Kutomuamini Mungu ni ujasiri?

Hakuna Mungu/mungu kwa maana ya sifa na tabia mlizozianisha kwenye vile vitabu vyenu.

Hakuna Mungu/mungu kwa aina ya vitisho mnavyowatishia watu

Hakuna Mungu/mungu kwa sababu sababu Hana athari kwenye maisha yako wewe, vizazi vyako na Taifa kwa ujumla.

Ndio maana ikaiwa Imani tu
Bahati mbaya mliyonayo Mungu Alisha jifunua Kwa watu na ameshafunga huo ukurasa kilichobaki Sasa ni maandiko tu

Wajinga hawawezi kuisha hapa duniani hata kama Leo hii Mungu atajifunua kwenu na mkaamini kuwa yupo believe me miaka 200 ijaya watatokea tena wajinga kama nyinyi watasema hakuna Mungu
 
Alijifunua kwa nani?
Babu mzaa Babu yako?
Bibi kizaa bibi yako?
Au Mwanaume aliyemzaa Babu aliyemzaa Babu wa Babu yako?

Sasa wewe mwerevu ulijuaje kwamba huyo ni Mungu/mungu?
 
Na hiki ndicho waliotuletea hizo dini walichokitaka (UOGA) na wamefanikiwa 100% kwa waafrikaView attachment 2756463
Mbona hata wazungu wanaamini uwepo wa Mungu na dini ndio imeshape maisha na maendeleo Yao.
Soma historia ya wazungu utayakuta haya.
Halafu nani kakuambia Mwafrika anaijua dini wengi wanashika dini na Sio wanaijua dini.
Unaposema dini una maanisha positivity.
Halafu tambua Kuna God na Gods ni nguvu mbili tofaut.
Mungu ni mmoja na miungu ipo zaidi ya hio elf 3.
Mwafrika angeijua dini asingekuwa masikini.
 
Mzee umemkosea sana mungu sema kuna sehemu mnafeli maombi yanaitaji mtu uwe msafi kiroho sasa wew Msela nondo ni ngumu kuamini kwanza ndio unaweza nguvu za mungu au kunyakati hujazifikia wew ishi ila Kuna siku anaweza kukuaminisha yupo
Kama yupo basi ye ndio kanikosea sana kwanini ajifiche?

Kwanini kutimiza majukumu yake ya msingi ni mpaka mimi nimuombe tena kwa kujitesa sometimes anataka nikae na njaa (nifunge)

Na hata ukifanya hayo yote bado hakuna kitu anafanya

Morroco watu wanakufa kwa sababu yake, aliumba ulimwengu mbovu wenye kuruhusu matetemeko yanayoua maelfu bila hatia.

Mungu huyu anayeona hayo yote yanayoendelea huko Morroco bado tena anahitaji kukumbushwa ndio afanye kitu, na still hata ukimkumbusha bado ni kazi bure hawezi kufanya chochote.

Ni Mungu ambaye kama yupo basi anatakiwa kutuomba msamaha wa magoti na mchozi.
 
Hivi huku duniani kuna ambao wanamuani Mungu? Kivipi na kila siku kuna mauaji, usinzi, uongo, utapeli na dhuluma tena vinavyanywa na kufurahiwa na watu wale wale ambao kila siku wapo misikitini na makanisani tena wengine ni viongozi wakubwa kwenye dini hizo
 
Unajua upendo haulazimishwi lakini dini zinalazimisha waumini wake kumpenda Mungu kwasababu wamewekewa hofu kuwa kwa wasiomuamini wataenda kuzimu.

“Mungu ni upendo” (1 Yohana 4:8)

Hapo Biblia inatueleza kuwa Mungu ni upendo. Kwanini Mungu mwenye upendo alitengeneza kuzimu? Akawapa binadamu free will akijua fika wapo watakaobisha uwepo wake. Mungu pamoja na uwezo wake wote akaruhusu binadamu wateseke.

Kwanini Mungu anataka kuombwa, kutukuzwa, kusifiwa? Alituumba kwanini hakufanya tumjue yeye bila kupitia dini maana kila dini inamuelezea Mungu kwa aina yake.

Mwisho wa siku uwepo wa Mungu na maisha baada ya kifo ndiyo silaha inayotumika kuwafanya waumini wa dini kuishi maisha ya hofu Duniani.

Hata Thomas, mwanafunzi wa Yesu hakuamini hadithi za ufufuo wa Yesu Kristo alitaka ajionee yeye mwenyewe.

Vitabu vya dini ni kama vitabu vingine vya hadithi tu.
 
Nyie watu wa dini sijui mna akili za namna gani kwanza sio wavumilivu kwa wale wasio kubaliana na mafundisho yenu.

Mnapenda kuforce watu wote wawe kama nyie kuishi, kufikiri na kutenda.

Halafu wanafiki sana nyie sijui mafundisho yenu ndio yana haya maujinga ni watu mlio na tabia za kijinga zisizo vumilika.

Kwa mfano wewe hapo watu wasiopo muamini sijui huyo Mungu wako wewe unaathirika nini ? mbona wasio amini wapo ok ila wewe ndie unashwa na kugadhabika wasipo muamini huyo Mungu wako ?
Watu wamekuwa wakiaminishwa vitu visivyokuwepo na visivyokuwa na msaada zaidi ya kutiana ujinga na umaskini, vikiendelea kunufaisha watu wachache, dini ni ujinga na utapiamlo wa ubongo.
 
Watu ambao hawamuamini MUNGU, hawafai kuanzia kwenye ngazi ya kifamilia mpaka ya kitaifa na kimataifa.. sio wa kuwaamini kabisa.

Ukiwa na imani ya MUNGU.. Moja kwa moja inakujengea hofu ya kufanya mambo maovu. Hivo unajichunga wewe kama wewe kuhakikisha huwakosei binadamu wenzako. Na hapo utu ndo unapojengeka
Watu hatuamini huwepo wa hivyo vitu lakini tunatenda yale yanayapaswa kutendwa na binadamu mwenye utu na aliyestaharabika, endeleeni na unafiki wenu...kabla ya hizi dini mababu zetu walikuwa wanaishi vipi?
 
Watu ambao hawamuamini MUNGU, hawafai kuanzia kwenye ngazi ya kifamilia mpaka ya kitaifa na kimataifa.. sio wa kuwaamini kabisa.

Ukiwa na imani ya MUNGU.. Moja kwa moja inakujengea hofu ya kufanya mambo maovu. Hivo unajichunga wewe kama wewe kuhakikisha huwakosei binadamu wenzako. Na hapo utu ndo unapojengeka
Bullshit. Watu wanaomuamini Mungu ndio watenda maovu kuliko wasiomuamini Mungu.
 
Mbona hata wazungu wanaamini uwepo wa Mungu na dini ndio imeshape maisha na maendeleo Yao.
Soma historia ya wazungu utayakuta haya.
Halafu nani kakuambia Mwafrika anaijua dini wengi wanashika dini na Sio wanaijua dini.
Unaposema dini una maanisha positivity.
Halafu tambua Kuna God na Gods ni nguvu mbili tofaut.
Mungu ni mmoja na miungu ipo zaidi ya hio elf 3.
Mwafrika angeijua dini asingekuwa masikini.
Huyo God ana tofauti gani na hao Gods?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom