Leo ukipewa nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira utafanya nini kuongeza Ajira nchini?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,481
8,334
Mara nyingi tumekuwa tukishauri viongozi vitu vya kufaya ili kusaidia maboresho katika Wizara na Serikali kwa ujumla. Sasa leo ukipewa wewe nafasi ya kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, utafanya nini cha tofauti ili kusaidia kuongeza Ajira katika nchi yako?
 
Tukubaliane kwanza sekta ya kilimo ndiomuajili mama.

Kwanza wizara ya kilimo inatakiwa iunganishwe na wizara ya kazi na Vijana. kisha kuwe na muunganiko na biashara.

Fungua mashamba ya mboga mboga na matunda wape vijana wayahudumie sio kama anavyofanya Bashe, Mara kupeleka vijana jeshini mara shamba la pamoja we uliona wapi.

Vijana wazalishe wizara utafute soko.

Sisi mko wapi, Fungua Kiwanda cha kusindika nyanya ziwe za unga, unga wa matunda mchanganyiko kupata juice in a low season.

Leo kijana anaenda kulima nyanya wanakutana sokoni kama wote,Nyanya wanalisha mifungo.

Fuga mbuzi peleka dubai nyama,
 
mpaka sasa, wizara na waziri mwenye dhamana wanafanya kazi nzuri, kwa bidii, maarifa na weledi wa hali ya juu sana na kwakweli wamefanikiwa pakubwa ukilinganisha na vipindi vilivyo pita 🐒

Hata hivyo pamoja na mipango mikakati mizuri sana iliyopo wizarani,
bado viwanda, biashara, kilimo na ufugaji inapaswa kua uelekeo mahususi kwa sasa na wenye msisitizo na jitihada za makusudi ili kuvutia wasaka ajira wengi zaidi, na kutibu mpka kupona bisa changamoto ya ajira nchini 🐒
 
Tanzania yetu hii hatuhitaji hata wizara ya kazi. Inahitajika kila wizara ikiwemo kilimo ufugaji uvuvi, sayansi na teknolojia, wizara ya fedha zifanye kazi kwa uzalendo, kusimamia haki, sera nzuri za uchumi basi ajira zitafunguka

Tozo zisizo na kichwa wala miguu TRA ziondolewe vijana tujiajiri. Wazazi wetu wastaafu wapewe mafao yao yote ili watupe watoto wao mitaji tujiajiri.

Ikifunguliwa wizara ya kazi halafu wizara zingine ziendelee kufanya uozo tutakua tunatwanga maji kwenye kinu.
 
1. Nitapunguza masaa ya kazi kutoka masaa 11 hadi masaa sita yaani kuanzia muda wowote unaoingia kazini iwe saa moja jioni, saa saba mchana, saa kumi na mbili asubuhi, then hesabia kuanzia muda huo then mbele yako ni masaa sita unakuwa umemaliza muda wa kazi na utapisha mtu mwingine aingie shifti yako.

Hii itapunguza kwanza masaa ya kazi na kuwapa wafanyakazi nafasi ya kushiriki shughuli zingine za kijamii kama malezi ya familia, ndoa na biashara.

Lakini pia itapunguza ubwanyenye na umangi meza ambapo mtu anaweza hodhi ofisi na mamlaka na kuyatumia vibaya akijua ofisi yupo pekee yake na hatimae kuleta urasimu na ukiritimba kwenye ofisi za serikali na kuharibu ufanisi.

2. Nitafuta malipo ya mshahara kwa mwezi na kupendekeza taaisisi moja baada ya nyingine kuingizwa katika malipo ya masaa. Yaani masaa sita utalipwa kwa kila lisaa chini ya uangalizi na ukaguzi wa kufa mtu. Hii itapunguza mzigo wa serikali kulipa wafanyakazi hewa, na kulipa watu wasiofanya kazi. Mtu anaingia ofisini na kutoka masaa manne hayupo eneo la kazi ila mwisho wa siku analipwa, kwann analipwa?

