Kuna ulazima wa kuanza Certificate kama unataka kusoma Diploma?

ozn

Member
Jan 19, 2022
27
19
Wakuu habari za majukumu.

Naomba kuuliza kama Kuna ulazima wa kuanza na certificate kwa mtu mwenye matokeo ya o level Physics-C, Chemistry B na biology-B na anataka kusoma diploma in clinical medicine
 
diploma ndo certificate labda huelewi maana ya certificate utapiga miaka mi 3 lazima ndani yake kuna NTA Level 4,5 na 6
 
  • Thanks
Reactions: ozn
Labda mtoa mada kuna kitu hakijaelewa. Hiko hivi, mfano ukitaka kusoma Diploma in Sanitation Engineering (ya miaka mitatu):

Mwaka wa kwanza ni Basic Technician Certificate in Sanitation Engineering.

Mwaka wa Pili ni Technician Certificate in Sanitation Engineering.

Mwaka wa Tatu ndio Ordinary Diploma in Sanitation Engineering.

Uzuri (na ubaya kwa upande mwingine) ukisoma Diploma kila mwaka ni exit. Inamaana unaweza kufanya jumla ya graduation 3 hadi unavopata diploma na pia unakua na vyeti vitatu ukiamua. Ila wengi uwa wanafanya graduu moja tu ya mwisho na cheti wanaomba kimoja.
 
Wakuu habari za majukumu.

Naomba kuuliza kama Kuna ulazima wa kuanza na certificate kwa mtu mwenye matokeo ya o level Physics-C, Chemistry B na biology-B na anataka kusoma diploma in clinical medicine

Hesabu na english una ufaulu gani?
maana hayo mengine una vigezo .
 
Haiwezekani ni lazima kuanzia certificate .
Hapana Unaweza kuanza diploma bila ya kupitia certificate kama una vigezo vya kujiunga diploma ambavyo nadhani ni D 4 kwa kozi nyengine ila afya unatakiwa uwe na B ya kemia , B ya biology C ya physics C ya hesabu na C ya english kama sikosei .

Kwa yeye ana hivyo vigezo ila sijajua kwa somo la hesabu na english.
 
diploma ndo certificate labda huelewi maana ya certificate utapiga miaka mi 3 lazima ndani yake kuna NTA Level 4,5 na 6
Diploma si certificate mkuu certificate ina level 3 na unasoma kila level moja mwaka mmoja na diploma ina level 3 pia ambayo kila level ina mwaka mmoja pia.

Kwa mfano kwa kozi za uhandisi kuna level 4 =basic technician, level 5= technician/qualified technician 6= diploma
 
nafikiri umejijibu kwamba certificate ina level 3 ndo diploma, kumbuka hapojuu nilisema ili upate diploma unapitia NTA level 4,5 na 6 kwa mtu wa form four mwenye zaidi ya D 4 kwa vyuo vya kati siyo VETA
 
Hapana Unaweza kuanza diploma bila ya kupitia certificate kama una vigezo vya kujiunga diploma ambavyo nadhani ni D 4 kwa kozi nyengine ila afya unatakiwa uwe na B ya kemia , B ya biology C ya physics C ya hesabu na C ya english kama sikosei .

Kwa yeye ana hivyo vigezo ila sijajua kwa somo la hesabu na english.
Afya unaweza kwenda kusoma diploma unaanzia level 4-6 chamsingi uwe na D4 za sayansi yaani physics,chemistry na biology, ukiwa na D ya english na hesabu hizo ni za nyongeza tu
 
Back
Top Bottom