Posho ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma ikoje?

SUTAGI-

JF-Expert Member
Nov 9, 2018
273
513
Posho ni malipo ambayo hulipwa kwa mtumishi wa umma kwa kuzingatia kiwango cha mshahara na mahali anapofanyia kazi.

Kwa maana hiyo tunaweza kuwa na kiwango sawa cha mshahara tukishiriki shughuli moja lakini tukalipwa viwango tofauti vya posho kwa sababu ya maeneo tuliyotokea.

Kwa mfano:

Kama kuna semina inafanyikia Dodoma mjini kwa maafisa elimu wote wa wilaya za Tanzania. Maafisa hao kama watakuwa na kiwango sawa cha mshahara watalipwa kiwango sawa cha posho isipokuwa afisa elimu wa wilaya ya Dodoma ambaye atalipwa nusu ya kiwango walicholipwa wengine wote.

Hii ni kwa sababu yeye yupo ndani ya wilaya ambayo semina inafanyika

Swali:

Je, Posho ya Mbunge wa jimbo la Dodoma ambaye anawakilisha wananchi katika eneo ambalo ndiko zilipo ofisi za Bunge analipwa sawa na wabunge wenzake toka maeneo mengine ya Tanzania?

Kama posho yake ni sawa na wenzake, Je sheria na taratibu za malipo ya posho za wabunge ni tofauti na watumishi wengine wa umma?
 
ndugu afisa Elimu, unatokea kata gani?🐒
 
Back
Top Bottom