Mbinu watumiazo Mafundi Ujenzi kuibia mabosi zao

Ujenzi nafanya nikiwa likizo tu,kila kitu nanunua mwenyewe fundi akiniagiza cement mifuko 30 mimi nanunua mifuko 20 tu,mbao 150 mimi nanunua mbao 100 halafu naangalia kama itatosha isipotoshea ndio naagiza mingine. Nafanya hivi kwa sababu mafundi wetu wengi hawajui makadilio walishawahi kuninunulisha mabati 200 zikatumika bati 140 tu 60 zikabaki
Njia unayoitumia nami nimewahi kuitumia.

Changamoto yake Fundi aliniagiza Tiles boksi 160, nikamletea boksi 130.

Baadaye Tiles zikafeli hivyo kazi kusimama Kwa muda.

Nikalazimika kufata Tiles boksi 25 Kariakoo na nikatakiwa kusubiri maana sikuweza kupata nilizotumia Mwanzo🙌
 
1.Mbinu ya kwanza maarufu kabisa ni ya 'kukuelekeza Duka gani akanunue vifaa quality "... wengine atakwambia vifaa vyao sio Bora kihivyo...

Akishakuelekeza...lazima ataongea na mwenye duka au ni Duka lake maalum tayari...akisema Tu huyu ni mteja wangu...baasi wanajua waweke vipi cha juu chake...hapo utakuta kitu cha sh 3000 wenye Duka anakomaa 5000 au zaidi huku fundi wako anakwambia "ndo bei zake " hizi quality sana
You have said it all 🤝
 
Fundi ujenzi asiye muaminifu atakuibia kupitia moja ya mbinu hizi, kutegemeana na umakini wa wewe unayejengewa nyumba.

1. Kuzidisha bei za vifaa - Hii hutokea kama wewe mwenye nyumba ni mgeni sana na masuala ya vifaa vya ujenzi na materials. Hapa bei zitaongezwa kiholela na utaibiwa kizembe kabisa.

Unawezaje kuepuka hili? Usiwe na papara, kabla hata ya kutafuta fundi jipe walau wiki moja ya kuuliza bei ya vitu kwenye maduka yaliyo karibu na site yako lakini pia pitia maduka makubwa kama yale ya Kariakoo - Mtaa wa Swahili, Kipata na mengineyo na ukiweza walau pitia pale Mwenge lakini pia maeneo ya Buguruni, Veterinary n.k
Kama ni mjanja unaweza kupita kwenye kurasa za mitandao za makampuni na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi.

2. Kuzidisha idadi ya vifaa vinavyohitajika - Hapa nazungumzia ''materials'', hapa sasa kutegemeana na uzoefu wako wa masuala ya ujenzi, fundi atakutajia idadi kubwa ya materials zinazohitajika. Hapa atakuibia kwa namna mbili, moja kama utaenda kununua vifaa mwenyewe basi atavisubiri vifike eneo la ujenzi ili vile vinavyozidi akaviuze, njia ya pili kama ukimtuma yeye kwenda kununua basi hapo ataenda kununua idadi sahihi na hela ya vifaa alivyozidisha atabaki nayo kujipongeza kwa ujinga wako.

Hili unaweza kuepuka kwa kuwa na mtu mwenye utaalum wa mahesabu ya materials (Mkadiriaji Majenzi - QS) na usimamizi wa uhakika kwenye eneo lako la ujenzi.

3. Kuuza vifaa ulivyonunua - Hapa sasa kama amekukosa kwenye njia ya kwanza na ya pili.
Hapa fundi anaamua tu kwa makusudi kuuza ama kuchukua vifaa ulivyonunua kwa ajili ya ujenzi na kuuza. Hii hutokea sana kama eneo la ujenzi halina usimamizi kabisa. Hapa fundi umempelekea Gypsum board 50
sawasawa na hesabu na yeye anaamua tu kuchukua na kuuza Gypsum board 5. Hapa jioni unapokea simu kuwa kuna chumba hakijawekwa gypsum kwa kuwa zimeisha hivyo anakuomba kesho umpelekee gypsum boards 5 ili amalizie kazi.
Au kwa hesabu nyumba inahitaji ndoo tano za rangi, anaanza kazi huku anakwambia kuwa zinatosha, saa tisa , mchana anakutumia meseji kuwa upande wa nyuma hajapiga rangi kwa kuwa rangi imeisha hivyo umletee ndoo moja amalize kazi. Hiyo ndoo moja ameamua kuichukua na kuuza. Hii hufanywa sana wakati wa finishing; gypsum, tiles, rangi n.k

Unaweza kukabiliana na hili kwa kuwa na usimamizi wa uhakika kwenye eneo lako la ujenzi.

