Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,351
- 11,223
Takwimu za vifo Gaza ni kubwa mno kiasi kwamba inakadiriwa kati ya kila wapalestina 20 mmoja kati yao ameuliwa.
Suala la vifo zaidi ya 100 na baadhi ya siku mpaka 700 ni kitu cha kawaida.Kuna wajumbe wa UN wanasema hawajawahi kushuhudia uwiyano wa vifo namna hiyo katika vita vyovyote duniani.
Katikati ya hali hiyo ya kutisha wajumbe wa mashirika ya misaada katikati ya wiki hii walipokuwa wakijaribu kupeleka misaada kaskazini ya Gaza walishangaa kuzuiliwa na majeshi ya Israel kufikia maeneo hayo wakielezwa kuwa kuna magaidi ya Hamas.
Hata hivyo walichokiona njiani ni maiti za watu wakiwemo watoto wadogo.Wale waliowakuta hai njiani walikuwa ni watu waliodhoofika sana kwa njaa wakikimbilia magari yao ambayo hayakuwa na kitu wakiomba maji na chakula. Waliposhindwa kuwasaidia walishuduia baadhi yao wakidondoka na kufa.
Hayo ni matokeo ya kushindwa kwa Israel katika vita na kubaki kuua watu kwa silaha za moto na kwa ktumia njaa na kiu. Na hali hiyo ndiyo iliyoitia huruma nchi ya Afrika kusini na kuamua kuifungulia kesi Israel kwenye mahakama ya ICJ