Miaka 60 ya Muungano imegubikwa na kamata kamata za polisi kuliko mijadala ya kitaifa? Nani yupo nyuma ya hujuma ya 4R za Rais?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
912
4,249
Vyombo vya habari zimeripoti mambo mengi ya Muungano lakini wananchi wamekataa kujadili na kusambaza habari njema ya uzima wa Muungano.

Mtaani hakuna mtu anahangaika na gwaride wala hotuba watu wapo busy kujadili picha za waliopotea. Boniface na Malisa wameteka mijadala ya ndani na muda si mrefu wataingia kwenye vyombo vya habari vya nje.

Akaunti za hawa watu za mitandao ya jamii zimejaa picha za watu waliopotea. Wageni wakiingia kwenye akaunti zao kutokana na habari kutoka vyombo vya nje watakata tamaa kuitembelea Tanzania.

Tumeona kelele za mitandao zilivyovuruga hadi benki ya dunia kusitisha ufadhili wa miradi ya maendeleo. Haya yote yanafanywa na watu waliopo nyuma ya mfumo kwa malengo yao

Nakumbuka JPM na ukali wake lakini siri za utawala wake zilikuwa zinavuja na kwenda kwa akina Kigogo. Yeye JPM aliaminishwa kwamba wapinzani ndio wanatoa siri na hakuwahi kujiuliza kama wapinzani wanapataje siri wakati hawapo Ikulu? Finally kila kiumbe mwenye akili alikuja kugundua kwamba wale JPM aliowaamini sana ndio walikuwa maadui zake.

Hali pia inatokea kwenye utawala wa SSH, anapofanya sherehe za miaka 60 then polisi wanakwenda kukamata watu wanaozua taharuki na kuwaondolea wananchi morali yakushiriki shughuli za Muungano; ni kweli kwamba intelijensia haikuona madhara ya ukamataji huu?

Leo mwitikio Taifa ni mdogo sana, sijui labda hali ya hewa huko DAR ni mbaya sana ila napata mashaka na wanaomsaidia Mh. Rais. Wanaweza wakawa wanaruhusu baadhi ya mambo yafanyike kwa hujuma bila yeye kufahamu.

Kwa mtazamo wangu tukio lakukamata wapinzani lilipaswa kufanyika Jumatatu wakati sherehe zimeisha. Wamesubiri usiku wa mkesha wa muungano ndipo wamewakamata ili wananchi wapate agenda mitandaoni.

Lakini pia kwanini viongozi wa vyama vya siasa wamepoteana ; Hawa wanaandamana wale wanasherekea Muungano. Wapi zilipopotea zile 4R? Hakuna tenda uvumilivu, maridhiano na ustahimilivu?

Naamini vita ya ubunge na urais ndani ya CCM inakwenda kupelekea ukatili kama aliouacha JPM.......Wasaidizi wa Mhe. Rais angalieni sana wale mliowaamini si wote wana misaada kwenu wengine ni mamluki.
 
Huyu jamaa anakuwaga jirani na Samia ni nani? Utakuta sometimes anaelekezana na Samia.
 
Back
Top Bottom