4. Kushirikiana na wauza vifaa vya Ujenzi - Hii hutokea fundi anapojua kabisa kuwa hautampa hela ya kwenda kununua vifaa na mtaongozana kwenda dukani kununua vifaa vya ujenzi. Atakachofanya ni kuwa na ushawishi wa kukuelekeza duka la kwenda kununua vifaa.
Hapa atampa taarifa mwenye duka kuwa kuna mteja namleta na hajui bei, hivyo kwenye bei ongeza hela ya juu. Ukifika dukani utashangaa kuona fundi wako anaunga mkono kila bei unayotajiwa lakini pia akisisitiza kuwa katika eneo hilo ni duka hilo ndio bidhaa zake ni bora zaidi.
Unanunua vifaa vya Milioni mbili na Laki tatu kumbe bei halisi ni Milioni Mbili kamili.

Njia ya kuepuka hili ni kuwa taarifa za bei kabla ya kwenda dukani na kutomshirikisha fundi kwenye wapi ukanunue vifaa vya ujenzi.

5. Kutumia mafundi wenzake kwenye kuzidisha bei - Hapa sasa una fundi wa ujenzi ambaye anajenga nyumba halafu umefika hatua fulani kwenye ujenzi unamuulizia kama anamfahamu fundi bomba (Plumber) au umeme (electrician). Hapa fundi akimleta huyo fundi bomba au fundi umeme ujue amashampanga azidishe bei ili na yeye apate chochote kitu.

Njia ya kuepuka hili ni kujua gharama za hizi kazi na kutomshikisha fundi wako kukutafutia mtaalamu wa haya mambo mengine.

6. Fundi kubaki na materials na vifaa vingine ambavyo ulinunua kwa ajili ya ujenzi - hapa sasa ndipo watu huwa wanawapa mafundi faida bila kujua. Unakuta unajenga nyumba na fundi anakwambia yanahitajika machepe, mbao za jukwaa, ndoo, mbao za kufungia column, beam , lintel na zile za slab. Unanunua vitu hivi kwa ajili ya nyumba yako. Lakini mwisho wa ujenzi hata wala hukumbuki kama kuna vitu ulinunua ili kurahisisha ujenzi wa nyumba yako. Fundi anatoka site akiwa na vitu vingi ambavyo sio mali yake ila wewe mwenye nyumba hujui kuwa zile ni mali zako.

Jinsi ya kuepuka hili ni kujua kuwa vifaa ulivyonunua wakati wa ujenzi ni mali yako na sio mali ya fundi.
 
Kwenye hii thread tutakuwa tuna share Mbinu za wizi za mafundi ujenzi ili kusaidia wale wanaotaka kujenga "wasipigwe ".

Wengi tumepigwa sana hadi kuzijua hizi mbinu.

Karibuni.

Hili somo Ni la muhimu Sana, kuepuka kujenga nyumba kwa gharama kubwa. Kumbe moja ya tatu ya gharama yote ya ujenzi aliichukua fundi
 
Mafundi wanazingua sana, kwa mtu asiye na uelewa japo kidogo kwa hiko anachokifanya fundi lazima amchezeshe!
Hii ni kama tabia asili ya ufundi.

Lakini pia hii ni kwa mafundi wasioenda na wakati, kuna semina na mafunzo yanatolewa jinsi gani fundi atafaidika na kazi yake ya ufundi bila kumuibia mteja wake.
Pia mafunzo ya ujasiriamali ambao unafundishwa kuufanya ufundi wako kama biashara yenye mtaji na faida.
Kwa mtu ama fundi anaefanya kazi zake kwa kujifunza hawezi kuwea tegemeo la faida kubwa kwa kumzidishia mteja garama za vifaa vya ujenzi nk.

Unapopata kazi ya kutoka kwa mtu ni kama mteja amekuja kwenye biashara yako kama mwenye duka, unabidi umfanye awe mteja wako na kuwa balozi wa kazi yako, kama kibiriti kwenye duka A kinauzwa 100 na kina njiti 45 basi na dukani kwako iwe hivyo hivyo.
Fundi yoyote anaezingati mengi pamoja na hayo hawezi kumpoteza mteja na hata kuwa na upungufu wa kazi.

