Kwa sasa kuishi Dar es Salaam ni utumwa na mateso makubwa mno

Papaa Gx

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
10,244
15,960
Hii Dar es Salaam sijajua ni kwa nini watu wanaipaparukia kiasi hichi, huu mkoa una paishwa tu lakini hamna kitu kabisa. Mkoa umejaa shida kila mahala.

Nitaongelea sekta ya usafiri, japo ki uhalisia kila sekta kwa Dar es Salaam ni matatizo. Raia wanao kaa Dar es Salaam wanapata kero kubwa Sana kwenye hii sekta. Usafiri kwa Dar es Salaam limekuwa ni janga ambalo linautesa mkoa huu kwa miaka mingi sasa, kero ya usafiri hasa wakati wa asubuhi na jioni ni mateso kwa kweli.

Siku mbili nyuma nilitoka huko mnako ita mkoani, jioni moja nikachukua pikipiki nikaanza kukata mitaa kwenye jiji la Dar es Salaam. Kiukweli ile jioni niliwaonea huruma sana wakazi wa huu mji wenye kipato kidogo cha uchumi, kila kituo nilikuwa nakuta nyomi la watu na hakuna dalili yoyote ile ya usafiri kuja. Niliwaonea huruma sana wale wanafunzi, nililia sana ndani ya moyo.

Njiani raia wengine wanatembea kwa miguu kutokana na usafiri kuto kuwepo, nilimchukua jamaa mmoja maeneo ya Uhasibu akanieleza yeye katembea umbali mkubwa mno na hakuna nafuu yoyote ile. Kutoka Posta mpaka Uhasibu, nilimuonea huruma sana. Raia mnaokaa maeneo ya Mbagala kwenda Mbande kutokea mjini aisee mko wengi ni hatari, poleni sana kwa kadhia mnazo kumbana nazo.

Mimi nalia na wale wanafunzi ule wakati wa asubuhi na jioni kwa kweli wanapata shida sana, ningekuwa na uwezo ninge mwaga mabasi kumi yawe yanabeba wanafunzi tu. Kiuhalisia jiji la Dar es Salaam bila kuwa na usafiri angalau pikipiki ni mateso na utumwa mkubwa mno, na hapa wanao umia ni wale wenye uchumi mdogo. Miundombinu yenyewe ni mibovu mvua kidogo tu ni shida kwa kweli.

Rai yangu kwa serikali ikamilishe haraka ule mradi wa mwendokasi ili iwe rahisi kwa wakaazi wa Mbagala na majirani zake. Watu mnarundikana Dar es Salaam wakati kuna mapori makubwa huko mnako mkoani, maisha ni popote wakuu. Kwanini uwe mtumwa kwenye jiji lenye matatizo chungu nzima.

Dar es Salaam bila ya kuwa na usafiri wako binafsi ni utumwa wa hali ya juu, wakuu tutafute hela.
 
Mkoa wenye Uchumi mkubwa alafu wakazi wake wanaishi kwa shida,sijui pesa zinazokusanywa huwa zinakwenda wapi!!!
 
Mnakukandai dar na kudai mkoani mapori mengi ila umasikini uliopo huko ni afadharu ya dar.

Huduma za kijamii vijiji vingi ni duni, shule huko maporini ni changamoti, mtandao wa simu ni kisanga( mara nyingi unaukuta mmoja au miwili tu)

Mjini ni akili tu, hizo adha za usafiri kupanga ni kuchagua.
 
Back
Top Bottom