All the best
Screenshot_20230730-033307.jpg
 
Habari yako mwanajamii, nina imani ulipo unaendelea vema, kama haupo sawa Mungu akutangulie katika jambo lako.

Leo tena nimepata muda wa ku-share vitu nilivyopitia katika maisha yangu.
Mimi ni mzaliwa wa Nyanda za Juu Kusini (Songwe -Mbozi) nimesoma shule ya primary Songwe Mwaka 2008 na nikajiunga na elimu ya Secondary huko kwetu Songwe, na high level nimesoma BIHAWANA secondary iliyopo kanda ya kati .

Japo nilisoma kwa kuunga unga kwa sababu ya uchumi wa Nyumbani haukuwa sawa,Baadae nikajiunga na Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) kwani nilifurahi sana kujiunga na elimu ya juu sababu ilikuwa Ndoto yangu ,kwa maana hiyo nilijua Ndoto zangu zimetimia na kuwasaidia wazazi wangu ambao walipata shida sana muda wa kunisomesha na muda huo nilikuwa mnufaika wa mkopo.

Maisha ya Chuo yaliendelea ndani ya miaka minne kwani nimesoma fani ya afya(UKUNGA)-MIDWIFERY.

Mungu ni mwema nilifanikiwa kuhitimu masomo yangu ya chuo kikuu na baada hapo nilienda kwenye mafunzo ya vitendo (internship) ndani ya mwaka mmoja katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mwanza(Sekeo Toure).

Baada ya hayo mafunzo hayo kuisha ikanibidi niendelee na maisha ya mtaani ya kawaida ili kujipatia riziki na muda huo naendelea kutuma maombi ya kazi kwenye taasisi mbalimbali japo ilikuwa ngumu sana kupata maana taasisi nyingi zilinipa masharti ambayo niliona kama magumu kwangu,kwani walikuwa wanahitaji wenye uzoefu na mimi nilikuwa naambiwa nifanye kazi bila malipo ndani ya miezi mitatu ili nipate uzoefu kwani ilinipa ugumu kufanya kazi bila malipo nilikuwa sina chanzo chochote cha kujipatia fedha ya kujikimu (chakula na pango),maisha yangu yalikuwa magumu sanaa kwani nilikuwa sina kazi maalumu.

Hatimae nilipata kazi ya kufundisha chuo cha afya huko Rorya sehemu moja inaitwa SHIRATI nilifanya kazi kwa nguvu na moyo wote kwani nilikuwa nimeteseka mtaani kwa kufanya kazi za kuunga unga ili kujipatia kipato lakini bado juhudi zangu hazikuzaa matumaini kwani malipo yalikuwa ya shida sana mpaka ikanibidi nishindwe kujikimu.

Nilishindwa kuendelea na kazi na Kurudi tena MWANZA kwani nilipazoea MWANZA sana kwa sababu niliishi kwa muda mrefu na kuzoea mazingira japo nilikuwa sina kazi maalumu ya kujipatia kipato.

Nilipoona hali yangu ngumu kuna jama yangu alinikopa fedha shilingi laki moja na nusu(150,000/=) ambayo tayari nilikuwa nime-plan kuanza biashara ya dagaa wakavu nilikuwa nanunua na kuuza minada ya karibu Mungu ni mwema niliona maisha yangu yanabadilika na kujikimu kabisa.

Mtaji wangu ulikua mpaka milioni mbili(2,000,000/=) hivyo nilijikuta nachukua mzigo mkubwa zaida na kupata faida zaidi nikaanza kupeleka mikoa ya karibu ,kila hatua Mungu alinisaidia kwani mtaji wangu ulikuwa sana kuliko matarajio yangu nilifikisha zaidi ya million 25 (25,000,000/=) nilitanua wigo zaidi ikanibidi nifungue ofisi soko kuu la dagaa Mwanza(KIRUMBA MWALONI MWANZA)

Namshukuru Mungu biashara yangu ilienda vizuri na kuuza kwa bei ya JUMLA na kuwauzia wateja wa mikoani.

HITIMISHO.
Biashara ya chakula kama dagaa ni bidhaa inayolenga watu wenye kipato cha chini na watu wa chini ndio wengi kwa hiyo ni moja ya biashara inaweza kukutoa kimaisha.

Japo biashara ni nyingi zinazolipa na hii pia inakutoa endapo ukapambana.

Pia vijana waliomaliza vyuo na ambao hawajasoma usikate tamaa maana kila jambo linahitaji umtangulize MUNGU.

KWA AMBAE ATAHITAJI MZIGO/DAGAA/USHAURI KWENYE HII KAZI UNAWEZA KUNITAFUTA WHATTSAPP/PIGA .
0755213580.
AU UNAWEZA KUFIKA KIRUMBA MWALONI MWANZA KWENYE SOKO LA DAGAA
View attachment 2702048
Umeelewa nini hapo?Wewe majaaliwa yako ni biashara na siyo usomi wa ukunga/midwifery!Umekuwa allocated kiroho bila kujua.Unakomaa na kusoma kumbe huko siyo kwako.
ANGALIZO
Tusome na kuitafuta elimu kwa bidii no matter what!
 
Mtoa mada ana akaunti ambayo ndiyo yatoa majibu humu, maana hiyo account ndo imetaja faida

Jinsi biashara inavyofanyika

Jinsi alivyoshuhudia faida ikipatikana.

Kuweni makini
 
Vijana tunazingua sana

Mtu umefanya Intern mwaka mzima unalipwa ila baada ya miezi michache baada ya kumaliza unakopa 150k.
 
Back
Top Bottom