3. Watu wataweza kuajiriwa na kuwa na mikataba zaidi ya mitatu. Yaani mfano mtu anaajiriwa CRDB, NMB na Exim, na kote huko anafanya kazi kwa masaa kulingana na uwezo wake. Au anaweza fanya kazi NMB, shirika la posta, na Hotelini kama Serena. Na kazi zote analipwa kwa masaa yake ya utendaji.

4. Nitabadilisha mfumo wa malipo badala ya mwezi waajiriwa watalipwa stahiki zao kwa wiki ili kupunguza msongamano wa malipo mwisho wa mwezi na pia kuwaondolea kadhia raia ya kupata malipo baada ya siku 30.

5. Nitashawishi mitaala ya vyuo vikuu kubadili masomo yasiwe notisi nyingi na mitihani mingi bali yawe ni lecture wastani, presentation za group na individual za kuongea ziongezwe, na seminars sessions,ziwe za kutosha ili kuwapa wanavyuo uwezo wa kitaaluma wa kuchanganua mambo, lakini pia nitashawishi serikali wanavyuo kutumia semester ya kwanza ya kila mwaka wa masomo kufanya field practice kwenye taaisisi mbali mbali popote walipo. Sio tu hadi kusubiri mwaka wa tatu.

Performance zao zikuwa nzuri zitawaruhusu kupata post za internships za kujitolea kwenye makampuni lengwa kulingana na taaluma zao, ili kuwasaidia kupata ujuzi na uzoefu wa kitaasisi na kuweza kutambua uhalisia na changamoto halisi na sio story za vijiweni au hadithi za matutorial na lecturers.

Pia vijana hawa nitashawishi serikali kutenga fungu maalumu waweze kupata vitu basic kama vifurishi vya simu kwaajiri ya mawasiliano, pesa ya chakula na nauli, na posho ya kujikimu kimaisha ili kuweza kuwasaidia kujihudumia kipindi wakiwa wanasubiria kupata mikataba kamili yenye stahiki zote. Watalipwa pia kwa masaa ila kwa 60% ya kiwango anacholipwa mfanyakazi wa kawaida kama basic salary.

6. Nitahakikisha kila taaisisi ya serikali ndani ya departments zake inakuwa na kitengo cha internships na kunakuwa na maofisa wake ambao wata act kama supervisors wa kurepoti kwenye taasisi yenyewe, vyuo, na wizarani kutoa ripoti za kimwenendo za hawa wahusika wataopewa nafasi aidha za trainings au internships.

Nitaongeza points nyingine baadae.
 
Tukubaliane kwanza sekta ya kilimo ndiomuajili mama.

Kwanza wizara ya kilimo inatakiwa iunganishwe na wizara ya kazi na Vijana. kisha kuwe na muunganiko na biashara.

Fungua mashamba ya mboga mboga na matunda wape vijana wayahudumie sio kama anavyofanya Bashe, Mara kupeleka vijana jeshini mara shamba la pamoja we uliona wapi.

Vijana wazalishe wizara utafute soko.

Sisi mko wapi, Fungua Kiwanda cha kusindika nyanya ziwe za unga, unga wa matunda mchanganyiko kupata juice in a low season.

Leo kijana anaenda kulima nyanya wanakutana sokoni kama wote,Nyanya wanalisha mifungo.

Fuga mbuzi peleka dubai nyama,
Wizara wala haina haja ya kutafuta soko, masoko yapo na madalali tunao shida ni sera za serikali katika kuachia biashara na wakulima kukua.

1. Bei za pembejeo kupanda bila utaratibu na serikali ikibakia bubu.

2. Sera za bei za mazao nani anakuwa refa pale mkulima au hawa middle men wanapoonewa. Kuna muda wakulima wanakuwa hawapo fair na kuna muda Middleman hawapo fair.

3. Kufunga funga mipaka bila utaratibu na kuwadhibiti wauzaji wa nje kwa kodi za kipumbavu na zisizo na vichwa wala miguu.
 
