Leo kama najiona nalala na njaa kali

southernboy

JF-Expert Member
Sep 27, 2015
836
1,029
Habari zenu wakuu, kijana wenu katika kuhangaika hii wiki nikapata kahela kidogo, sasa leo nilikuwa nimebakiwa na sh. 12,000/= kwenye mfuko wangu wa suruali
..nikiwa ninaenda kanisani asubuhi kwenye daladala akaingia kipofu ambaye anaombaomba mule ndani nikaona sio mbaya nikachukua mia5 moja nikampa nikafanya hivo,,

sasa wakati nashuka gari nikatoa miatano nyingine nimempa konda nikamuomba mia sina ,nikaacha noti mfukoni nikaichomoa ile mia 5 nikakampa huku najua zile mfukoni ni noti mbili yaani elfu moja na elfu kumi,,, sasa nimetembea mbele kidogo nataka niweke vizuri hela ya sadaka nakuta nimeishika noti moja tuu ya elfu moja ,kujisachi sioni kitu nikaanza kuchanganyikiwa hela yenyewe ndio ilibaki hiyo kesho niingie mahangaikoni tena sasa nimebaki mtupu, na ile daladala imeshajichanganya nikaanza jilaumu kwanini sikusoma ile plate number,
nikataka niahirishe na kusali kwenyewe ila nikasali na ile elfu moja nikaitumia kama nauli ya kurudia.
 
Hapa ndipo unapoona kanisa halina msaada ukiwa na shida. Tunaenda kanisani ili kujifunza upendo wa Mungu nasi tupendane vivyo hivyo. Lakini ukaona uanzie JF badala ya kanisani
 
Back
Top Bottom