maoni, ushauri, mapendekezo, kuhusu elimu yetu

White party

JF-Expert Member
May 5, 2015
1,021
1,151
Salaam,
Naamini watanzania wengi tunapenda nchi yetu isonge mbele, na hili linaweza kubebwa vyema kama elimu yetu itakuwa kwa ajili ya kutukomboa

Hivyo basi tuungane katika kushauri serikali, wanafunzi na wote wanaohusika, nini kifanyike ili elimu yetu isaidie vizazi vyetu, mimi ntaanza na yafuatayo :-
1)serikali iachane na mfumo wa kupeleka watoto wote sekondari hata wasiojua kusoma eti tu kila mtu awe na elimu ya kidato cha nne, hii itafanikiwa kwa kurejesha Ile mitihani inayompima mwanafunzi na sio hii ya Sasa ya kushade

2)wanafunzi watakaofeli darasa la saba wapelekwe veta kwa watakaokuwa na umri wa kuanzia miaka15, na anaekua chini ya hapo aruhusiwe kurudia (wengine wanamaliza wadogo).
Hii itatusaidia kuwa na vijana watakaoweza kujiajiri kuliko kufika kidato cha nne na kuachwa bila muelekeo

NB:serikali inaweza tumia vijana hao kwa kututengenezea madawati, kujenga na kukarabati shule na ofisi zingne za serikali nk, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetengeneza vipaji na ajira hivyo elimu itatumika vyema kwa wale watakaofaulu na itatusaidia kupata wataalamu wenye vigezo pamoja na wasimamizi wazuri (officers)

Asanteni na karibu kwa michango zaidi

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom