Polisi Mbeya wawapa mahitaji Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lyoto

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,323
5,493
WhatsApp Image 2024-04-19 at 18.11.22_7385daa6.jpg

WhatsApp Image 2024-04-19 at 18.11.22_6e8b8966.jpg
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lyoto iliyopo Kata ya Ilemi Jijini Mbeya wamepatiwa mahitaji ya Shuleni na nyumbani kutoka kwa Polisi Kata ya Ilemi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Elibariki Mambuye.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mahitaji hayo Aprili 19, 2024 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Elibariki Mambuye amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao za maisha.

"Mimi kama Polisi Kata ya Ilemi, kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo nitajitahidi kutatua changamoto zenu ili asiwepo mwanafunzi atakayeshindwa kusoma kwa kigezo cha kukosa madaftari au penseli," alisema Mkaguzi Mambuye.
WhatsApp Image 2024-04-19 at 18.11.23_9580f53e.jpg
Aidha, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Mambuye amewataka wanafunzi hao kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia iwe ni kwa kufanyiana wenyewe kwa wenyewe au kufanyiwa na watu wengine ambapo amewataka kutosita kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.

Naye, Afisa Mtendaji Kata ya Ilemi Sikitu Msomba amepongeza juhudi za Polisi Kata ya Ilemi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Elibariki Mambuye kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwa lengo la kutokomeza uhalifu.

Sambamba na hilo, ametoa wito kwa wananchi na wadau wengine kuunga juhudi za Polisi Kata za kuwafikia na kuwasaidia wanafunzi na watu wengine wenye uhitaji waliopo katika Kata ya Ilemi kwani bado wapo wengi.

Naye, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lyoto ndugu PrayGod Albert amesema kuwa Shule yake ina zaidi ya wanafunzi 3,000 huku zaidi ya wanafunzi 300 wanatoka kwenye familia duni hivyo kuhitaji msaada wa vifaa vya Shule kama vile madaftari, penseli, pamoja na nguo kama vile sare za Shule, masweta kwa ajili ya kujistiri kutokana na baridi.

Vifaa vilivyotolewa na Polisi Kata ya Ilemi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Elibariki Mambuye ni pamoja na madaftari, penseli, masweta ya Shule na nguo za nyumbani kwa wanafunzi zaidi ya 150 wa kuanzia darasa la kwanza hadi la saba wa Shule ya Msingi Lyoto.
 
Back
Top Bottom