mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,041
Kimsingi Law School of Tanzania inapaswa kushughulika na kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi kwa vitendo ndiyo maana inaitwa LEGAL PRACTICAL TRAINING! Inalenga kuwapatia wanafunzi weledi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa vitendo zaidi. Hawajaenda pale kushindiliwa tena elimu ya sheria kwa nadharia maana hiyo waliipata vyuoni. Kama kuna vipengele vya kinadharia vimepungua, basi waviingize kwenye mitaala huko vyuoni.
Kinyume na lengo hilo la msingi, law school inalazimisha kutumia semister nzima ya kwanza kufundisha tena kwa nadharia yale ambayo tayari wanafunzi waliyasoma vyuoni. Mwisho wa siku wanafunzi hufanyishwa tena mitihani kwa nadharia zaidi. Haya matokeo yanayovuma ni ya nadharia.
PENDEKEZO: Semister zote mbili zitumike kuwapeleka wanafunzi field maeneo mbali mbali na wapimwe huko huko field kwa vitendo kuonekana wamefaulu au la!! Kusiwepo tena mitihani ya nadharia, ambayo tayari walishaifuzu vyuoni.
WANACHOFANYA: Ni kutengeneza pesa isivyo halali na kutengeneza mazingira ya rushwa zaidi!! Hapo law school kuna rushwa sana!
PIA WENGINE WAMESHAIGA: Bodi ya wafamasia na yenyewe ina mwelekeo huo huo. Baada ya Internship ambayo kimsingi ni mafunzo kwa vitendo, badala ya kuwapima wanafunzi kwa vitendo huko huko field, huwataka kufanya mtihani tena wa NADHARIA ili kuwasajili!! Ebo!! Lengo ni pesa na kulazimisha mazingira ya rushwa!! Kufanya mtihani ni pesa, na kurudia mtihani ni pesa!