Pia wateja nao wanamchango mkubwa wa fundi kutokuwa mwaminifu, kazi ya ufundi unatumia akili nyingi na nguvu nyingi na muda mwingi kufanikisha, ila mteja anakubana kwenye malipo yako mpaka inafika nusu bei!
Na hii nikutokana na ufundi na fundi kutokuwa na thamani kwenye jamii ni kazi inayochukuliwa ya kawaida mno ingawa inahitajika, hivyo fundi ili kufidia walao japo kidogo , kama cement zingekuwa kumi basi lazima akuambie 12.
Au hizo kumi atatumia 8 kwa kupunguza ubora ili aweze walao kufidi muda nguvu na akili zitakazotumika.

Pia sheria za ufundi hupaswi kufanya makadirio kamili ya vifaa vya kazi bali uzidishe, ila uzidishapo iwe ni kuzidi kwa kiasi na mwenye kazi anashirikishwa vifaa vikivyobaki baada ya kazi .
Mkuu unaongea kisiasa na uaminifu, yote hayo ya nini?

Hapa tunataka tuelekezane mbinu chafu zinazotumiwa na mafundi kufirisi matajiri zao.

Zungumzia mbinu za upigaji wanazozitumia mafundi ili kuwanusuru wale wenye mipango ya ujenzi ili wapate mbinu za kujisimamia na kuwadhibiti mafundi pindi waanzapo miradi yao ya ujenzi.
 
Tatizo kubwa lipo kwa mteja,yaan mteja yupo tayari kununua vifaa kwa gharama yeyote,njoo sasa kwenye mapatano ya ufundi ndio utacheka.

Hii imepelekea mafundi bora kukusanya nusu nusu,maana nusu kwenye vifaa na nusu kwenye ujenzi ili apate,lakini kama tungenyooka kwenye malipo ya ufundi haya yote yasingetokea,mimi sio fundi ujenzi lakini.
 
Maskini tunaojenga tuna taabu saana. Hata sisi huko maofisini tunapiga kwa nafasi yetu.

Dukani hulii lii bei njoo kwa fundi sasa. Unataka umnyonye why asikupige?
Unanunu materials mamilioni fundi anayefanyia kazi hayo materials ya mamilioni unampunja. Kazi unaitaita mafuñdi zaidi ya watano kuangalia nani kapunguza hata 20000 eti ndio umpe kazi.

Hapa unamsema fundi unasahau hata ww huko kazini kwako unapiga... Kama ni biashara unaipiga serikali kwenye kodi.
 
Mafundi wanalalamikiwa bure,na hali hii ndio imepelekea kuwa mazoea kwa hiyo hata wewe ukiwa na lengo la kumlipa fundi vizuri anaona wote ndio walewale.

Mimi fundi simu nipo kariakoo, anaweza akaja mteja ukamwambia kioo kinauzwa 50,000 na akakubali kabisa,sasa mwambie ufundi 20,000 au 15,000 kama atakubali kutoa atakwambia nina 5000.

Kama asingezaulika fundi basi haya yasingetokea,ila kweli mteja yupo tayari kununua bidhaa(materia)kwa bei kubwa lakini si kumlipa hela nzuri fundi.
 
Yaani umejibu vzr sana. Kwa kuwa uko kwenye idara husika.
 
Mafundi ujenzi, welding, mafundi wa vitu vya kielectroniki wote ni wezi tu.

Kuna jamaa yangu ni fundi welding anasema yeye lazima akuibie hata ulinde vipi.

Na muuzaji yeyote wa hardware anajua kula na mafundi maana hao ndo wanamletea wateja.

Kama hujui kabisa ishu za ujenzi utapunguza kwa rate ndogo kupigwa ila utapigwa, na kama unajua mambo ya ujenzi na material unanunua mwenyewe utapigwa kidogo maana utamkaba koo.
 
Fundi ujenzi asiye muaminifu atakuibia kupitia moja ya mbinu hizi, kutegemeana na umakini wa wewe unayejengewa nyumba.

1. Kuzidisha bei za vifaa - Hii hutokea kama wewe mwenye nyumba ni mgeni sana na masuala ya vifaa vya ujenzi na materials. Hapa bei zitaongezwa kiholela na utaibiwa kizembe kabisa.

