Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,095
- 4,417
Nyakati huja na nyakati hupita
Na nyakati ambazo huja na kupita, zingine huja kwa namna yake na changamoto zake, na zinapokuja, huja ili zibadilishe kitu na ama kuharibu kabisa,
Kikawaida, Ni mjinga tu ambaye hudhani Dunia haina Changamoto na kwamba anaweza kukaa maisha yake yote bila kupitia dholuba, Changamoto huwa zipo kuanzia kwenye familia zetu, taasisi mbali mbali mpaka za dini na vyama mbalimbali za kiraia na kisiasa, sembuse suala la Muungano lililokaa kisheria? Na nijuavyo, Sheria ambazo watu huzitunga, hufikia hatua zinapitwa wakati na hivyo huhitajika kurekebishwa ili zifiti kwa wakati uliopo
Na ndiyo maana hata Katiba hufanyiwa marekebisho na ama kuandikwa upya ili iendane na wakati au mahitaji ya wakati huo n.k
Linapokuja suala la kwa nini Muungano unawafeva watu fulani na kuwakandamiza watu fulani, na kelele hizo zikaendelea sana, iko haja kwa mamlaka kuanza kuchukua hatua kwa kufanyia kazi mahitajio hayo ili mambo yaende sawa,
Maswali ya kikatiba kuuhusu muungano yaliyoibuliwa na mwanasheria wa kimataifa Tundu Lissu, wanaojaribu kujibu, hakuna hata mmoja aliyesema si ya kweli,
Ukiwasikiliza wate wanaojaribu kujibu, utakuta wameyaacha maswali hayo kwa maksudi kabisa na kisha kuwamwagia sifa viongozi waliotoka/wanaotoka upande wa pili, eti wanafanya na wamefanya mambo mazuri tu Tanganyika
Wanashindwa kuelewa kinachoulizwa siyo ubora wa utendaji kazi wa viongozi hao isipokuwa ni ubovu wa sheria zinazolinda muungano wetu kama alivyobainisha mh.Tundu Lissu
Kwa namna vijana wa CCM wanavyojitutumua kujaribu kupotezea hoja hiyo, ni sawa na kujaribu kuzuia mafuriko ya Tsunami kwa udongo wakijua fika hawataweza
Muda umefika kwa kamati maalumu inayoshughurikia masuala ya muungano wetu, wakazichukua hoja hizi pia ili zipatiwe mwafaka na kisha tusonge mbele kwa umoja wetu
Tulikotoka na mahali tulipo kama Nchi, bado Mungu wetu amekuwa mwema sana, ila kwa sasa kuna alarm inagonga, basi tusisubiri muda ukaenda sana badala ya kujenga ukuta tukajikuta tunalazimika kujenga nyumba upya