Kupata Haki ni gharama sana kwa nchi yetu, mnasabisha watu kujichukulia sheria mkononi na kuachana na mifumo ya haki jinai

kijana wa leo

JF-Expert Member
Nov 28, 2011
2,856
7,005
Leo niliibiwa materials kutoka eneo langu la kazi Mkoa A, baada ya kufatilia nikagundua mwizi amesafiri kwa njia ya Bus kuelekea mkoa B, nikafanya mawasiliano na Police wa mkoa B, wakanipa ushirikiano na kumkamata mwizi wangu akiwa na hayo material kwenye Bus kama nilivo report, na bahati nzuri alikiri kuyaiba kutoka Mkoa A.

Sasa, kwanza police wa Mkoa B wakanishauri kufungua kesi katika mkoa yalipoibiwa ambao ni mkoa A, nimetekeleza hilo na kuandika maelezo katika kituo cha police mkoa A, na kupata RB number ambayo niliwatumia police wa kituo cha Mkoa B wanaomshikiliwa mtuhumiwa.

Sasa, sa hivi nimeambiwa natakiwa kumsafirisha mtuhumiwa, ushahidi pamoja na askari kwa gharama zangu mwenyewe, ili aje kushtakiwa mkoa A, na bado mkoa A na B police wote wanataka posho kwa kushughulikia swala langu.

Sasa najiuliza pamoja na kuibiwa Mali zangu, bado natakiwa kutumia gharama zaidi ili nipate haki yangu.

Nimewambia sina hela kwa Leo ya kumsafirisha wanasema wanamwachia mtuhumiwa pamoja na kuwapa RB number.
 
kwa huu ujunga wa nchi yetu ndo maana kuna watu wanaamua kumaliza juu kwa juu tu
 
Kumuachia ni makosa inatakiwa ashikiliwe Hadi utakapo pata pesa ya usafiri.
Nenda kituo A kaongee na OCD aongee na mwenzake wa kituo B hao ni askari wadogo njaa inawasumbua weekend hii
 
Kuna hii kasumba nyingine ukilipoti tukio polisi na ikitakiwa wakamkamate mtuhumiwa watakudai uwape hela ya mafuta.
 
Kuna hii kasumba nyingine ukilipoti tukio polisi na ikitakiwa wakamkamate mtuhumiwa watakudai uwape hela ya mafuta.
Then unatumia gharama kuliko thamani ya ulichoibiwa.
Ila gharama zote unazijumlisha mtuhumiwa ndie atakuja kuzilipa
 
Pole sana.
Ukiibiwa gharama za kukamata mtuhumiwa ni kubwa kuliko thamani ya ulichoibiwa.

Jifunze kusamehe au kumalizana juu kwa juu kimtaa mtaa.

Kitendo cha kwenda kushitaki tu polisi ni lazima utoe hela.

Hapo ukiwachekea watakupuna hadi maji uite mma, af walivyo walafi wanakula kote kote kwa mshitaki na kwa mshitakiwa atakae mzidi mwenzie maokoto ndio wanakuwa upande wake.

No money no haki.

Polisi ni laana
 
Kama kuna mtu unamuamini uko mkoa B mtume akachukue materials zako mambo yaishe.
Hawampi ng'o!
Unawajua polisi au unawasikia.
Polisi kuwaweza nenda nao kipolisi polisi. Km unajamaa mkubwa polisi mtumie huyo.
Ila hakikisha awe mkubwa kweli
 
Back
Top Bottom