Unawezaje kuepuka hili? Usiwe na papara, kabla hata ya kutafuta fundi jipe walau wiki moja ya kuuliza bei ya vitu kwenye maduka yaliyo karibu na site yako lakini pia pitia maduka makubwa kama yale ya Kariakoo - Mtaa wa Swahili, Kipata na mengineyo na ukiweza walau pitia pale Mwenge lakini pia maeneo ya Buguruni, Veterinary n.k
Kama ni mjanja unaweza kupita kwenye kurasa za mitandao za makampuni na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi.

2. Kuzidisha idadi ya vifaa vinavyohitajika - Hapa nazungumzia ''materials'', hapa sasa kutegemeana na uzoefu wako wa masuala ya ujenzi, fundi atakutajia idadi kubwa ya materials zinazohitajika. Hapa atakuibia kwa namna mbili, moja kama utaenda kununua vifaa mwenyewe basi atavisubiri vifike eneo la ujenzi ili vile vinavyozidi akaviuze, njia ya pili kama ukimtuma yeye kwenda kununua basi hapo ataenda kununua idadi sahihi na hela ya vifaa alivyozidisha atabaki nayo kujipongeza kwa ujinga wako.

Hili unaweza kuepuka kwa kuwa na mtu mwenye utaalum wa mahesabu ya materials (Mkadiriaji Majenzi - QS) na usimamizi wa uhakika kwenye eneo lako la ujenzi.

3. Kuuza vifaa ulivyonunua - Hapa sasa kama amekukosa kwenye njia ya kwanza na ya pili.
Hapa fundi anaamua tu kwa makusudi kuuza ama kuchukua vifaa ulivyonunua kwa ajili ya ujenzi na kuuza. Hii hutokea sana kama eneo la ujenzi halina usimamizi kabisa. Hapa fundi umempelekea Gypsum board 50
sawasawa na hesabu na yeye anaamua tu kuchukua na kuuza Gypsum board 5. Hapa jioni unapokea simu kuwa kuna chumba hakijawekwa gypsum kwa kuwa zimeisha hivyo anakuomba kesho umpelekee gypsum boards 5 ili amalizie kazi.
Au kwa hesabu nyumba inahitaji ndoo tano za rangi, anaanza kazi huku anakwambia kuwa zinatosha, saa tisa , mchana anakutumia meseji kuwa upande wa nyuma hajapiga rangi kwa kuwa rangi imeisha hivyo umletee ndoo moja amalize kazi. Hiyo ndoo moja ameamua kuichukua na kuuza. Hii hufanywa sana wakati wa finishing; gypsum, tiles, rangi n.k

Unaweza kukabiliana na hili kwa kuwa na usimamizi wa uhakika kwenye eneo lako la ujenzi.

4. Kushirikiana na wauza vifaa vya Ujenzi - Hii hutokea fundi anapojua kabisa kuwa hautampa hela ya kwenda kununua vifaa na mtaongozana kwenda dukani kununua vifaa vya ujenzi. Atakachofanya ni kuwa na ushawishi wa kukuelekeza duka la kwenda kununua vifaa.
Hapa atampa taarifa mwenye duka kuwa kuna mteja namleta na hajui bei, hivyo kwenye bei ongeza hela ya juu. Ukifika dukani utashangaa kuona fundi wako anaunga mkono kila bei unayotajiwa lakini pia akisisitiza kuwa katika eneo hilo ni duka hilo ndio bidhaa zake ni bora zaidi.
Unanunua vifaa vya Milioni mbili na Laki tatu kumbe bei halisi ni Milioni Mbili kamili.

Njia ya kuepuka hili ni kuwa taarifa za bei kabla ya kwenda dukani na kutomshirikisha fundi kwenye wapi ukanunue vifaa vya ujenzi.

5. Kutumia mafundi wenzake kwenye kuzidisha bei - Hapa sasa una fundi wa ujenzi ambaye anajenga nyumba halafu umefika hatua fulani kwenye ujenzi unamuulizia kama anamfahamu fundi bomba (Plumber) au umeme (electrician). Hapa fundi akimleta huyo fundi bomba au fundi umeme ujue amashampanga azidishe bei ili na yeye apate chochote kitu.

Njia ya kuepuka hili ni kujua gharama za hizi kazi na kutomshikisha fundi wako kukutafutia mtaalamu wa haya mambo mengine.

