo chao na si mshahara wao. Si wote kwa mfano wanaojengewa nyumba wakistaafu. Baadhi yao wanatengewa makazi kwa ajili ya matumizi yao. Wakifariki, yanarudi serikalini.
Stahili ya mheshimiwa Rais mstaafu ni safari mbili nje ya nchi, kila mwaka, bila kujali ameenda kwa ajili ya nini. Hizi analipiwa kila kitu. Sasa wewe mwenzetu, swahiba wao, unataka kutudanganya kuwa hizi ni za matibabu tuu! Safari ya matibabu (ulivyotaka kutudanganya) ni tofauti na ya check-up. Ndiyo maana nikapinga logic yako. Rais mstaafu akiugua anahaki ya kutibiwa popote inapobidi bila kujali mara ngapi ameugua.
Wakati unamlaumu Kuhani uwe unajiangalia na wewe mwenyewe.
Amandla............
Briefly, ni 80% ya mishahara yao walipokuwa job, magari mawili SUV mapya kila mwaka, nyumba mbili za serikali Dar na Dodoma, Wafanyakazi wa ndani ya nyumba na nje wasiozidi watano, both Dar na dodoma, Askari wa kulinda nyumba zote mbili, safari za matibabu ulaya mara mbili kwa mwaka wao na wake zao na walinzi wakifuatana na mpishi mmoja na msaidizi wa karibu, free msosi wa government, walinzi wawili personal na mengineyo!
All this ni mpaka watakapoitwa kwenye haki.
Haya yote ni nonesense, hujui unachokisema nitakusaidia baadaye nikirudi tena, later bro!
Yote niliyoyasema nimeyaona wakifanyiwa, ya katiba sijui inasema nini ila ninajua ilipitishwa in the middle ya 90s