Ni kucoordinate na wizara ya kilimo kujenga irrigation schemes. Mito, maziwa na mvua tunavyo kibao. Ukijenga irrigation scheme ya ekari 100,000. Vijana wakawa wanakodi kuanzia ekari 1-5 utatoa ajira kwa vijana maximum 100,000. Na hii nchi ina ekari milioni 29 za kufaa kwa kilimo.

Hakuna namna nzuri ya kutengeneza ajira kwa vijana kama hii.
 
Wizara wala haina haja ya kutafuta soko, masoko yapo na madalali tunao shida ni sera za serikali katika kuachia biashara na wakulima kukua.

1. Bei za pembejeo kupanda bila utaratibu na serikali ikibakia bubu.

2. Sera za bei za mazao nani anakuwa refa pale mkulima au hawa middle men wanapoonewa. Kuna muda wakulima wanakuwa hawapo fair na kuna muda Middleman hawapo fair.

3. Kufunga funga mipaka bila utaratibu na kuwadhibiti wauzaji wa nje kwa kodi za kipumbavu na zisizo na vichwa wala miguu.
Nasema Haya kutafuta Soko sababu KFC bado anaagiza kukunje,Frozen chips nje carot nje,na mboga mboga kibao.WIZARA YA KILIMO NDIO INATOA kibali.Huyu ni mmoja tu wa mfano Bado subway Chiken king na wengine.
 
Tatizo mleta mada ndio tatizo la viongozi wengi walioko Madarakani huwaza ajira za ndani ya nchi ti wanasahau kuwa kama ilivyo Kwa bidhaa Kuna za Soko la ndani na Soko la nnje

Na ajira ziko za ndani na nje ya nchi

Hilo kufanikiwa kunatakiwa upatikanaji wa Passport kwanza iwe rahisi kama nchi za wenzetu vijana wakasake fursa za ajira nje Huwezi Pata kazi mfano za vibarua nje ya nchi ukiwa Tanzania inatakiwa kwenda huko ukaombe huko huko

Hakuna mtu atakuletea hizo kazi za kibarua nk nchini kwako

Wakenya wako Hadi wafagia barabara marekani Lakini walipata hizo kazi baada ya kufika kule

Ubaniaji kutoa passport ni moja ya chanzo Cha tatizo kubwa la Ajira.Sababu wizara yenyewe ya kazi inamka na kuwaza ajira za ndani ya nchi tu wakati Soko la ajira la ndani limeshafurika
 
Nasema Haya kutafuta Soko sababu KFC bado anaagiza kukunje,Frozen chips nje carot nje,na mboga mboga kibao.WIZARA YA KILIMO NDIO INATOA kibali.Huyu ni mmoja tu wa mfano Bado subway Chiken king na wengine.
Sababu kuu hatuna kilimo kikubwa Cha kisasa na ufugaji wa kisasa mkubwa wa kuku Cha kuzalisha quality kubwa nankwa standard za kimataifa

Hao wanajali quality unachokula Tanzania kinakuwa standard Ile Ile na anayekula hoteli zao ulaya au marekani
 
Ntaanza na Michezo na sanaaa, Hapa ntajenga miundombinu ya kila aina kwenye michezo kama viwanja na Vyuo kwa ajili ya kupata wataalam ambao tutawatumia ndani na wengingine watasambaa dunia nzima, Ntakuja kwenye kilimo hapa ntahakikisha Tanzania tunaacha kabisaa kutegemea mvua. Ukocheki kwenye Raman ya Dunia utagundua ni Tanzania pekee ndio imezungukwa na Maziwa Makuu, kwa kutumia rasilimal ya maj tulionayo basi ntahakikisha kuna Kilimo kikubwa cha umwagiliaji ambapo vijana maelfu watafanya kazi huko. Magereza yote yatakuwa vyuo vya ufundi stad.

Nina mengi sana ya kufanya.. Kikubwa kuliko yote sitavumilia uzembe hata kidogo
 
Nitapunguza muda wa kustaafu uwe mwisho 50yrs.
Kwa hiyari 45 yrs.
Faida zake ni kuwa;
1.Itatoa fursa ya ajira kwa vijana.
2.Itawapa fursa wastaafu kutengeneza ajira zao,na kwa ajili ya wengine,kwani watastaafu wakiwa na nguvu&mtaji wa kutosha.
 
1. Nitapunguza masaa ya kazi kutoka masaa 11 hadi masaa sita yaani kuanzia muda wowote unaoingia kazini iwe saa moja jioni, saa saba mchana, saa kumi na mbili asubuhi, then hesabia kuanzia muda huo then mbele yako ni masaa sita unakuwa umemaliza muda wa kazi na utapisha mtu mwingine aingie shifti yako.

Hii itapunguza kwanza masaa ya kazi na kuwapa wafanyakazi nafasi ya kushiriki shughuli zingine za kijamii kama malezi ya familia, ndoa na biashara.

Lakini pia itapunguza ubwanyenye na umangi meza ambapo mtu anaweza hodhi ofisi na mamlaka na kuyatumia vibaya akijua ofisi yupo pekee yake na hatimae kuleta urasimu na ukiritimba kwenye ofisi za serikali na kuharibu ufanisi.

2. Nitafuta malipo ya mshahara kwa mwezi na kupendekeza taaisisi moja baada ya nyingine kuingizwa katika malipo ya masaa. Yaani masaa sita utalipwa kwa kila lisaa chini ya uangalizi na ukaguzi wa kufa mtu. Hii itapunguza mzigo wa serikali kulipa wafanyakazi hewa, na kulipa watu wasiofanya kazi. Mtu anaingia ofisini na kutoka masaa manne hayupo eneo la kazi ila mwisho wa siku analipwa, kwann analipwa?

3. Watu wataweza kuajiriwa na kuwa na mikataba zaidi ya mitatu. Yaani mfano mtu anaajiriwa CRDB, NMB na Exim, na kote huko anafanya kazi kwa masaa kulingana na uwezo wake. Au anaweza fanya kazi NMB, shirika la posta, na Hotelini kama Serena. Na kazi zote analipwa kwa masaa yake ya utendaji.

4. Nitabadilisha mfumo wa malipo badala ya mwezi waajiriwa watalipwa stahiki zao kwa wiki ili kupunguza msongamano wa malipo mwisho wa mwezi na pia kuwaondolea kadhia raia ya kupata malipo baada ya siku 30.

5. Nitashawishi mitaala ya vyuo vikuu kubadili masomo yasiwe notisi nyingi na mitihani mingi bali yawe ni lecture wastani, presentation za group na individual za kuongea ziongezwe, na seminars sessions,ziwe za kutosha ili kuwapa wanavyuo uwezo wa kitaaluma wa kuchanganua mambo, lakini pia nitashawishi serikali wanavyuo kutumia semester ya kwanza ya kila mwaka wa masomo kufanya field practice kwenye taaisisi mbali mbali popote walipo. Sio tu hadi kusubiri mwaka wa tatu.

Performance zao zikuwa nzuri zitawaruhusu kupata post za internships za kujitolea kwenye makampuni lengwa kulingana na taaluma zao, ili kuwasaidia kupata ujuzi na uzoefu wa kitaasisi na kuweza kutambua uhalisia na changamoto halisi na sio story za vijiweni au hadithi za matutorial na lecturers.

Pia vijana hawa nitashawishi serikali kutenga fungu maalumu waweze kupata vitu basic kama vifurishi vya simu kwaajiri ya mawasiliano, pesa ya chakula na nauli, na posho ya kujikimu kimaisha ili kuweza kuwasaidia kujihudumia kipindi wakiwa wanasubiria kupata mikataba kamili yenye stahiki zote. Watalipwa pia kwa masaa ila kwa 60% ya kiwango anacholipwa mfanyakazi wa kawaida kama basic salary.

6. Nitahakikisha kila taaisisi ya serikali ndani ya departments zake inakuwa na kitengo cha internships na kunakuwa na maofisa wake ambao wata act kama supervisors wa kurepoti kwenye taasisi yenyewe, vyuo, na wizarani kutoa ripoti za kimwenendo za hawa wahusika wataopewa nafasi aidha za trainings au internships.

