yogan
Senior Member
- Feb 26, 2013
- 133
- 85
Mimi ninauza genge la mboga mboga na matunda.Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa biashara katika masoko ya jijini Dar es salaam kama Mabibo, Buguruni, Temeke, Stereo na Ilala.
Katika masoko yote haya hakuna mkulima anaruhusiwa kuuza BIDHAA zake sokoni. Mzigo unapofika sokoni Wanakabidhiwa MADALALI ndo wanauza kadiri ya makubaliano na mkulima.
Chakusikitisha ni kwamba hawa jamaa wanafaidika sana hata kuliko wakulima wa nchi hii kwani wanatumia faida ya wakulima kutohusika kuuza BIDHAA nao kupandisha bei za BIDHAA kiholela.
imefikia hatua hata BIDHAA zikiwa zimefurika sokoni bado wanaziuza bei ya juu Jambo linalosababisha wakulima kupata hasara kwani kuna bidhaa huharibika kwa kukosa wateja. Mpaka sasa Mimi sioni umuhimu wa madalali sokoni kwani wanaleta maisha magumu bila sababu za msingi.
Hawa jamaa wakuondolewa bidhaa zitauzwa Kwa mfumo huru WA kibiashara na kuzingatia chain ya demand na supply ambayo inaweza kutupa unafuu wa maisha yetu.