KWELI Kubana pumzi wakati wa tendo la kujamiiana kunamfanya mwanaume achelewe kufika mshindo

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Wakuu,
1713486213109.jpeg

Nimesikia sikia sehemu kuwa wakati wa tendo pale mwanaume akiwa anabana pumzi stamina inakua inaongezeka na anaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi.

Kuna mwenye amewahi kushuhudia hili au kuna maelezo ya kisayansi yanayothibitisha hili? Mimi naona nilipigwa kamba tu hapa!



Kwenu wataalam wa JamiiCheck, ni ukweli au uzushi tu?
 
Tunachokijua
Kupumua ni kitendo cha kusukuma au kuvuta hewa ndani na nje ya mapafu kupitia pua au mdomo ili kuweza kubadilishana gesi na mazingira ya ndani, hasa kwa kuleta oksijeni na kutoa kaboni dioksidi.

Ngono (Tendo la ndoa) ni kitendo cha kujamiiana kati ya mwanamke na mwanamume ambapo tendo hilo humalizika vizuri kwa wenza hao kufika kileleni

Kufika kileleni ni msisimko wa kipekee unaoleta hisia nzuri baina ya wenza wanaojamiiana na huwa ni moja ya ishara ya kumalizika kwa haja za tendo hilo.
images
Je, ni kweli kubana pumzi wakati wa tendo kunaweza kusababisha Mwanaume kuchelewa kufika kwenye mshindo?

JamiiCheck
ilimtafuta na kuzungumza na mtaalam wa Afya, Dkt. Godfrey Chale Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake ambae alibainisha kuwa:

Ni kweli inawezekana kubana pumzi wakati wa tendo kunaongeza nguvu kwa Mwanaume na kuweza kuendelea na hilo tendo kwa muda.

Unapofika kuelekea katika hali ya mshindo, mwili unakuwa unajiachia, hivyo kwa kubana pumzi unakuwa umeuzuia mwili kuendelea kujiachia.

Kubana pumzi ni mojawapo ya njia ya kujizuia, kwa Kiingereza inaitwa “stop-start technique”. Ukiona ukaribia kufika mshindo unabana pumzi huku ukiwa unabana makalio, hili huzuia manii zisitoke, hivyo unaweza ukaendelea na tendo.


Kutokana na majibu ya mtaalam wa afya JamiCheck inathibitisha kuwa ni kweli kubana pumzi mwanaume akiwa anakaribia kufika mshindo humsaidia kuchelewa kuchelewa kufika mshindo.
Acha kuskia skia mambo mkuu,hebu jaribu uone kama huta kunya
Wenye wamekutana na wabana pumzi wapo ndio watupe uzoefu, ili tukikutana na mtu anabana tusishangae, pia wataalamu hapa JamiiCheck watanyoosha maelezo kama ni kweli au fix tu
 
Mkuu una ka experience?
Yeah nina experience nayo nimewahi practice kwa mda fulani and it works. Cha kufanya ni hivi unatakiwa ubane pumzi then uwe una release taratibu sana yaani kiasi mtu akikuangalia ahisi kama haupumui hivi.

Ukizoea hivi utakuwa ni mtu wa ku last mda mrefu sana on bed
 
Kubana pumzi katika tendo la ndoa hakukufanyi kuwa Strong sababu tendo la ndoa ni mchakato hadi kukamilika kwake na nguvu nyingi hutumika hasa kwa mwanaume sasa huwezi kubana pumzi mda mrefu wakati wa sex.

Ila baadhi ya watu hutumia mbinu ya kubana pumzi kama mbinu mojawapo ya kuongeza utamu wakati wa mshindo kwa mwanaume sababu kuweza kubana pumzi angalau kwa sekunde 15 pale unapokaribia mshindo hufanya mshindo kuwa mrefu kwahiyo mwanaume huweza kupata raha zaidi lakini hii ipo psychologically zaidi.

Pia kubana pumzi huweza kustimulate uwezo wa kufikia haraka mshindo pale unapoukaribia.
 
Scientifically ni kweli, nikiongea kwa wanandoa, ninyi vijana wazinzi siongeni na ninyi, oeni ili mje kwenye mambo ya kikubwa. kwa kawaida, mwanaume akibana pumsi huwa anachelewesha kuejuculate, na mwanamke ni vise versa, akibana pumzi ndio anawahi. na kwasababu kikawaida wanaume ndio huwa wanawahi kufika kilimanjaro kuliko wanawake, inashauriwa mwanamke awe anabana pumzi na kumeditate the way movement zinavyoendelea ili awahi, ili mwanaume naye akibana akachelewa walau wakutane au kama hawakutani basi mwanamke afike na ndio mwanaume naye aje.

