Mwanahabari wa Taifa
JF-Expert Member
- May 27, 2020
- 1,452
- 805
RC Kafulila apiga marufuku ‘michomoko’ kusafirisha abiria Mkoa wa Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (RC) nchini Tanzania, David Kafulila amepiga marufuku magari madogo maarufu michomoko kusafirisha abiria mkoani humo.
Ni baada ya kuhusika kwenye matukio ya ajali yaliyosababisha vifo vya watu 10 na majeruhi 17 ndani ya siku 12 zilizopita.
Amri ya Kafulila imetolewa leo Jumatano Julai 13, 2022 ikiwa ni siku moja baada ya ajali iliyotokea eneo la Magereza nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu usiku wa kuamkia jana ikihusisha "michomoko" na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi 11.
Wakati majina ya marehemu watano waliofariki kwenye ajali ya Simiyu bado hayajawekwa wazi na waliojeruhiwa ni Elizabeth Nestory (26), Yohana Mwita (22), Sumai Mabula (43), Joseph Masanja (32) na Neema Samson (20).
Wengine ni, Felister Maganda (54), Happy Manyama (23), Oscar Nsolo (47), Stephano Stephene (22) na Joyce Manyama (27) huku majeruhi mmoja ambaye yuko kwenye hali mbaya hajafahamika.
soma pia hii
Ajali hiyo litokea baada ya magari madogo mawili madogo aina ya Toyota pro box na Toyota wish yanayosafirisha abiria kati ya miji wa Bariadi Wilaya ya Bariadi na Lamadi wilayani Busega kugongana uso kwa uso.Tukio hilo limetokea siku 12 pekee baada ya ajali nyingine iliyohusisha “mchomoko” aina Toyota wish iliyotokea eneo la Luguru Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi watano.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bariadi yaliko makao makuu ya Mkoa wa Simiyu, Kafulila amesema magari hayo madogo yanafanya shughuli ya kusafirisha abiria kinyume cha sheria na maelekezo ya Serikali kupitia Mamlaka ya Usafirishaji wa ardhini (Latra).
"Wamiliki na waendeshaji wa nigari haya ya michomoko wamepewa maelekezo ya kufuata ili kuwaruhusu waendelee kufanya kazi ya kusafirisha abiria, lakini ni zaidi ya miezi sita sasa hawajatekeleza,” amesema Kafulila
Mkuu huyo wa mkoa amesema kutokatana na ukaidi wa wamiliki hao huku watu wakiendelea kupoteza maisha na kujeruhiwa katika ajali zinazohusisha magari hayo, Serikali inasitisha shughuli za magari hayo ya kusafirisha abiria kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Usafirishaji inayoipa mamlaka ya kufanya hivyo.
Ametumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji katika sekta ya usafirishaji wa abiria kwenda mkoani Simiyu kuwekeza katika usafirishaji salama kwa mujibu wa sheria.
Naye ofisa mfawidhi wa Latra mkoa wa Simiyu, Amaniel Sekulu amesema kwa mujibu wa leseni, magari madogo yanayofahamika kwa jina maarufu ya ‘mchomoko’ yanayosafirisha abiria katika miji mbalimbali mkoani humo yamesajiliwa kama Taxi, akini badala yake, wamiliki wamebadilisha shughuli kwa kusafirisha abiria kinyume cha sheria.
“Magari haya yanatakiwa kusajiliwa, kupakwa rangi, kuandikwa namba za utambulisho ubavuni na kubandika vibao maalum vinavyoonyesha kuwa ni Taxi na zinatakiwa kupakia abiria kwa idadi inayoruhusiwa kisheria,” amesema Sekulu
======================
WAKATI HUOHUO LATRA YAPIGILIA MSUMALI AGIZO LA KAFULILA, MICHOMOKO YOTE KUONDOLEWA BARABARANI NCHI NZIMA!
Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini( LATRA) limetoa tamko kali kuunga mkono maamuzi magumu aliyochukua Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Kafulila ya kupiga marufuku gari ndogo zinazotumika kusafirisha abiria maarufu kama michomomoko kuanzia Julai13, 2022.
Kafulila alipiga marufuku gari hizo kuendelea kutumika kutokana na kuwa sababu kuu ya ajali mkoani Simiyu kufuatia gari hizo kutimika kubeba abiria wengi na kukaidi agizo lake la muds mrefu kutaka zitumike kama taxi badala ya kujigeuza daladala kwa kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo. " Kwakua kutokana na mwenendo usioridhisha gari hizi zimekuwa chanzo kikubwa cha ajali, na kwakuwa gari hizi zimekaidi maelekezo ya serikali kutaka zifuate taratibu za kujiendesha kama taxi kwa kisingizio kuwa mfumo huo haulipi kibiashara, basi kuanzia leo Julai13, 2022, nasitisha usafiri wa MICHOMOKO mpaka hapo itakapoamuliwa vinginevyo" alisisitiza RC Kafulila.
Katika tamko Lao, LATRA wamesisitiza mikoa wakuu wa mikoa mingine kufuata mfano huo kukabili tatizo la ajali nchini kwani gari hizo sio salama , nihatari kwa usalama wa wananchi kwani zimekuwa chanzo cha ajali maeneo mengi nchini na kuahidi kushirikiana na vyombo vingine ikiwemo jeshi la polisi kuhakikisha inafanyika opareshen nchi nzima
RC Kafulila anatumia kifungu cha 25 cha kwenye sheria ya Land Transport Reguratory Act
Nae kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani ACP Wilbroad Mtafungwa amekandamizia kuwa sasa Tanzania michomoko basi kwa usalama wa Watanzania na mali zao, msikilize mpaka mwisho huyu Mwamba,