Mabingwa wa kutunga nyuzi za uongo uongo

Wakuu habari?

Natumaini wote mko wazima huku mkijiandaa kusherehekea ufufuko wa bwana.

Humu ndani kuna mabingwa wa kutunga nyuzi za uongo uongo; ukisoma mstari wa kwanza mpaka wa mwisho, unakuta hakuna uhalisia wowote.

Ebu tuwataje hawa mabingwa, ikiwezekana wapate pepsi kwa gharama ya mifuko yao.

Nipo pale, napata gahawa.

Twende kazi :CarltonPls:
Hivi kuna mtu anakuzidi wewe kwa chai humu.?? 😂😂😂
Nikisoma uzi nikiona ni ww naendelea na mambo mengine najua fix tyuuu hapa..!!!
 
Na da mau jamani ana fix sijapata kuona!! 🤣🤣🤣

Saa 1 anakuja na uzi wa kurogwa, saa 3 amerudi na uzi wa kutapeliwa kazi, saa 5 anarejea na uzi wanawake hawampendi wanahisi atawaibia mabwana zao wa JF ( wa afu tatu) 🤣🤣🤣🤣

Saa 7 akila nguna kashiba anakuja na dedication song la mahaba ( kashafall in love) 🤣🤣🤣🤣

Jioni anarudi na umri umeenda kuna mtu kamroga na kamtia mikosi..!! Yani ni fix kwa kwenda mbele
 
Back
Top Bottom