Binafsi uwa napambana na kuhakikisha mke wangu amefika kwanza ndipo na mimi naweka msisitizo kwenye tafakuri ili nifike ama la tukutane. kwasababu wanawake wengi pale mwanzoni kama hawajaandaliwa huwa wanachelewa kushika line/connection wakati mwanaume ukishaanza tu hata bila maandalizi connection ipo, unatakiwa upige mahesabu, aidha umwandae yeye kwanzaaa hadi uhakikishe hapa sitachukua muda atafika ndipo uingie, ukianza utakuta umefika dakika 10 au 15 wakati wewe ndio unafika au unakaribia kufika, mwenzio ndio kwanza connection inaanza. ukimaliza pale lazima atapatwa na hasira kwani umemwacha njiani na dharau zitakuja tu. hii ndio maana wazungu huwa wanatake time sana kwenye foreplay ili wakienda waanze pamoja na kumaliza pamoja.

Kwa kufanya hivyo mtaepusha kujaribiwa na shetani, mtaongeza upendo, mtapunguza magombano na kununiana, mtapunguziana stress kwasababu Mungu aliweka tendo la ndoa kama jambo la furaha na linalofurahisha nafsi na ndoa yenu itakuwa ya upendo na kuvumiliana sana.
 
Huo muda wakubana mpuuzi utautoa wapi kwa K mnato , dakika ni kubwa mnoo ushamaliza kazi ,kiukweli siwezi kubana pumzi asee kwanza ntaibanaje ?
 
1. Inabidi ifahamike kuwa, round ya kwanza kwa mwanaume huwa inawahi sana, this is nature, so it is normal unless mwanaume awe na shida ktk uume wake kwa kuukomaza na masturbation, hapo anaweza chelewa sababu ule mshipa umeshaharibika kwa masturbation.

2. Mwanaume pia anaweza akawahi kumaliza tenda kutokana na nyege kuwa nyingi, kwahiyi unapowahi kumaliza elewa kwamba yamkini inaweza ikawa nyege nyingi kuwa ndani ya mwili wako.

3. Pornography pamoja umalaya wa wanawake wengi ndio chanzo kikubwa cha sex kuvurugika. Pornography na umalaya ndo vimeleta chanzo cha wanaume vibamia. Mwanaume ukimtoa mwanamke bikira mwenyewe, kamwe hatokuja kukulaumu mbeleni kwamba una kibamia au humridhishi.

Kama mwanamke anakutana na wewe mwanaume, na wewe unakuwa mwanaume wake wa 10 au na zaidi una kazi kubwa saana ya kufanya ili atulie ktk sex. Na kwa maana hii hata kama ukamfikisha kwa namna gani, yupo ambae atamkumbuka pia ktk sex mbali na wewe.

4. Sex ni suala la saikolojia zaidi, kama akili ya mwanamke haijaingizwa uchafu wa kutokukojoa, kibamia n.k ana uwezo mkubwa sana wa kutulia na mwanaume wake ila sasa akili ikisharibika kwa story za mitandaoni, vijiweni n.k hapo ndipo na yeye atatamani kujua huko kwa wanaume wengine maumbile yao yapoje, wanawake wenzao wanakojoleshwa vipi.

5. Mwanaume before sex hakikisha kwanza kabisa mwanamke anafeel moyoni, mnapendana ili kwamba hata usipofanya vyema, atakuvumilia kipindi ambacho wewe unatafuta solution ya kuwa vyema. Mtu akikupenda atavumilia, hatoweza kuondoka kwako. Pili, wakati wa tendo, hakikisha akili yako imetulia, baada ya hapo tumia muda mwingi kumuandaa mwanamke, muandae haswa even for 5 to 8 minutes au hata 10.

Ukianza sex epuka sana kupush kwa kasi nenda taratibu sababu ile kasi inavuta msuguano ambao utasababisha wewe umalize haraka.

Ukiona umekaribia kumwaga, haraka chomoa uume, jipe sekunde kama 45 au dakika 1 kisha chomeka tena, ndani ya hiyo dakika 1 itume kwa romance na mambo mengine.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom