Kwanini baadhi ya binaadamu wanakuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi?

Kwanini baadhi ya watu wanakuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi yani unaweza kukutana na mtu ana vipaji vingi ukastaajabu na uwezo wake aliojaaliwa?
kila mtu akaja hapa duniani na talanta yake ndugu, wewe fanya kwa bidii hadi pale uwezo wako unafikia, hapo ndipo uliumbwa napo, usijilinganishe san ana wengine. labda kama una uwezo kama wao.
 
Lakini unakuta mtu anaweza kufanya mambo mengi tofauti na watu wengine
 
wao mazingira yamewaruhusu kujaribu na kuonyesha vipaji walivyojaalwa, ni tofauti na wengine mtu ana kipaji flani ila hawezi kujua hakuna mazingira ya kujaribu, pia maslahi yanaingilia

wengine wenye vipaji vya kucheza basket ila wapo vijijini hakuna viwanja

wapo wenye vipaji vya kuogelea ila wapo sehem zisizo na mabwawa

wapo wenye vipaji vya kuimba ila wanatishwa na wazazi mziki uhuni

wapo wa kushona viatu ila hawawezi hata kujaribu wanaona ni kazi ya chini sana
 
Back
Top Bottom