Mbunge Santiel Kirumba Ataka Serikali Kutatua Changamoto ya Ajira Kwenye Miradi ya Kimkakati ya SGR Mkoani Shinyanga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,021
969

MBUNGE SANTIEL KIRUMBA Ataka Serikali Kutatua Changamoto ya Ajira Kwenye Miradi ya Kimkakati ya SGR Mkoani Shinyanga

Swali la Mhe. Santiel Eric Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga aliyetaka kufahamu, Serikali ina mpango gani kutatua changamoto ya ajira kwenye Miradi ya Kimkakati Standard Gauge Railway (SGR) kwa Mkoa wa Shinyanga?

"Mpaka Machi 2024, Mradi wa SGR imetoa ajira kwa watanzania 30,176 za moja kwa moja na 150,880 zisizo za moja kwa moja. Kati ya hao, kipande cha Mwanza - Isaka walikuwa 6,826 kati ya hao, wafanyakazi 2,070 wanatoka Mkoa Mwanza, 1,387 Shinyanga, 365 Tabora, 376 Simiyu na 2,628 kutoka Mikoa mingine ya Tanzania kwa pamoja" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi

"Kwenye mradi wa SGR Ajira zimekuwa zikitolewa kimtandao, Nini kauli ya Serikali kuhakikisha Ajira ngazi ya chini ili watu wengi wapate fursa? Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza fedha nyingi sana katika MGR na SGR, Lini Utekelezaji huu utakamilika ili kutatua changamoto ya ajira hasa Mkoa wa Shinyanga? - Mhe. Santiel Eric Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga

"Ikumbukwe kuwa Taifa letu linajenga SGR ndefu kuliko nchi zote barani Afrika kwa sasa tuko karibu kilometa 2100 huku tukifuatiwa na Ethiopia km 700. Kutoka Dar - Mwanza kilometa 1219, Tabora mpaka Kigoma kilometa 506 wakandaras wako site. Kutoka Uvinza - Gitega Msongati kolometa 282 Nchini Burundi kwenye madini ya Nikeli tuko hatua za kumpata mkandaras, Kutoka Kaliua - Mpanda - Kalema kilometa 317, kutoka Isaka - Rusumo - Kigali Kilometa 495 study imekamilika tuko hatua ya kutafuta fedha, Reli ya Mtwara - Mbamba Bay kilometa 1,000 tuko hatua ya kuhuisha study na Reli ya Kaskazini Tanga- Arusha Musoma Kilometa 1028 tuko hatua ya kutafuta mtaalam wa uwekezaji" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi

"Kwenye SGR tumeashaanza majaribio ya Lot 1-4 Dar mpaka Makutupola. Kati ya Mabehewa ya Mizigo yanaingia hivi karibuni 250 na mengine yaliyobaki yataingia mwaka huu, Kati ya Vichwa vya Treni 17 vimeingia 9 bado 8 vitaingia by Oktoba. Seti za Treni za kisasa 10 imeingia seti moja na zilizobaki zotaingia mwaka huu" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi

"TAZARA yenye urefu wa KM 1860 kutoka Dar mpaka Kapilimposho Zambia iko kwenye hatua ya uboreshaji upya kupitia Makubaliano ya wakuu wa Nchi zote tatu (Tanzania, Zambia na China)" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-05-04 at 18.41.15(1).mp4
    38 MB
Back
Top Bottom