Bilioni 1.7 Kulipa Posho za Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,033
974

Bilioni 1.7 Kulipa Posho za Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa

Serikali imeendelea kulipa posho za wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa posho wenyeviti wa vitongoji na vijiji na kuongeza posho ya Madiwani ili kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

“Katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.7 ambapo kufikia Februari, 2024 shilingi Bilioni 1.15 zimetolewa kwa ajili ya kulipa posho za wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa.” amesema Dkt. Dugange

Aidha amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imetenga shilingi Bilioni 20.8 kwa ajili ya kulipa posho za Madiwani katika halmashauri 168 ambapo kufikia Februari, 2024 kiasi cha shilingi Bilioni 13.5 kimetolewa.
 
Attachments

  • imagesqasxdsza.jpg
    imagesqasxdsza.jpg
    14.2 KB · Views: 3
  • GKYZLPfWoAA2DzA.jpg
    GKYZLPfWoAA2DzA.jpg
    343.4 KB · Views: 2

Bilioni 1.7 Kulipa Posho za Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa

Serikali imeendelea kulipa posho za wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa posho wenyeviti wa vitongoji na vijiji na kuongeza posho ya Madiwani ili kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

“Katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.7 ambapo kufikia Februari, 2024 shilingi Bilioni 1.15 zimetolewa kwa ajili ya kulipa posho za wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa.” amesema Dkt. Dugange

Aidha amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imetenga shilingi Bilioni 20.8 kwa ajili ya kulipa posho za Madiwani katika halmashauri 168 ambapo kufikia Februari, 2024 kiasi cha shilingi Bilioni 13.5 kimetolewa.
1.7B kwa mwaka? ambayo ni posho ya mbunge mmoja kwa mwaka?
 
Msiwakasirishe Wenyeviti wa Vijiji/Mitaa. Hakuna fedha iliyolipwa kwa wahusika. Shahidi ni Mwenyekiti wangu wa Mtaa.
 
Hakuna mwenyekiti wa kijiji au mtaa anayelipwa nchi hii zaidi ya hela kidogo wazipatazo watoapo huduma mfano wapiga kura wao kugongewa muhuri
 
Back
Top Bottom