Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

mutu murefu

JF-Expert Member
Jan 3, 2017
938
2,329
Habari za asubuhi wakuu.

Kwa muda kidogo nimekua nikifanya utafiti mdogo wa madalali wauzaji wa magari instagram na social media nyingine.

Kuna kitu nimegundua nikaona nijadiliane nipate majibu sahihi.

Nimeona madalali wa mwanza wanauza gari kwa bei rahisi sana ukilinganisha na wa Dar es Salaam (kwa gari zenye specificationa sawa)

Mfano
Toyota crown
Mwanza nakuta nyingi average milion 8 (zinaanza 7m mpaka 10m hivi) ila dar es salaam average milion 11 (zinaanzia 10m mpaka 13m).

Toyota mark x
Mwanza around 5.5m mpaka 7m, ila Dar es salaam around 8m mpaka 11m

Toyota kluger
Mwanza 9m mpaka 14m.. ila Dar es salaam 14 mpaka 18

Toyota harrier tako la nyani
Mwanza 14m mpaka 18m
Dar 16 - 22m

Sasa ndugu zangu naomba kujua sababu ya utofauti huu mkubwa wa bei! Je madalali wa Dar ni kwamba wanapiga cha juu kingi au watu wa mwanza wana pesa sana ndio sababu wanauza bei ndogo?

Maana nimeshawishika kidogo kununua harrier kwa hawa jamaa wa Mwanza maana bei zao kitonga sana.

Nawasilisha
8E5F74CD-C9BA-4ABB-AE0B-27631EB73C0E.png
14521864-B72A-4446-932C-C6C41D21716A.png
0F11CAC9-202A-46DB-B942-6961F191F6EA.png
FB2741B3-CFC6-4AE9-A5BE-77A1C9ED720B.png
13CFB436-3A37-47A1-9F48-39D5A0D1E16F.png
0F11CAC9-202A-46DB-B942-6961F191F6EA.png
0F11CAC9-202A-46DB-B942-6961F191F6EA.png
14521864-B72A-4446-932C-C6C41D21716A.png
 
Magari ya Mwanza mengi yamechoka sana ukilinganisha na ya Dar..magari yanayouzwa Mwanza yametumika Dar kisha yakauzwa huko..inasemekana 70% ya magari yanayoingizwa nchini hubaki Dar..na yanapochoka huuzwa huko mikoani
 
Gari za Mwanza ni bei chee kweli shida ni wamiliki wa magar huko hawajui kuyatunza
Unakuta gari mtu anatembelea vioo wazi ili aonekane na watu wakat gar ina ac inasababisha ichoke ndani mapema
Unakuta mtu hajui mambo ya kufanya service gari inakufa vipur ye yuko tu anakomaa so unashangaa gari mpya inaanza kumsumbua

Yes gari za mwanza used ni cheap but ukibahatisha ambayo haisumbui shukuru Mungu
 
Magari ya Mwanza mengi yamechoka sana ukilinganisha na ya Dar..magari yanayouzwa Mwanza yametumika Dar kisha yakauzwa huko..inasemekana 70% ya magari yanayoingizwa nchini hubaki Dar..na yanapochoka huuzwa huko mikoani

Hapo nimekupata mkuu, but how about yale
Magari unakuta halijatumika sana nchini

Lets say namba DYZ, nmekuta harrier mwanza anauza 15m while dar 22m, na wote ni DY

Na pia dar gari hio hio moja unakuta bei tofauti, kuna harrier nmekuta madalali watano kila mtu bei yake 16m, 17.5m, 19m .. na ni gari hio hio
 
Back
Top Bottom