Kwanini madhehebu mengi ya kikristo tunafumba macho wakati wa kusali?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,396
4,138
Hivi karibuni nimejikuta naanza kuhoji baadhi ya vitu ambavyo ninaamini wengi tunavifanya kwa mazoea.

Jinsi ya kusali kwa kufumba macho ni kitu kingine ningependa kujua msingi wake.Je nisipofumba macho,nitakuwa nimepoteza nini?

Mambo mengi yameingia katika ukristo kidogo kidogo na vizazi vinarithi na kushindwa kuhoji. Nikiviorodhesha ni vingi sana,na ukiuliza kanisani wale wanaojifanya watakatifu zaidi kuliko watu wengine, watakukemea na hata kujengewa chuki.Naamini hapa wapo wateule wa Mungu wanaweza kunipa maarifa.

Asante sana
 
Ni suala la imani kuwa unapofumba macho hisia na fikra zako zote unazielekeza kwa muumba wako

Hiyo ni sambamba na kupiga magoti wakati wa maombi ni ishara ya unyenyekevu na heshima

Haimaanishi ya kuwa ukisimama, ukikaa sivyo, ila ni kuupa uzito maombi yako

Mengine wataalamu wa theolojia wataeleza
 
Kama hayo ndiyo majibu sahihi,basi tunahitaji kijifunza maana huenda ni njia ya kumtukuza shetani na sisi hatujui
 
Hivi karibuni nimejikuta naanza kuhoji baadhi ya vitu ambavyo ninaamini wengi tunavifanya kwa mazoea...
kwanza umewahi kuomba? Lengo la kufunga macho ni kumakinika ndani rohoni, huwezi kuomba Mungu huku unakodoa macho. Kwanza utaonekana kituko, funika macho wakati unaomba huo ndio utaratibu unapokuwa kwenye maombi.
 
Nilishangaa kuona pastori mmoja kwenye luninga anaomba huku kakodoa macho. Maombi gani hayo? Alitakiwa afunike macho
 
Kwanza kabisa hukuna sehemu yoyoye katika Biblia inayoagiza watu kufumba macho wanapoomba,Kwa hiyo swala la kufumba macho ni swala la kisaikolojia.Watu hufumba macho Ili kuzuia chochote tofauti na maombi unayomba kisiingie kwenye tafakari yako hata hivyo lazima uangalie mazingira uliyopo wakati unayomba kama yanaruhusu kufumba macho au la.Kufumba macho au kutokufumba wakati wa kuomba hakuna tatizo Kwa hiyo unayemuomba.
 
Aya tufumbe macho tuombe

Baba katika jina la Yesu nakemea roho ya kutokufumba macho wakati wa kuomba ..na ishiiindwee ..nasemaaa na ishindweee

Antanananarivo..ashakalabagia....
 
Sio Lazima kama hutaki...
Kuna maandiko mengi Tu walioinamishi vichwa, waliotazama juu, walikuwa macho, n.k
Kufunga ni heshima Tu kwatuliza kutangatanga Kwa mawazo
 
Hivi karibuni nimejikuta naanza kuhoji baadhi ya vitu ambavyo ninaamini wengi tunavifanya kwa mazoea.

Jinsi ya kusali kwa kufumba macho ni kitu kingine ningependa kujua msingi wake.Je nisipofumba macho,nitakuwa nimepoteza nini?

Mambo mengi yameingia katika ukristo kidogo kidogo na vizazi vinarithi na kushindwa kuhoji.Nikiviorodhesha ni vingi sana,na ukiuliza kanisani wale wanaojifanya watakatifu zaidi kuliko watu wengine,watakukemea na hata kujengewa chuki.Naamini hapa wapo wateule wa Mungu wanaweza kunipa maarifa.
Asante sana
Lakini pia kuijua imani huendana na kushiriki katika ibada na mafundisho ya dini
 
Tunafumba macho ili kutoruhusu macho kuona kitu ambacho kitaleta hisia nyingine zinazoweza kukuondoa kwenye maombi!
 
Back
Top Bottom