Nitaongeza points nyingine baadae.
Andiko lako ni zuri miongoni mwa wachangiaji wengine.
Hata hivyo kutokana na mchango wako huu ili uweze kufikia lengo lako unatakiwa uwe rais wa nchi mwenye maamuzi kwenye eneo kubwa.

Pamoja na hivyo ikiwa una uwezo wa kumshawishi rais na baraza lake la mawaziri kwa hoja, unaweza kufikia lengo lako kwa mipango ya muda wa kati na muda mrefu.
 
Wiki iliopita niliona kwenye CNN habari yenye caption 'US ECONONY GENERATES 170,000 JOBS IN APRIL' Umeona nini hapo? In short the ECONONY CREATES JOBS' not Waziri wa kazi. Hii inabidi ifanywe na wizara ya fedha,wizara ya kilimo,wizara ya viwanda na biashara. Wizara ya ajira itasimamia Sera na haki za wafanyakazi etc
The Economy Creates JOBS.
 
Jambo la kwanza ntasitisha vibali vya Wahindi na Wachina wote wanaofanya kazi ambazo Mtanzania anaweza kufanya, no matter what na sheria kali dhidi ya yeyote anayevunja.

Baada ya hapo ndio ntaanza kufikiria kuongeza ajira kupitia viwanda na biashara na kilimo. Atakayetaka mkopo wa biashara atapewa in instalmenta badala ya mkopo wa kusoma chuo kikuu.
Leseni zote za biashara ni bure kwa mtu mwenye umri miaka 18 mpaka 35. Kodi (income tax) itawekwa 1/4 ya kiasi kinacholipwa sasa kwa vijana wa umri huo.

Fao la kujitoa ruhusa, cha msingi usiwe na umri chini ya miaka 45 na utapewa 90% ya peza zako zote.

Mikopo katika mabanks kwa subsidies.
Ngoja ntarudi.
 
Mosi, nitashusha umri wa hiyari wa kustaafu hadi kufikia miaka 50. Wastaafu watarajiwa wote watapata mafunzo maalum ya kuendesha viwanda vidogo vya kuchakata mazao ya kilimo mfano: kupack nyama/matunda, usindikaji wa mbogamnoga na mazao ya nafaka, kuongeza thamani kwenye bidhaa ghafi hususani za masokoni kama maharage n.k.
Mstaafu mmoja akipata mafunzo vyema ana uwezo wa kuendesha processing industry yake mwenyewe na kutoa ajirq za moja kwa moja kwa vijana wasiopungua 5 na wengine zaidi ya 10 ktk mnyororo wa malighafi.
Kuna mambo mengi sana nitakayofanya, ila kwasasa niombe mnipe hiyo nafasi kwa walau mwaka mmoja kisha muone hali itakavobadilika kwa ghafla.
 
1. Nitapunguza masaa ya kazi kutoka masaa 11 hadi masaa sita yaani kuanzia muda wowote unaoingia kazini iwe saa moja jioni, saa saba mchana, saa kumi na mbili asubuhi, then hesabia kuanzia muda huo then mbele yako ni masaa sita unakuwa umemaliza muda wa kazi na utapisha mtu mwingine aingie shifti yako.

Hii itapunguza kwanza masaa ya kazi na kuwapa wafanyakazi nafasi ya kushiriki shughuli zingine za kijamii kama malezi ya familia, ndoa na biashara.

Lakini pia itapunguza ubwanyenye na umangi meza ambapo mtu anaweza hodhi ofisi na mamlaka na kuyatumia vibaya akijua ofisi yupo pekee yake na hatimae kuleta urasimu na ukiritimba kwenye ofisi za serikali na kuharibu ufanisi.

2. Nitafuta malipo ya mshahara kwa mwezi na kupendekeza taaisisi moja baada ya nyingine kuingizwa katika malipo ya masaa. Yaani masaa sita utalipwa kwa kila lisaa chini ya uangalizi na ukaguzi wa kufa mtu. Hii itapunguza mzigo wa serikali kulipa wafanyakazi hewa, na kulipa watu wasiofanya kazi. Mtu anaingia ofisini na kutoka masaa manne hayupo eneo la kazi ila mwisho wa siku analipwa, kwann analipwa?

3. Watu wataweza kuajiriwa na kuwa na mikataba zaidi ya mitatu. Yaani mfano mtu anaajiriwa CRDB, NMB na Exim, na kote huko anafanya kazi kwa masaa kulingana na uwezo wake. Au anaweza fanya kazi NMB, shirika la posta, na Hotelini kama Serena. Na kazi zote analipwa kwa masaa yake ya utendaji.

4. Nitabadilisha mfumo wa malipo badala ya mwezi waajiriwa watalipwa stahiki zao kwa wiki ili kupunguza msongamano wa malipo mwisho wa mwezi na pia kuwaondolea kadhia raia ya kupata malipo baada ya siku 30.

5. Nitashawishi mitaala ya vyuo vikuu kubadili masomo yasiwe notisi nyingi na mitihani mingi bali yawe ni lecture wastani, presentation za group na individual za kuongea ziongezwe, na seminars sessions,ziwe za kutosha ili kuwapa wanavyuo uwezo wa kitaaluma wa kuchanganua mambo, lakini pia nitashawishi serikali wanavyuo kutumia semester ya kwanza ya kila mwaka wa masomo kufanya field practice kwenye taaisisi mbali mbali popote walipo. Sio tu hadi kusubiri mwaka wa tatu.

Performance zao zikuwa nzuri zitawaruhusu kupata post za internships za kujitolea kwenye makampuni lengwa kulingana na taaluma zao, ili kuwasaidia kupata ujuzi na uzoefu wa kitaasisi na kuweza kutambua uhalisia na changamoto halisi na sio story za vijiweni au hadithi za matutorial na lecturers.

Pia vijana hawa nitashawishi serikali kutenga fungu maalumu waweze kupata vitu basic kama vifurishi vya simu kwaajiri ya mawasiliano, pesa ya chakula na nauli, na posho ya kujikimu kimaisha ili kuweza kuwasaidia kujihudumia kipindi wakiwa wanasubiria kupata mikataba kamili yenye stahiki zote. Watalipwa pia kwa masaa ila kwa 60% ya kiwango anacholipwa mfanyakazi wa kawaida kama basic salary.

6. Nitahakikisha kila taaisisi ya serikali ndani ya departments zake inakuwa na kitengo cha internships na kunakuwa na maofisa wake ambao wata act kama supervisors wa kurepoti kwenye taasisi yenyewe, vyuo, na wizarani kutoa ripoti za kimwenendo za hawa wahusika wataopewa nafasi aidha za trainings au internships.

Nitaongeza points nyingine baadae.
Ukigombea Urais nakupa kura yangu!
 
Wizara wala haina haja ya kutafuta soko, masoko yapo na madalali tunao shida ni sera za serikali katika kuachia biashara na wakulima kukua.

1. Bei za pembejeo kupanda bila utaratibu na serikali ikibakia bubu.

2. Sera za bei za mazao nani anakuwa refa pale mkulima au hawa middle men wanapoonewa. Kuna muda wakulima wanakuwa hawapo fair na kuna muda Middleman hawapo fair.

3. Kufunga funga mipaka bila utaratibu na kuwadhibiti wauzaji wa nje kwa kodi za kipumbavu na zisizo na vichwa wala miguu.
Andiko lako ni zuri miongoni mwa wachangiaji wengine.
Hata hivyo kutokana na mchango wako huu ili uweze kufikia lengo lako unatakiwa uwe rais wa nchi mwenye maamuzi kwenye eneo kubwa.

Pamoja na hivyo ikiwa una uwezo wa kumshawishi rais na baraza lake la mawaziri kwa hoja, unaweza kufikia lengo lako kwa mipango ya muda wa kati na muda mrefu.

Serikali yetu ina Vizuizi vingi kiasi kwamba kuna viongozi wapo juu lakini bado wanashindwa kufanya maamuzi ya kimapinduzi katika swala zima la vijana na ajira.
 
Back
Top Bottom