Mbeya: Mtoto wa darasa la nne shule ya msingi Mkapa alawitiwa na mwenzie wa darasa la saba

Mwanongwa

Senior Member
Feb 15, 2023
170
205
Mtoto mmoja wa kiume ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Mkapa iliyopo Jijini Mbeya amefanyiwa ukatili wa kulawitiwa na mwanafunzi mwenzie wa darasa la saba shule hapo aliyejulikana kwa jina moja la Arafat.

Mtoa habari hizi amefanikiwa kumuhoji maswali mwanafunzi huyo wakati akifanyiwa vipimo na daktari katika Kituo cha Afya Mwanjelwa maarufu kama Ruanda na amekiri kuwa huwa anaingiliwa.

Mwanafunzi huyo amesema kuwa kitendo hicho huwa anafanyiwa shuleni wakati wa mapumziko maeneo ya chooni na nyumbani maana mtuhumiwa wanaishi naye jirani huko Uyole jijini humo.

Mnyetishaji wa taarifa hizi ambaye ni kiongozi wa Serikali amesema kuwa familia ya mtoto huyo imechelewa kugundua kuwa kijana wao anafanyiwa unyama huo maana kijana anasema mchezo huo mchafu wameanza kuufanya muda mrefu.

Mwanongwa na nongwa zangu baada ya kutoka hospitali na kupata majibu kuwa ripoti ya daktari inadhibitisha kuwa mwanafunzi huyo kaingiliwa nikajibeba kwenda shuleni hapo ili kuonana na mwalimu mkuu.

Na katika safari ya kwenda shuleni tuliongozana na huyo kiongozi wa Serikali pamoja na bibi wa mwanafunzi huyo huku wakiwa na ripoti ya Daktari mkononi, basi nikawaacha watangulie wao kuingia kuonana na huyo mwalimu mkuu kisha baadae nikaingia mimi na kiongozi wa Sumaujata ambaye nilimkuta hapo akiwa anafuatilia tukio hilo.

Kituko kilichotokea kutoka kwa mwalimu mkuu huyo baada ya sisi kuingia na kujitambulisha huku tukiwa na uhakika kuwa taarifa za tukio hilo anazo na huku akiwa ameshika kopi za ripoti ya daktari mkononi alichotujibu ni kwamba hana taarifa yoyote na kibaya zaidi tulikuwa hatujamuuliza jambo lolote zaidi ya kujitambulisha tu, lakini akahamaki na kudai hana taarifa yoyote.

Swali ni je, kwanini Mwalimu Mkuu ameshindwa kutoa ushirikiano au naye ni miongoni mwa wanaofurahia vitendo hivyo?

Pia tulipata nafasi ya kupiga story na Walimu wa pale baada ya mkuu wa shule kutoka walimu walisema hali ni mbaya shuleni hapo na wanaomba kusaidiwa maana imefikia kipindi inabidi waanze kuwasindikiza watoto chooni.

Kwa wale ambao mna watoto shuleni hapo jaribuni kuwa makini na kuzungumza na watoto wenu.

Kwa leo niishie hapa, kesho nitakuja na muendelezo wa taarifa hii.
 
Ukifatilia vzr asilimia kubwa ya wanaolawitiwa au kuingia ktk ishu za ushoga wengi wao ni wanalelewa na Mama pekee au BIBI yaan BABA anakuwa hayupo ktk circle ya malez.

Mfn hapo tumeona BIBI ndio kaenda huko kufatilia kulawitiwa kwa Mjukuu wake. Wakat kwa hali ya kawaida hilo swala anatakiwa BABA asimame mbele.

Sas kama BABA hauna uangalizi mzuri wa mtt wako hasa wakiume lazima watampiga BORINGO tu.
 
Back
Top Bottom