6. Fundi kubaki na materials na vifaa vingine ambavyo ulinunua kwa ajili ya ujenzi - hapa sasa ndipo watu huwa wanawapa mafundi faida bila kujua. Unakuta unajenga nyumba na fundi anakwambia yanahitajika machepe, mbao za jukwaa, ndoo, mbao za kufungia column, beam , lintel na zile za slab. Unanunua vitu hivi kwa ajili ya nyumba yako. Lakini mwisho wa ujenzi hata wala hukumbuki kama kuna vitu ulinunua ili kurahisisha ujenzi wa nyumba yako. Fundi anatoka site akiwa na vitu vingi ambavyo sio mali yake ila wewe mwenye nyumba hujui kuwa zile ni mali zako.

Jinsi ya kuepuka hili ni kujua kuwa vifaa ulivyonunua wakati wa ujenzi ni mali yako na sio mali ya fundi.
Mkuu umejitahidi kuangazia rough nyingi za mafundi lakini yote uliyoandika nimeona kuwa bado yameacha mianya ya 'tajiri' kupigwa na fundi, hasa kwa mambo madogo madogo usipoyachukulia serious!

Cha kwanza muhimu kabisa kama umeanza ujenzi, hata kama una pesa kiasi gani, jishushe na kuuweka pembeni uboss wako, kubali kutembea na kuzurula madukani, maana humo madukani ndipo hasa palipo na vyanzo vya hela za bakshishi za maana kwa mafundi na wewe kuweza kujenga nyumba yako kwa gharama halisi.

Usije ukaridhika na usimamizi unaoufanya hadi pale kazi hiyo unayoisimamia itakapokuwa imemalizika kwa ukamilifu wake.

Kwa mfano, kwa siku hiyo umemuuliza fundi atafyatua tofari ngapi akakueleza atafyatua tofari 1000 umpatie mifuko 25 kwa ratio ya karai 40 kwa mfuko, basi cha kufanya mpatie hiyo mifuko, usimamie inavyofumuliwa na kuchanganywa yote na pia tofari zote zifyatuliwe unashuhudia,, hapo kazi itakuwa imekwenda barabara.

Ukisema wafumue mifuko wachanganye halafu uridhike kwamba tayari na wewe uondoke, baba hapo utakuwa umepigwa na tofari zako zitapukutika kwa ratio kubwa ya mchanga.

Ipo hivii, kuna washenzi mitaani wana kariba za kufyatulia tofari majumbani zipo stand by kupokea tope la wizi.

Ndoo ya tope la saruji iliyochanganywa tayari ni sh. 500 na ndoo moja ya lt10 iliyojaa inafyatua tofari moja lililokamilika.

Hivyo fundi ama msaidizi akizoazoa tope na kulikimbiza sehemu anaweza akaondoka hadi na sh 5,000 site akiwa mwepesi.

Halafu usiweke mkataba na fundi wa kuhesabiana siku kwa kutwa, hapo ndipo utashuhudia materials zikihujumiwa kwa mfano saruji iliyochanganywa kumwagwa pindi masaa yakifika mwisho na saruji iliyochanganywa ikawa bado ipo.

Ingia mkataba wa kumaliza kazi yote ama mhesabiane tofari kama ni kazi ya kutwa na usimamizi uwe tight.

Fundi asishirikishwe kwa ushauri wowote kuhusu project hiyo na kama hauna uwezo wa kupiga mahesabu ya kitaalamu, mshirikishe fundi mwingine asiyehusika na kazi hiyo.

Mbinu za kufukia mifuko ya saruji na vifaa vingine kwenye michanga na baadaye kuvirudia ni uzembe wa wenye miradi kujiona ni maboss wasiostahili kusimamia kwa ukaribu na kwamba wanaona kumsimamia kwa ukaribu fundi ni kumkwaza.
 
Mafundi ujenzi, welding, mafundi wa vitu vya kielectroniki wote ni wezi tu.

Kuna jamaa yangu ni fundi welding anasema yeye lazima akuibie hata ulinde vipi.

Na muuzaji yeyote wa hardware anajua kula na mafundi maana hao ndo wanamletea wateja.

Kama hujui kabisa ishu za ujenzi utapunguza kwa rate ndogo kupigwa ila utapigwa, na kama unajua mambo ya ujenzi na material unanunua mwenyewe utapigwa kidogo maana utamkaba koo.
Mi huyo fundi welding tungelikuwa jiofrafia moja ningelimtafuta na kumpatia kazi ili nione akili zake zinapoishia.

Mi siibiwi kwa udanganyifu wa bei wala kuzidishiwa idadi.

Mbinu za kuniibia mimi mpaka ajifunge vikaze, ama aje kijambazi kwa kuvunja.
 
Back
Top Bottom