UZUSHI Kula nanasi kunafanya uke unukie vizuri

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu mko salama?

nanasi.jpg

Nimekuwa nikisia stori nyingi kuhusu nanasi, kuwa ukila unafanya uke kuwa na harufu nzuri, wengine wanasema unaongeza "ladha", yaani ute/maji maji yanakuwa na utamu kama vile umechanganywa na sukari hivi?

Kuna ukweli kwenye hili wataalam wa JamiiCheck?
 
Tunachokijua
Nanasi ni miongoni mwa matunda yenye ladha nzuri mdomoni, lakini pia lina vitamini nyingi na virutubisho vyenye uwezo wa kuupa mwili nguvu na kuepuka kushambuliwa na maradhi.

Nanasi lina virutubisho vya vitamin A,B na C na lina madini ya chuma, kopa na Phosphorous ambayo ni muhimu kwa afya ya binadamu.

images
Ni kweli kula Nanasi kunafanya uke unukie vizuri?

JamiiCheck
imezungumza na Dkt. Elias Kweyamba, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi ambaye ameeleza kuwa si kweli kuwa kula nanasi kunafanya harufu ya uke iwe nzuri.

Dkt. Elias Kweyamba amesema: Hapana, Si Kweli, hii ni imani hamna uhusiano katika ya kula Nanasi na kufanya uke unukie vizuri.

Unapokula chochote kinaenda kwenye utumbo na mfumo wa damu, hivyo hakuna uhusiano wowote wa Kisayansi.

Chakula kinaenda kwenye utumbo na mfumo wa damu, harufu itasikika kwenye haja kubwa pia huwa imechanganyika na vitu vingine hivyo harufu hutoka tofauti.

Vinywaji vinanvyoyeyuka mwilini kama pombe kali vinatoka kama jasho na mdomoni na hapo ndipo utaweza sikia harufu hio.

Aidha, Wanawake wengine hujifukiza na udi ili uke unukie lakini hamna uhusiano wowote.


Kutokana na maelezo ya mtaalam wa afya kuwa si kweli kula nanasi hufanya harufu ya uke kuwa nzuri hivyo JamiiCheck imejiridhisha kuwa nadharia hiyo si ya kweli.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom