Mbinu watumiazo Mafundi Ujenzi kuibia mabosi zao

1.Mbinu ya kwanza maarufu kabisa ni ya 'kukuelekeza Duka gani akanunue vifaa quality "... wengine atakwambia vifaa vyao sio Bora kihivyo...

Akishakuelekeza...lazima ataongea na mwenye duka au ni Duka lake maalum tayari...akisema Tu huyu ni mteja wangu...baasi wanajua waweke vipi cha juu chake...hapo utakuta kitu cha sh 3000 wenye Duka anakomaa 5000 au zaidi huku fundi wako anakwambia "ndo bei zake " hizi quality sana
 
Ujenzi nafanya nikiwa likizo tu,kila kitu nanunua mwenyewe fundi akiniagiza cement mifuko 30 mimi nanunua mifuko 20 tu,mbao 150 mimi nanunua mbao 100 halafu naangalia kama itatosha isipotoshea ndio naagiza mingine. Nafanya hivi kwa sababu mafundi wetu wengi hawajui makadilio walishawahi kuninunulisha mabati 200 zikatumika bati 140 tu 60 zikabaki
 
Mafundi wanazingua sana, kwa mtu asiye na uelewa japo kidogo kwa hiko anachokifanya fundi lazima amchezeshe!
Hii ni kama tabia asili ya ufundi.

Lakini pia hii ni kwa mafundi wasioenda na wakati, kuna semina na mafunzo yanatolewa jinsi gani fundi atafaidika na kazi yake ya ufundi bila kumuibia mteja wake.
Pia mafunzo ya ujasiriamali ambao unafundishwa kuufanya ufundi wako kama biashara yenye mtaji na faida.
Kwa mtu ama fundi anaefanya kazi zake kwa kujifunza hawezi kuwea tegemeo la faida kubwa kwa kumzidishia mteja garama za vifaa vya ujenzi nk.

Unapopata kazi ya kutoka kwa mtu ni kama mteja amekuja kwenye biashara yako kama mwenye duka, unabidi umfanye awe mteja wako na kuwa balozi wa kazi yako, kama kibiriti kwenye duka A kinauzwa 100 na kina njiti 45 basi na dukani kwako iwe hivyo hivyo.
Fundi yoyote anaezingati mengi pamoja na hayo hawezi kumpoteza mteja na hata kuwa na upungufu wa kazi.

Pia wateja nao wanamchango mkubwa wa fundi kutokuwa mwaminifu, kazi ya ufundi unatumia akili nyingi na nguvu nyingi na muda mwingi kufanikisha, ila mteja anakubana kwenye malipo yako mpaka inafika nusu bei!
Na hii nikutokana na ufundi na fundi kutokuwa na thamani kwenye jamii ni kazi inayochukuliwa ya kawaida mno ingawa inahitajika, hivyo fundi ili kufidia walao japo kidogo , kama cement zingekuwa kumi basi lazima akuambie 12.
Au hizo kumi atatumia 8 kwa kupunguza ubora ili aweze walao kufidi muda nguvu na akili zitakazotumika.

Pia sheria za ufundi hupaswi kufanya makadirio kamili ya vifaa vya kazi bali uzidishe, ila uzidishapo iwe ni kuzidi kwa kiasi na mwenye kazi anashirikishwa vifaa vikivyobaki baada ya kazi .
 
Nadhani uzi huu utatusaidia kung'amua janja janja wanazofanya mafundi, kwahiyo tutawamudu, juzi nimemuuliza fundi hii kazi itahitaji mifuko mingapi ya sementi, akanambia 25, nikamuuliza Bei ya sementi ipoje, akasema 16 Hadi 16 Mia 5. Nikaamua kwenda mwenyewe dukani bila kumwambia, nimekuta Bei Ni 14 na 15. Sijamwambia chochote, ntamletea sementi na nitamsimamia bampa to bampa, Kwanza ntampelekea mifuko 20 Kwanza. Ila Kuna mdau katoa wazo la kuulizia ratio kwa mafundi wengine ili kujua idadi halisi, nalo Ni Jambo la busara sana
 
Kuorodhesha idadi kubwa zaidi ya vinavyohitajika

Kuelekeza ununuzi wa material katika maduka wanayojua wao
Uko vizuri sana Mkuu

Hopefully upo kwenye field ya Ujenzi ama umejenga sana.

Mara ya mwisho nilimwajiri Fundi rangi MMama, she was good at decorating

Shida yake, alikuwa anaenda Dukani nilipolipia rangi, anamwambia Mzabuni boss kasema badala ya rangi Lita 20 nipe Lita 10....


Hiyo 10 inayobaki alikuwa anabeba anapeleka anapopajua mwenyewe 🙌
 
Back
Top Bottom