JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 631
- 960
MDAHALO KUHUSU MITANDAO YA KIJAMII KWA VIJANA TANZANIA
Katika mwendelezo wa kuibua mawazo na mijadala katika suala la matumizi ya Mitandao ya Kijamii na Mtandao wa Internet kwa ujumla, JamiiForums imeandaa mdahalo kabambe kuhusu Mitandao ya Kijamii nchini Tanzania.
Lengo kuu la mdahalo ni kuibua hoja za msingi kutoka pande mbili zinazokinzana na kuzijadili kujua ukweli, maana, faida na hasara zake. Baada ya mdahalo wabobezi katika fani husika huchambua hoja zilizotolewa kitaalamu na wote kutoka na wazo moja litakalotusaidia katika maisha yetu na hata uhamasishaji kwa wengine.
Mdahalo utakaofanyika jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 13 Oktoba 2018, utahusisha wanafunzi wa Vyuo na Wasomi mbalimbali kutoka fani mbalimbali.
=> Je, wewe ni mwanafunzi au mhitimu wa Elimu ya juu? Una umri wa kati ya miaka 20 na 35? Unapendelea kushiriki mijadala kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii(social media)? Basi unaweza Kushiriki.
Maombi ya ushiriki yatafanyika mtandaoni kwa kufuata kiunganishi hiki >> JamiiTalks Debate Application
Mwisho wa kupokea maombi ni Ijumaa tarehe 5 Oktoba 2018 saa 11 jioni.
Karibuni.
Mdahalo uliopita >> "NAFASI ZA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI" - Yaliyojiri katika Mdahalo wa Wanachuo New Africa Hotel - JamiiForums