Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,549
- 34,452
Sifa mojawapo ya kuwa kiongozi wa umma ni kuwa na maadili yanayokubalika kwa wananchi. Kiongozi wa chama cha siasa ni yule mtu anayesimama mbele kwa niaba ya chama chake kwenye maslahi ya wananchi wote bila ya kujali kama ni wanachama wake ama la.
Kama kiongozi anaona kuawa kwa watu ni jambo la kawaida sana na anaona ni sawa kukaa na watu walioua wanachama wake, ni mtu wa hatari sana. Mbele ya safari Zitto anaweza kufanya au kukubali jambo lolote lile ili mradi yeye maslahi yake yalindwe.
Kauli hii imenisiktisha sana. Yaani mtu aliyemiminiwa risasi 38 kama Tundu Lissu ama aliyechapwa mijeledi kama Godbless Lema unawezaje kudhani kuondoka kwao ili kuwa ni kwa kujipendea. Yeye anayedai alibaki kupambana alipambana kivipi na kuhusu nini ambacho sisi hatukijui?